profHarryEnock
Member
- Dec 18, 2023
- 15
- 31
Mimi ni msomi mwenye PhD ya Saikolojia kutoka Makerere University, Uganda na pia nina msingi wa uchumi nilioupata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Licha ya maarifa haya, sijawahi kuajiriwa na serikali, na si kwa sababu sina uwezo, bali kwa sababu serikali nyingi hazipendi kutumia watu wenye independent thinking. Wanahitaji watu wa "ndiyo bwana", si watu wa kuuliza maswali na kuchambua hoja kwa critical lens.
Kitu cha kushangaza zaidi, ni kwamba serikali yenyewe ndiyo iliwashawishi vijana waingie vyuoni, ikawapimia mitihani, ikawapa mikopo, ikawahakikishia better future... lakini leo hii vijana hao wamejaa mitaani, wakiwa na vyeti lakini hawana mwelekeo wa maisha. Wengi wanaishi na wazazi, wengine wamekata tamaa kabisa.
Serikali haiwezi kuendelea kuzunguka mduara huu wa ahadi zisizotekelezeka. Kama kweli tunataka kuondoa tatizo la ajira, hatuwezi kuendelea kufundisha watu "kupita mitihani" bila kuwapa skills halisi za maisha. Tunahitaji elimu inayowajenga vijana kuwa problem solvers, innovators na value creators. Siyo tu watafuta kazi.
Watanzania hawana tatizo la uvivu. Wanachokosa ni mfumo unaowapa nafasi ya kujitegemea. Access to capital, elimu ya biashara, teknolojia sahihi na mazingira ya kupumulia bila kubanwa na tozo na urasimu visivyoisha.
Kama serikali inataka kuona mabadiliko, basi isimamishe sera zinazozungumzia ajira kwa maneno tu. Ianze kusikiliza wasomi walioko mitaani. Wapo wenye uwezo mkubwa wa kuchangia ideas, lakini hawapewi nafasi kwa sababu siyo sehemu ya mfumo wa political favoritism.
Kama taifa halitathubutu kufanya paradigm shift, basi vijana wataendelea kuwa na hasira, kutengwa, na hatimaye kulipuka kiakili na kijamii.
Tusipofumua mfumo wa elimu na ajira, tutajikuta tunafuga tatizo kubwa kwa kizazi kijacho. Siku ya kubadilika ni leo. Kesho itakuwa too late.