Madabwada
JF-Expert Member
- May 8, 2009
- 541
- 320
Kwa kweli nimependezwa sana na uwajibikaji wa huyu mama, last week aliamuru kufungwa mara moja kwa shule ya sekondari ya Bundikani huko kibaha baada ya kugundulika wanafunzi wa kidato cha kwanza wanakaa chini, lakini pia jana ameamuru kukatwa mishahara kwa watendaji wazembe wa kisarawe.
Naomba tu isiwe just a move to gain popularity ili baadaye atimize azma yake ya kuwa mbunge (ameshatangaza azma yake ya kugombea ubunge katika jimbo la Kiteto mwaka huu - 2010) na pengine kutimiziwa ahadi nyingine alizoahidiwa baada ya kuukwaa huo ubunge. Binafsi nitafurahi kuona huu moto aliouanzisha basi awe ana maanisha. Kwa sasa nakupa hongera mama lakini ......!!
Naomba tu isiwe just a move to gain popularity ili baadaye atimize azma yake ya kuwa mbunge (ameshatangaza azma yake ya kugombea ubunge katika jimbo la Kiteto mwaka huu - 2010) na pengine kutimiziwa ahadi nyingine alizoahidiwa baada ya kuukwaa huo ubunge. Binafsi nitafurahi kuona huu moto aliouanzisha basi awe ana maanisha. Kwa sasa nakupa hongera mama lakini ......!!
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Hajjat Amina Said, sasa ameamua kutoa makucha yake dhidi ya watendaji wazembe ambao amedai kuwa ndio wanaokwamisha maendeleo ya mkoa huo na si kukosekana kwa fedha kama inavyodaiwa na baadhi ya watendaji.
Mkuu huyo alifanya hivyo juzi akiwa wilayani Kisarawe, ambako aliaamuru watendaji sita wa halmashauri ya wilaya hiyo, wakatwe asilimia 15 ya mishahara yao kwa kipindi cha miezi miwili, ikiwa ni adhabu kwa kosa la kuchelewesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Watendaji hao ambao wataanza kukatwa mishahara yao kuanzia mwezi ujao ni pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Alquin Ndungwi.
Wengine ni Ofisa Elimu ya Msingi wa Wilaya ya Kisarawe, Winifrida Mbuya, Ofisa Elimu ya Sekondari Donard Chavila, Ofisa Afya Dk E. Helela, Mhandisi wa Wilaya Ayoub Myaule, Ofisa Mipango, Deus Mbalamwezi, na Mweka Hazina, Isaya Moses.
.
Mkuu huyo wa mkoa alitaja baadhi ya miradi iliyokwama kutokana na uzembe wa watendaji hao kuwa ni ile ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari za kata, zahanati na ukosefu wa madawati, jambo linalosababisha wanafunzi kuketi sakafuni.
Hijat Amina alitoa agizo la kukatwa sehemu ya mishahara watendaji hao katika kikao chake cha majumuisho ya ziara ya siku moja aliyoifanya wilayani humo, ziara iliyokuwa na lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kimsingi, wilayani hiyo imeshindwa kutekeleza ipasavyo ilani hiyo.
Alisema serikali ilikwishapeleka fedha za miradi katia vipindi tofauti vya kuanzia Julai mwaka jana na kwamba alichogundua ni kwamba watendaji hao kila mmoja kwa nafasi yake, alikaa nazo hadi Februari na Machi mwaka huu, walipoamua kuzipeleka kwa wananchi.
Mkuu huyo alisema kitendo kukalisha fedha hizo kwa muda wa miezi sita bila kufika kwenye miradi, kinaashiria kuwa zilikuwa zinahifadhiwa katika akaunti za watu binafsi kwa lengo la kupata faida.
"Hapa msinieleze kitu,katika taarifa mlioniletea, mmeonyesha miradi imekamilika sasa leo nimeamua kupita na kujionea hali halisi kuwa nyie ni waongo, na mmeidanganya serikali katika hili simfumbii macho mtu wala sitajali cheo chake,"alisema Mkuu wa wilaya.
Katika ziara hiyo kiongozi huyo alitembelea shule tano za sekondari za kata za Gongoni, Makulunge, Msimbu, Mfuru na Kibuta.
Hijat Amina alielezwa kuwa kwa pamoja shule hizo zina madawati 120 tu kati ya madawati 640 yanayohitajika.