Ujasiri wa Rais Magufuli katika vita dhidi ya Corona umeleta matumaini kwa Watanzania

Ujasiri wa Rais Magufuli katika vita dhidi ya Corona umeleta matumaini kwa Watanzania

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2019
Posts
223
Reaction score
202
Hatuwezi kilinganisha Tanzania na nchi kama China, US, UK na Italia katika nyanja ya miundombinu ya huduma za Afya.Pia hatuna uhakika kuwa ni lini ugonjwa huu wa Corona utapata tiba au chanjo. Pia ni wazi kuwa hatuwezi kuendelea kuwa na watu waoga ambao wanajifungia kutokufanya kazi kukabiliana na changamoto ya ugonjwa. Kwa nchi zilizojifungia inakua vigumu kujifungulia kwani ni lazima upime wananchi wako wote ili kuwa na uhakika hakuna maambukizi ambayo yatarejesha ugonjwa.Hakuna nchi yeyote Afrika na duniani ina uwezo wa kufanya vipimo kwa watu wake wote.

Hotuba ya Raisi Dr.John Magufuli ya tarehe 03 May 2020 ilikua ni hotuba ya kiongozi wa wanachi, baba kwa watoto wake kwani ilileta matumaini mapya kwa wanachi kutokana na janga linaloikabili taifa na dunia la ugonjwa huu wa corona. Raisi aliongelea hofu iliyopandikizwa na taharuki iliyopo kwa wananchi,na kuwapa matumaini kuwa serikali inafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wananchi wake wapo salama.

Tunafahamu kuwa majanga makubwa yanapoikumba nchi madhara yanayotokana na janga husika mara nyingi hayawi makubwa ukilinganisha na madhara ya hofu inayosababishwa na lile janga. Hii inathibitika katika majanga mengi ya kidunia kama yale ya vita ya kwanza na ya pili ya dunia,mlipuko wa kinu cha nyuklia nchini Japan na ajali nyingine kubwa na ndogo ambazo zinatutokea katika maisha yetu ya kila siku. Kwa upande wa ajali ndogo kama ni dereva na umeshawahi kupata ajali hata ya kukwaruza gari jingine unaweza elewa vema juu ya hali unayokuwa nayo kwa muda wa siku mbili mpaka tatu.

Utafiti wa kisayansi unaonesha kuwa hofu licha ya kusababisha kifo moja kwa moja inaweza kusababisha magonjwa ya moyo,ini,ngozi,kibofu,matatizo ya kupumua,uwezo wa kufikiri na kadhalika. Ndio maana wahalifu wamekua wakitumia hofu ili kuweza kutekeleza mambo yao,mfano uwepo wa makundi ya kihalifu kama magaidi, umiliki wa silaha za maangamizi,na vitisho vya uvamizi wa kivita,na matumizi ya mitandao ya kijamii kupandikiza hofu katika jamii.

Matumizi ya mitandao kama silaha ya kutia hofu jamiii kwa nchi kama Tanzania yamekua yakiongeza kila kukicha, wanaharakati na wanasiasa kwa malengo yao binafsi wamekua wakipotosha umma kwa kutoa habari za vifo vya watu wanaokufa kwa sababu zingine kuwa wamekufa kwa corona.

Hali hii inaweza kuwasabaishia watanzania wengi kuwa na ugonjwa unaojulikana kwa kitaaluma Nosophobia,huu ugonjwa unawapata watu kutokana na hofu ya kuumwa ugonjwa hatari mfano ugonjwa wa Corona ambao vyombo vya habari vimekua vikiuripoti kuuwa watu wengi.Ugonjwa wa aina hii huweza kuendelea hata pale ambapo umepata vipimo na kujua kuwa huna ugonjwa wa Corona.

Kuwatia hofu wananchi,kutoa taarifa zisizo za ukweli, na kutoa siri za wagonjwa ni aina za uhalifu ambazo pengine wanaotenda makosa hayo wanafahau au hawafahamu. Ila zipo sababu mbalimbali zinapelekea kushamiri kwa uhalifu huu ndani ya jamii kwa lile kundi linalofanya uhalifu huu kwa makusudi, miongoni mwa sababu hizi ni wanasiasa na wanaharakati kutumika na ma adui wa Tanzania, utendaji wa mazoea wa watumishi, ubinafsi na roho mbaya za baadhi ya wanasiasa na wanaharakati.

1. Wanasiasa kutumika
Wanasiasa wa Tanzania tofauti na wanasiasa wa Kenya,Uganda,pamoja na Rwanda wanakosa uzalendo kwa nchi yao na upendo kwa wananchi kwa kuruhusu wadhamini wa vyama vyao kuwatumia kuharibu mustakabali mwema wa nchi yao.Tunafahamu sote kuwa majirani zetu wanakabiliwa na ukabila katika siasa zao,lakini wanasiasa wao linapokuja suala la utaifa huwa mstari wa mbele kuweza kukabiliana na hilo tatizo.
Viongozi wa siasa Tanzania wamekua wakitafuta kunufaika kupitia majanga yanayoikumba Tanzania huku wakiwaacha wananchi katika madhila.Tunakumbuka sakata la serikali na makapuni ya madini,sakata la kushiliwa ndege za Tanzania na mifano kama hiyo mbayo inahitaji kutuunganisha na kuangalia maslahi mapana ya Taifa.

2. Utendaji wa mazoea
Utendaji wa mazoea kwa watanzania unachangia kwa kiwango kikubwa hasa kipindi cha majanga.Uwezo wa kufikiri kwa baadhi ya watendaji umekua changamoto kubwa kiasi cha watendaji kuwa wagonjwa wa kuiga kila kinachofanywa na nchi zingine hata kama kinachofanyika hakiwezekani kwa mazingira ya Tanzania.
Kwenye hili pia tunaona vyuo mbalimbali na taasisi mbali mbali zikiwa zinafanya tafiti kuweza kuja na suluhisho kwa mujibu wa changamoto zilizopo.Vyuo vyetu vimekua vikizalisha wanafunzi na kutumia mamiliaoni ya fedha katika tafiti ambazo hazina tija kwa taifa.Ni muda wa wataalamu wetu kuja na tafiti zinazotoa suluhisho la matatizo yanayowakabili Watanzani.

3. Ubinafsi na roho mbaya
Tunafahamu kuwa wananchi wengi wanachota maji mitoni,wanafuata mahitaji yao nje, wanalipwa kwa siku, na shughuli zao wengi sio rasmi. Kuwafungia wananchi hawa kwa kuwa kiongozi wa upinzani ambaye anamaisha mazuri na ya kifahari yanayomuwezesha kujifungia ndani na familia yake na kuishi zaidi ya mwaka mmoja ni kuwadhulumu wananchi kwa nia ya kumlinda huyu mwanasiasa asipate maambukizi

Ombi Kwa Serikali Kama Mh Rais alivyosema katika hotuba yake kuwa anakusudia kuruhusu ligi ya mpira kuendelea,pia afikirie kurejesha wanafuni pia mashueni kwani kwa sasa watoto mitaani wanacheza na watoto wenzao kama kawaida bila uangalizi wa wazazi,kama ni suala la maambukizi linafanyika watoto wakiwa nyubani. Hivyo kuendelea kufunga shule pamoja na shughuli zingine ni kulitatua tatizo kwa mbinu ambay sio sahihi.

Serikali pamoja na wale wanaoitakia nchi mema waendelee kuondoa hofu kwa wananchi na watu warejee katika shughuli zao za kila siku huku wakichukua tahadhari kama wanavyochukua tahadhari katika magonjwa mengine. Nchi ya Taiwan haikufunga nchi ila ilifuata taratibu za kiusalama ili kuiokoa jamii yake na ugonjwa huu.

Hivi sasa nchi nyingi ambazo zilifungia watu wake ndani kama Uhispania zimekumbwa na madhara makubwa kuliko vifo vya corona katika nchi hizo na kuamua kuwaruhusu watu wake watoke kwa sharti la kuvaa barakoa.

Vita hii haiwezi kupiganwa uchumi wa nchi ukiwa chini, vita hii haiwezi kupiganwa kwa wananchi kufungiwa ndani,vita hii haiwezi kupiganwa kama tafiti hazifanyiki.

Mungu Mbariki Rais wetu, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
 
Bado nitaendelea kusema kwamba Mtaji Mkubwa wa Magufuli ni Jeshi Kubwa la Wajinga waliopo nyuma yake! There's no way mtu anayejitambua akashangilia kutombiwa ukweli kuhusu status ya gonjwa lenye uwezo wa kuua familia yake yote within a week! Yaani unashangilia kuwekewa mazingira ya "...kufeni tu kuliko kuwaambia ukweli utakaothiri kumalizika kwa SGR"!

Wekati nyie mnatengenezewa mazingira ya "kufeni tu" mwenzenu kajificha Chato manake anafahamu akiwa Dar es salaam atalazimika kukutana na wageni mbalimbali na kumweka kwenye risk ambayo hajali nyie kuwa nayo lakini bado mnashangilia kama mazuzu!
 
Rais Magufuli ni nahodha bora

Mungu aendelee kumpa siha njema
Nahodha chombo kimeyumba kidogo kachumpa na boya, na sasa yuko chini ya mnazi anavuta fegi huku anakiangalia chombo kinavyopata dhoruba, huku akiwaambia abiria waombe Mungu! aisee tuna nahodha wa ajabu haijawahi kutokea duniani! 🤔 😅
 
Mimi nazika ndugu zangu kila siku ujasiri upi?Usinichefue kabisa
 
Nahodha chombo kimeyumba kidogo kachumpa na boya, na sasa yuko chini ya mnazi anavuta fegi huku anakiangalia chombo kinavyopata dhoruba, huku akiwaambia abiria waombe Mungu! aisee tuna nahodha wa ajabu haijawahi kutokea duniani! 🤔 😅
Hujui serikali ni nini wewe
 
Bado nitaendelea kusema kwamba Mtaji Mkubwa wa Magufuli ni Jeshi Kubwa la Wajinga waliopo nyuma yake! There's no way mtu anayejitambua akashangilia kutombiwa ukweli kuhusu status ya gonjwa lenye uwezo wa kuua familia yake yote within a week! Yaani unashangilia kuwekewa mazingira ya "...kufeni tu kuliko kuwaambia ukweli utakaothiri kumalizika kwa SGR"!

Wekati nyie mnatengenezewa mazingira ya "kufeni tu" mwenzenu kajificha Chato manake anafahamu akiwa Dar es salaam atalazimika kukutana na wageni mbalimbali na kumweka kwenye risk ambayo hajali nyie kuwa nayo lakini bado mnashangilia kama mazuzu!
Maandishi haya yamenionesha kiwango cha upumbavu wako, mama yako ana kazi sana.
 
Hata Kinjekitile aliwapa ujasiri wale wajinga wake. Kila zama zina wajinga, na zina viongozi wa kuwapekelesha wajinga.

Usisahau pia mzee Kinje bado yuko Chato anaogopa Corona.
 
Maandishi haya yamenionesha kiwango cha upumbavu wako, mama yako ana kazi sana.
Vp dadangu, unawashwa na kwahiyo unatafuta basha kwa nguvu, au una frustration za kuletewa nyumba ndogo na mumeo?! No way... let me guess! Itakuwa ni frustration za kuingiliwa kwa nguvu kinyume na maumbile na mumeo!
 
Mungu akubariki sana ndugu yangu, acha watu wakutukane lakini umefanya kazi yako, umeandika umemaliza, na maandishi yameshiba, sijaona ushabiki wa kisiasa katika andiko lako bali umeandika ukweli, kazi uliyoifanya ni kubwa na Mungu atakubariki.
 
Bado nitaendelea kusema kwamba Mtaji Mkubwa wa Magufuli ni Jeshi Kubwa la Wajinga waliopo nyuma yake! There's no way mtu anayejitambua akashangilia kutombiwa ukweli kuhusu status ya gonjwa lenye uwezo wa kuua familia yake yote within a week! Yaani unashangilia kuwekewa mazingira ya "...kufeni tu kuliko kuwaambia ukweli utakaothiri kumalizika kwa SGR"!

Wekati nyie mnatengenezewa mazingira ya "kufeni tu" mwenzenu kajificha Chato manake anafahamu akiwa Dar es salaam atalazimika kukutana na wageni mbalimbali na kumweka kwenye risk ambayo hajali nyie kuwa nayo lakini bado mnashangilia kama mazuzu!
nyinyi wapumbavu,afadhali wajinga waliopo nyuma ya magufuli.

Magu anazungumza kama mtanzania lakini anaishi kama rais wa jamhuri,ulitaka aende na wewe buguruni kusubiri ndizi zinazoshushwa na fuso kutokea moshi!!!

kama nawewe ni rais,rudi kwenu kajifungie,kama unajua huli pasipo kutoka,bro acha kuandika ujinga,hiki ulichoandika hata nafsi yako haikipendi,ila sababu tumbo ndio limekaimu madaraka ya kichwa kwa muda,kila kitu kimesimama mwilini mwako.

wabunge wenu walivyo wanajua kwamba nyinyi ni manugu,wanataka muwaunge mkono,wakati hata kurudisha wasichokiingiza wamekataa,uone kama wana hawafanyi kusudi wangejua kama wao ni waajiriwa tofauti na nyinyi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikijaribu uangalia comment za watu wanaopinga hili andiko naona upeo wao,wanatumia hii platform kama zinavyotuika facebook...Nadhani ni vizuri mkaheshimu hii platform na mkaitenea haki kwa kujadili mambo kwa hoja
 
Back
Top Bottom