Ujasiriamali: Miliki kiwanda kidogo cha sabuni kwa mtaji mdogo

Ujasiriamali: Miliki kiwanda kidogo cha sabuni kwa mtaji mdogo

shago

Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
50
Reaction score
47
Habari wadau wa JF.

Kutokana na kaulimbiu ya nchi yetu ya Tanzania ya Viwanda leo nataka kuwapa funzo/mafunzo ya jinsi ya kutengeneza sabuni za kipande au kufulia.

Jiulize wewe uliyekuwa Katavi, Simiyu, Songea, Songwe, Shinyanga nk mikoa mbalimbali uliwahi fikiria fursa hii kwanini unasubiri sabuni mpaka itoke jijini Dar es salaam, mpaka ikufikie huko wakati hapo ulipo wewe ukiwa tayari unaweza kuanza kudahalisha bidhaa hii muhimu kwa binadamu na kutumia malighafi zinazokuzunguka.

Fikiria sasa jiongeze kibiashara zaidi kwanini unachelewa, hata wenye viwanda vikubwa leo walitoka chini na kufika huku walipofika mpaka unaipata bidhaa huko uliko.

Embu tuone malighafi na vifaa vitumikavyo.

Malighafi za sabuni:

MAFUTA
Asikwambie mtu katika sabuni 80% ni mafuta yenye asili ya kuganda mfano mawese,nazi, mise, nk.

CAUSTIC SODA
Hii ni kemikali inayofanya kazi ya kuibadilisha mchanganyiko wa mafuta na kuwa sabuni sasa na kazi kubwa hii ya kemikali kwenye sabuni ni kuleta povu, kuitakatisha nguo.

SODIUM SILICATE
Kazi ya kemikali katika mchanganyiko wa sabuni yako ni kuondoa muwasho kama utazidisha kiwango cha Caustic Soda hupelekea kuwa kwa sabuni, kemikali hii huondoa muwasho, na kuifanya sabuni kuwa ngumu kutowahi kuisha kwa haraka.

PAFYUM
Hii kaz yake kuleta harufu nzur katika sabuni yako nzuri uliyoitengeneza.

Vifaa vitimikavyo:
• Lazima uwe na pipa, ndoo, chombo kikubwa cha kukorogea sabuni yako.
• Lazima uwe na box la kugandishia sabuni, la chuma au la mbao.
• Unahitaj uwe na meza ya kutatia sabuni yako.
• Nguvu kazi ya kuanzia watu wawili
• Muhuri wa chapa ya sabuni yako kama utahitaji pia.

Katika mchanganyiko wako wa sabuni lazima uendane kwa malighafi zako kwa maana ratio za uchanganyaji wa mafuta, caustic soda nk, ziwe sawa.

Njoo nikufundishe uanze sasa kutengeneza na kupeleka mzigo sokoni. Nakufundisha kwa vitendo hapo hpo ulipo na ikitokea sabuni umeharibika nitakurudishia gharama zako za malighafi

Soko lake ni kubwa kwa maana usambazaji wake katika maduka makubwa mpaka maduka ya mtaani kwako (kwa Mangi).


Chini ni pichaa za baadhi ya wanafunzi ambao niliwafUndisha na kurejesha mrejesho walichokifanya.

Shukran sana, karibuni

IMG_20191114_121221.jpeg
IMG_20191113_125006.jpeg
IMG_20191114_124508.jpeg
IMG_20191114_121204.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo mtaji mdogo unaotakiwa ni kama kiasi gani?
Mkuu karibu kwanza upate mafunzo afu ndio ujue uanzee na kiasi gan, siwez kukwambia uwe na kiasi gan wakat sijajua uko wap na gharama za material kwa uko uliko zinapatikana kwa gharama gana kwaiyo kikubwa naomba upate kwanza mafunzo ya jinsi ya utengenezaji afu sasa ndio baadae ujue unawekeza kiasi gan,karibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiasi kinatosha kuanzisha hicho kiwanda?
Mkuu neno kiwanda kisikupe dhana kubwa sana kwamba ni lazm uwe na kiasi kikubwa hapana , kikubwa kwanza unahitaj mafunzo kwanza ya utengenezaj ili ujue gharama za malighafi na sehem ulipo upatikanaj wake ndio sasa uanze kujadil hapa naweza kuwa na kiasi gan cha kuanzia kutoka na soko lako la mahal hpo, mm siwez kukwambia kwa mfno, uanze na mtaji wa kiasi fulan wakat bdo hauna mafunzo ya elimu, so gharama ya mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa hii natoa kwa shs 10000 tu, nakufundisha kwa nazalia na kitendo hapo hapo mpk kinapatikana kitu tulichokikusudia kwa mda huo,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mafunzo natoa kwa njia ya simu nakufundisha nadhalia na kwa vitendo na tunafanya hapo hapo nakwambia uandae malighafi ukiwa tayar tunaanza somo, hapo hapo tunachanganya wote, hatua ya kwanza mpk ya mwisho ya sabuni, wala hakuna ttzo,karib mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mali ghafi zinapatikana wapi ili niwe na uhakika wa kupata Mali ghafi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unaweza kunitafutia soko mimi takuletea sabuni unaonaje ?

Yaani mimi nitengeneza kama ulivyonifundisha nilete kwako nikuuzie ili wewe usambaze koote huko uliposema tutengeneze pesa pamoja
 
Nianze kukushukuru sana mkuu Shago kwa kujitolea kushare nasi elimu hii mhimu ktk ujasiliamali. Swali mkuu ww uko mkoa gani?
 
Sehemu pekee inayolipa kwa kutengeneza sabuni in kyela na kigoma kwingine bora uagize au uwe na mtaji mkubwa.Watu wengi wamefeli kwenye utengenezaji was sabbuni kwa sbabu malighafi no ghali
 
Kama unaweza kunitafutia soko mimi takuletea sabuni unaonaje ?

Yaani mimi nitengeneza kama ulivyonifundisha nilete kwako nikuuzie ili wewe usambaze koote huko uliposema tutengeneze pesa pamoja
Mkuu biashara ni mapambano ,kuhusu soko ww usiliogope ,soko lipo nankubwa tu kwa maaana ya walaji ila km utakuwa na wasiwasi huwez kulipata soko, kingne mm nitakusaidia kwa kukupa mkakati jinsi gan utaingiza sabun zako sokon utumie njia ipi, hilo nitakusadia kukuongezea maarifa kidogo juu ya soko, na jinsi ya kuliingia,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu pekee inayolipa kwa kutengeneza sabuni in kyela na kigoma kwingine bora uagize au uwe na mtaji mkubwa.Watu wengi wamefeli kwenye utengenezaji was sabbuni kwa sbabu malighafi no ghali
Si kwel mkuu, unataka kusema mafuta ya mawese yanapatikana kigoma na kyela tu, hapana mkuu mafuta ya mawese yanapatikana sehem kubwa tu tanzania, pia kuna mafuta ya nazi, kuna mafuta ya wanyama, nk kwaiyo kufel kwa wanaujasiriamali ktk sabuni kuna mambo mengne meng hasa la ukosefu wa elimu ya uendelevu wa biashara zao hii ndio ishu kubwa sbb nmewashudia weng wakidondoka lkn baada ya kupata elimu ya jinsi ya kuifanya biashara ako iwe endelevu waliinuka na kusonga mbele,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boss am interested na hii business naweza vp kupata elimu na mafunzo juu ya hii business kutoka kwako.
 
Back
Top Bottom