Mturutumbi255
JF-Expert Member
- Jun 7, 2024
- 200
- 420
Ilikuwa Jumamosi asubuhi na jua lilikuwa linawaka vizuri. Majirani wa mtaa wa Mjini Ndani walikuwa wanapanga mipango ya weekend yao. Lakini kijana mmoja, anayeitwa Toto, alikuwa na plan ya kipekee kabisa.
Toto alikuwa na sifa ya kuwa na ujanja wa kijinga lakini wenye kuleta matokeo. Alikuwa maarufu kwa kuweza kujipatia vitu bila kutumia hata senti. Siku hiyo, Toto aliamua kuwa leo lazima atapata soda ya bure.
Alifika kwenye duka la mama Kamau, duka maarufu la mtaa ambalo kila mtu alipenda kwenda kununua vinywaji na vitafunio.
"Mama Kamau, vipi leo biashara?" Toto aliuliza kwa sauti ya uchangamfu.
"Hamna shaka, Toto. Vipi nawe?" mama Kamau alijibu, akifurahia kumuona mteja wake mdogo.
"Basi poa, mama. Naomba unifanyie fadhili ndogo. Kuna jamaa ameniambia kuwa anaweza kunilipa soda moja leo, ila hajafika. Naomba tu unipe sasa, nitamlipa akija," Toto aliongea kwa mbwembwe.
Mama Kamau alikuwa na moyo wa huruma, akampa Toto soda moja ya baridi. Toto akaanza kuitupa mdomoni kama hana akili nzuri, akifurahia ujanja wake.
Wakati anapiga shoti ya mwisho ya soda, akasikia sauti ya mama Kamau ikimuita.
"Toto, mbona huyo jamaa yako haji kumalizia pesa? Ulimwambia aje lini?" mama Kamau aliuliza kwa taharuki kidogo.
Toto, akijua amechemsha, alitabasamu na kusema, "Mama Kamau, labda amesahau au ana shughuli nyingi. Nisubiri kidogo tu, lazima atakuja tu."
Mama Kamau akamwambia, "Sawa, Toto, lakini hakikisha anakuja. Hatuwezi kufanya hivi kila mara."
Toto akaondoka pale kwa mwendo wa taratibu, akiwa na mawazo mengi kichwani. Alijua lazima atafute njia ya kumlipa mama Kamau au kujua plan ya siku zijazo.
Sasa hapa ndipo swali linakuja: Je, Toto ataweza kumpata huyo jamaa aliyemlaghai mama Kamau au ataendelea kutumia ujanja wake kupata vitu bila kulipa? Na kama ni hivyo, siku moja atakutana na kiboko wake au ataendelea kutesa?
By Mturutumbi