Ujasiriamali: Usindikaji wa Yoghurt na Mtindi

Asante kwa kunikumbusha kaka.
Nitaziweka mwishoni mwa topic,
 
UTENGENEZAJI WA YOGHURT Part2

Kabla sijaenda moja kwa moja kwenye utengenezaji wa Product hii pendwa toka kwenye maziwa, nataka niwape hints ambazo ni muhimu kuzingatia ili uweze pata Yoghurt nzuri na bora.

1. Ukaguzi wa ubora wa maziwa
Ni muhimu kukagua kama maziwa uliyonunua yanakidhi ubora.
Baadhi ya ukaguzi unaohitajika kwa level ya kawaida ni kama zifuatazo.

i. Kukagua kama Maziwa uliyonunua yame chakachuliwa(Yameongezwa maji).
Tambua kwamba maziwa yakiongezwa maji huaribu ubora wake na kuathiri upatikanaji wa Yoghurt bora.

Maji hufanya maziwa kuwa mepesi na pia kusababisha yogurt kuwa nyepesi au yenye maji. Pia maji yanaweza kuwa na bacteria wengi hivyo kusababisha kutoganda kwa maziwa na kufanya yoghurt iliyo jitenga maji.

Hivyo nilazima ufanye ukaguzi ili kujua kama maziwa yako yameongezwa maji au la.

ii. Kujua kama maziwa yamesha chacha.
Maziwa yakisha anza kujichachisha yenyewe basi huwezi pata yoghurt nzuri.
Hapa unaweza kugundua kwa njia ya kawaida ya nyumbani. Chukua Kijiko cha chai chota maziwa kidogo, kama robo kijiko, then weka kijiko juu ya mshumaa unao waka. Ukiona maziwa yamejitengeneza vibonge vibonge vidogo kama vya mtindi basi maziwa yako yameharibika, hivyo hayafai kutengeneza Yoghurt.

Ukiona maziwa yako yanachemka kawaida bika kutengeneza vibonge basi maziwa yako yapo safi.

iii. Ukaguzi wa harufu na ladha.
Ni vizuri ukatumia Milango ya fahamu/sense organs kutambua ubora waaziwa. Hapa tuna angalia harufu na ladha. Kumbuka kuna maziwa mengine hukamuliwa katika hali ya uchafu au kuhifadhiwa kwenye chombo kichafu. Unakuta maziwa yana shombo ya kinyesi cha Ng'ombe. Pia maziwa wengine huweka madawa ya kienyeji ili yasiharibike.
Hivyo kwa kutumia macho, ulimi na pua unaweza kugundua utofauti huo.

TUTENGENEZE YOGHURT SASA.
Hakikisha kabla hujaanza una vitu vifuatavyo.
*Maziwa, Moto(jiko), Sufuria ya kuchemshia, mwiko wa kukorogea

*Thermometer kupimia jotoridi

*Sukari kwa ajili ya kuongeza utamu/ ingawa sio lazima

*Flavour kama vanilla, Strawbarries nk zinapatikana supermarket kwa bei nafuu, vichupa vidogo ni kama Tsh 600-1500.

*STARTER CULTURE- (Yoghurt culture contain these two symbolic bacteria Lactobacillus bulgaricus na Streptococcus Thermophillus) Hii ndio itatusaidia kugandisha maziwa yetu. Ni bacteria maalumu ambao wapo kwa wingi, kwa ajili ya kugandisha maziwa.
Hapa unaweza nunua ya kisasa. Zinapatikana ofisi ya PROMACO pale Kamata Opposite na Nakumati Supermarket , Nyerere Rd. Inauzwa 20,000 ipo kwenye Pakti, na unaweza kutumia kugandishia mpaka Lita 500 za maziwa. Kiasi utakacho tumia inategemea na kiasi cha maziwa. Ipo kama chengachenga.

Pia unaweza tumia Starter Culture ya kienyeji, nayo inatoa Yoghurt safi kabisa. Hii ni Yoghut ambayo ipo tayari. Yani unaweza nunua Yoghurt ya dukani au mtu ambae ameitengeneza.

HATUA ZA UTENGENEZAJI.
i. Chemsha maziwa kwa joto la 85-90 centigrade. Wakati unachemsha hakikisha unakoroga kila wakati ili kupata Yoghurt nzuri, na pia kuepusha kuungua chini.

Tunachemsha ili kuua Bactetia, enzymes, na virus. Pia kuongeza uzito na ladha ya yoghurt.

ii. Pooza maziwa kwa joto la 42-43 centigrade. Weka kwenye Ndoo safi iliyo safishwa kwa maji ya moto sana, ili kuuwa bacteria waliopo. Hapa ndipo unapaswa kuhakikisha maziwa yapo kwenye joto hilo la 42 au 43, ukikosea basi Hutopata Yoghurt, au yoghurt yako itachukua muda mrefu. Unaweza yapooza kwenye Dishi kubwa lenye maji baridi kushusha ile Temperature 90 centigrade hadi 42-43centigrade. Yakisha fikia joto hili 42 au 43 centigrade unayaondoa.

Tunapooza kwa hiyo temperature ili kuwezesha culture tutakayo iweka waweze kugandisha vizuri . Kumbuka Starter culture ina bacteria maalumu kwa kugandisha maziwa, na joto hilo ndio hufanya kazi vizuri kwa kuitafuna ile sukari ya maziwa na kufanya maziwa kuganda (Rejea maelezo ya nyuma).

iii. Weka Starter Culture 2% ya maziwa. Hapa nazungumzia Starter culture ya kienyeji, yani yoghut iliyotayari ndio unachanganya na haya maziwa kwa 2%. Yani kama
maziwa yako ni lita 10 (10,000 ml) (ndoo ndogo) basi unapaswa kuweka Culrture kile kikombe kidogo cha chai ambacho ni 200ml (0.2L), hala ndio 2%inapatikana. Culture ndio hutumika kugandisha maziwa kwa haraka (3hrs).
Funika maziwa kwa saa 3 yangande.

iv. Koroga na yavundike kwa joto la 42 au 43 centigrade

v. Baada ya masaa matatu(3hrs) yataganda, hivyo haraka sana yaweke kwenye freezer au Friji lenye ubaridi mkali. Lengo ni kuwapooza wale bacteria ili wasifanye kazi. Kwa joto la 0 hadi 4 centigrade bacteria hawa hupooza na kushindwa kuendelwa kuchachusha maziwa. Hapa tunafanya hivi ili Yoghurt yetu isiwe na uchachu mkali. Hii Process ndo tunaita Rippening/ kuiva kwa Yoghutt. Iweke kwenye Friza kwa muda wa masaaa nane (8hrs).

vii. Baada ya masaa 8, Ondoa Yoghut yako kwenye friza. Hapa unaweza kuondoa kiasi kingine cha Cultute kwa matumizi ya kugandisha maziwa wengine baadae. Hakikisha chombo cha kuhifadhia culture ni sterile au kisafi.

vi. Unaweza weka sukari na flavour. Sukari ni 4% ya maziwa. na Flavour ni kijiko kidogo tu.

Vii. YOGHURT YAKO IPO TAYARI.
Hapa unaweza kuiuza unavyotaka, kama ni kwa kupak kwenye nylon plastic au cup ni sawa tu. Au ukiamua kuuza kwa glass ni sawa pia.

NOTE MUHIMU.
Yogurt ni Cold chain Product, ni bidhaa inayo hitaji ubaridi muda wote. Hivyo unapaswa kuiweka kwenye Friji, ila isigande kuwa barafu. Usipo iweka kwenye ubaridi basi kumbuka wale culture wataendelea kuchachusha na kuifanya mtindi kuwa mchachu zaidi.

VITU VINAVYOSABABISHA YOGHURT ISIGANDE.
1. Starter Culture imechoka/ yani hapa culture imetumika kwenye chain ndefu sana. Pia culture kuvamiwa na virus (Bacteriophage)

2. Maziwa yametoka kwenye Ng'ombe mgonjwa au ambae yupo kwenye dozi za dawa. Dawa zile huingia kwenye maziwa yake hivyo huja kuua culture.

3. Vyombo vimesafishwa ka sabuni ya Unga. Sabuni ya Unga huwa haiondoki kwa haraka, hivyo huuwa Culture. Hivyo ni vizuri ukatumia sabuni ya kipande kwenyenuoshaji.

4. Joto la kughandisha halipo sahihi

FAIDA ZA YOGHURT.
i. Yoghurt ina Calcium nyingi hivyo husaidia mifupa kuwa imara

ii. Umeng'enywaji wake ni rahisi mwilini. Pia husababisha chakula kumeng'enywa kwa haraka. Kama umeshiba sana kunywa Yoghurt isiyo na sukari

iii. Ni nzuri kwa watu ambao wanatatizo la LACTOSE INTOLERANCE. Watu ambao hawanywi maziwa fresh

iv. Inapambana na bacteria kibao mwilini hivyo kuepusha magonjwa ya kuharisha na kuumwa tumbo

v. Inapunguza vitambi, kuondoa kichefuchefu.

vi. Protein iliyopo kwenye yoghurt inasaidia kuongeza kuvu za kiumee
[emoji7][emoji7][emoji7][emoji7][emoji7][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji8][emoji8]

TUNYWE YOGHURY KWA FAIDA YA AFYA ZETU.

Nakaribishwa maswali.

Somo litakalo fuata ni Utengenezajinwa Mtindi(Cultured milk au maziwa Mala.)

Karibuni
 
CC General Mangi dame Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena @Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss deejay Nasmile gkileo JUMA Chief mangi flani hivi Ngongo makaveli10@KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo Jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo @Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa MyM 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 erick The Future nancy1983 Bulah binsaad @Fazzaly@ the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton GEORGE betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi madame @B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA @adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o @naan ngik-@kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great EMANUEL r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto CUTE kawombe zinginary @MLALUKO Jr Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody King Easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys Muhunzi Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph @Theory honey@ Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo @kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria @hambiliki Mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie @1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE Abuu @garcia @Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz papaa azonto Msemachochote mdomo BAKULI tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL kareem @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu@ nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto CUTE Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden<br /><br /><br />bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya SITAKI ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell toyota @escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel Ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 Ngushi ANATORY Antony ukhuty chris van chicha auxillius GOMA son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo @Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin @mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer heavy METAL KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck mshana julius Darcy Denis @Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed shaban Middle @east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa @gambada YNWA ney kush Al-Watan
The bold, Valentina, Miss Natafuta, Paprika,
 
Mkuu somo lime endelea.
 
Mkuu, umesema kwenye kutengeneza Yogurt, unapooza maziwa toka centigrade 90 hadi 42-43, halafu ndo unaweka starter culture, na kuwa mchakato wa maziwa kugeuka kuwa yogurt unachukua saa 3, na hao bakteria wanaohusika wanafanya kazi kwny joto hilo la 42-43 centgrd.. Sasa je, unafanyaje ili maziwa yakae na hilo joto kwa muda wote huo wa masaa 3 bila kupoa zaidi ili bakteria waendelee kukamilisha kazi?
 
Swali zuri kaka, na unaonekana upo makini.

Kwanza kabisa katika maeneo ya joto kama Dar, Tanga mjini, Moro mjini kwa muda wa masaa 3 kwa joto hilo maziwa hayawezi shuka kwaraka sana, labda iwe ni kipindi cha baridi. Hivyo unaweza changanya Culture na maziwa yako kwa hilo joto na yakaganda ndani ya masaa 3 bila hilo joto kushuka.

Kwa zile sehemu zenye ubaridi kama Lushoto, Iringa, Makambako, Mbeyya Part 1 ya somo la yoghurt nilosema unapaswa kuwa na incubator. Hiki ni chombo ambacho kina maintain temperature constant ukisha iseti. Zinatofautiana ukubwa. Kwa matumizi ya kibiashara unapaswa unjengewe chamber au ununue zile kubwa ambazo utaweka culture, maziwa, sukari, flavour kwenye package una seal then unaweka kwenye incubator, baada ya masaa 3 unapunguza temperature mpk 0-4.

Lkn kwa mtaji midogo najua ni ngumu kuimudu hiyo incubator, hivyo unapaswa kufanya kama ifuatavyo kwa sehem zenye baridi

1. Chemsha maji mpaka temperature 43
.2. Weka maji hayo kwenye chombo kikubwa ambacho kitaweza beba chombo ulichoweka maziwa na culture.
3. kazi yako itakuwa kuhakikisha maji ya nje temperature yake haishuki chini ya hapo kwa kuongeza ya moto pale inalotokea temperature inashuka.

N.B Pia niwakumbushe kufunika maziwa hayo baada ya kuweka culture, kwani hewa haipaswi kuingia ndani, na pia joto lisitoke nje.

Karibu
 
nakufuatilia mkuu, tofauti ya yoghurt na mtindi ni ipi? ninaswali jingine linategemea jibu la hapa
Mkuu nikileta uzi wa Kutengeneza Mtindi utaona utofauti wake.

Ila wewe Jua utofauti upo kuanzia kutengeneza mpaka culture zinazotumika.
 
1.Umesema kuna culture ya kisasa je jina lake linaitwaje kwa maana si kila mtu yupo Dar na je zinapatikana kwenye maduka yanayo uza bidhaa gani kwa mfano??

2.(A)Pia kwa uzoefu wako culture za kienyeji ni yoghurt ipi bora kutumia mfano Asas,Tangafresh n.k ipi ni bora??

(B)Pia Yoghurt nyingi zinaradha tofauti je kuna madhara yoyote kutumia radha tofauti wakati wa kuchanganya ,
Mf. Culture yako uliyonayo ni strwaberry ila radha uliyonayo ww ni Vanilla inaweza kuleta effects yoyote kwenye yoghurt utakayozalisha??
 



1. Mkuu Nafahamu sehemu moja tu ambayo inauza Culture. Nenda pale ofisi ya Promaco, ni wakenya hawa. Hii ofisi ipo Pale Kamata opposite na Nakumati Supermarket, Nyerere road. Wewe Mwambie akupe Culture ya Yoghurt. Hizi culture zinatengenezwa na kampuni mbalimbali, hivyo anaweza kukupa Culture za kampuni tofauti tofauti za yoghurt, wewe ndo utachagua. Bei yake ni kama around 30,000/=

2. Sijawahi tumia Culture za hizo kampuni, ila nilikuwa natumia ya yoghurt ya pale SUA. Pia unaweza kwenda SUA ukanunua Mother Culture, watakuuzia kwa bei rahisi tu, sidhan km itafika 3,000. Sema hii mother culture inakuhitaji ujue jinsi ya kuitumia na kuendelea kuhifadhi zaidi.

3. Kwanza hakuna Culture ya Strwaberry. Strwaberry ni Flavour kama Flavour ya vanilla. Culture haileti hizo flavour bali hubadilisha maziwa kuwa yoghurt.

Tunaweka Flavour ili yoghurt iwe na harufu ya kuvutia. Unaweza usiweke Flavour na yoghurt ikawa safi tu, kama utazingatia utaalam.

Karibu.
 
Swali jingine,
Je maziwa toka yakamuliwe yanatakiwa yawe fresh kwa muda gani?? Kwa maana je maziwa yakiyowekwa kwenye friji kwa ajili ya kuhifadhiwa tu lakini bado ni fresh yanafaa??
Maziwa yana uwezo wa kukaa masaa 4 bila kuharibika baada ya kukamuliwa. Ila sasa pia inategemea na usafi(hygiene) katika kukamua. Usafi wa vyombo vyako vya uhifadhi, usafi wa mkamua maziwa, usafi wa chuchu za Ng'ombe n.k

Ukikamua maziwa na kuhifadhi moja kwa moja kwenye Freezer, hata kwa siku mbili yakiwa humo, unaweza kutengeneza Yoghurt yako safi.

Kama hutokuwa msafi maziwa yanaweza kukaa masaa 2 na kuanza kuharibika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…