Napenda Kutumia Fursa Hii Kuwajuza Wale Wanaotaka "kujaribu" Ujasiriamali Kwamba Hiyo Ni Moja Kati Ya Wazazi Wa Matatizo Na Changamoto Lukuki! Ukitaka Kufanya Ujasiriamali Ufanye Tu Kwa Moyo Mmoja, Na Si Kujaribu; Na Kama Ukihisi Uwezi Basi Ongeza Juhudi Katika Mambo Yako Mengine Utafanikiwa Vyema Tu. Hata Kama Una Mtaji Wa 100,000/= Tu Amua Kuwa Committed Na Uwe Serious Kweli, Utarudisha Mtaji Wako Wote Na Kupata Faida Lukuki (kipato, Ajira, Uhuru, Muda N.K.). Jiandae Kwa Changamoto Mbalimbali ( Loss, Overworking, Kodi, Hali Ya Hewa, Wateja Wasumbufu, Bidhaa Kuharibika, Mtaji Kupungua Au Kukata, Muda, Price Fluctuations, Sheria Za Nchi HII N.K.) Na Ukaze Msuli Kweli Huku Ukizipatia Changamoto Zote Ufumbuzi Wa Kudumu. Omba Mungu Kwa Imani Thabiti Na Uchape Sana Kazi Hadi Upate Mafanikio Uliyokuwa Unayataka. Ukiingia Kwa Kujaribu Ndugu Yangu Jiandae Kushindwa Changamoto Na Kubwaga Manyanga. Kwa Leo Naomba Niishie Hapa.