mcTobby
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 7,894
- 22,679
Kwenye kituo kimoja cha treni ndani mji wa Rotterdam, alionekana mwanaume mmoja akiwa amevalia miwani nyeusi ya jua huku amekamata begi aina ya briefcase mikononi mwake. Bwana huyu kama ungebahatika kumuona siku hii alikuwa ni jamaa fulani hivi mwenye umri wa makamo kama miaka 40 hivi ambaye kwa haraka ungeweza kusema ni profesa wa chuo au mfanyabiashara fulani hivi kutokana na aina ya mavazi aliyokuwa amevalia. Alikuwa ni miongoni mwa abiria wengi waliowasili kwenye mji huu wa Rotterdam wakitokea Paris nchini Ufaransa.
Baada ya kukamilisha taratibu kama abiria wengine kwenye kituo hiki cha treni ,aliondoka moja kwa moja hadi kwenye hoteli ya kifahari jirani katikati ya mji iliyoitwa Rheinhotel kwa ajili ya ku book chumba cha kupumzika. Mgeni huyu alijiandikisha katika hotel hii kwa jina Anton Kunzle raia wa Austria akijitambulisha kama mfanyabiashara. Na ndivyo hati yake ya kusafiria yaani passport ndivyo ilivyomtambulisha.
Baada ya hapo alienda moja kwa moja kwenye ofisi ya posta ili kufungua na kusajili anwani ya sanduku la posta (P.O.BOX)kwa jina hilohilo la Anton Kunzle . Baada ya kukamilisha taratibu zote za posta , moja kwa moja alielekea kwenye benki jirani na hapo iliyoitwa Amron bank kwa ajili ya kufungua akaunti ya benki kwa kutumia anwani aliyoisajili muda mchache uliopita. Na hapo benki aliweka kiasi cha fedha, dola elfu tatu kama amana (deposit)kwenye akaunti yake.
Baada ya hapo alielekea tena kwenye duka la stationery na kununua business cards ambapo alitaka zichapishwe na jina lake pamoja na anwani yake kama Business Manager in Investment Company , Rotterdam kama utambulisho wake rasmi .Alitengeneza business cards kadhaa kwa ajili ya matumizi yake ya baadaye.
Baada ya kukamilisha hili zoezi ,moja kwa moja alienda hadi kwenye ofisi za ubalozi wa brazili ( consulate) hapo mji wa Rotterdam kwa ajili ya kujaza fomu ya ku apply hati ya kusafiri ya Tourist Visa ya kwenda Brazil. Baada ya kukamilisha hakusita , akaelekea tena kwenye clinic moja mjini hapo kwa ajili ya kufanya medical check up kama utaratibu ulivyotaka kwa msafiri yotote yule. Hapo clinic alidanganya baadhi ya Taarifa zake za kiafya ili apewe miwani ya macho yenye magnifying lens ingawaje hakuwa na matatizo ya macho.
Baada ya harakati zote hizi , huyu Anton Kunzle kama alivyojitambulisha alirudi kwenye hoteli kwa ajili ya kupumzika. Asubuhi yake aliamua tena kusafri hadi kwenye mji wa Zurich. Na huko pia alifungua account nyingine kwenye benki ya Suisse ya uswizi kisha akaweka amana ya dola elfu sita. Na hapo aliamua kurudi tena kwenye mji wa Paris.
Punde baada ya kufika tu mjini Paris ,aliamua Moja kwa moja kwenda kwa mtaalamu wa maswala ya urembo , yaani makeup artist kwa lengo la kubadilisha muonekano wake wa usoni . Hapo alitaka awekewe mustachi wa bandia . Kisha akapigwa picha za passport size , akiwa na mustachi huku amevalia miwani yenye lensi aliyoipata kwa daktari. Picha hizi zilimbadilisha muonekano wake kwa ajili ya kutumiwa katika passport yake ya visa ambayo ilikuwa inafanyiwa process kwenye ubalozi wa brazili hapo Rotterdam. Baada ya passport yake kukamilika ndani ya ubalozi , ilipigwa muhuri ambapo pia iliambatanishwa na passport yake ya Austria.
Sasa hapa bwana huyu mchakato ukawa umekamilika wa kupata passport iliyomruhusu kusafiri hadi Brazil kama mtalii. Moja kwa moja huyu bwana hakutaka kupoteza muda ,aliamua kununua ticket ya ndege itakayompeleka Rio de Janeiro Brazil,kisha akifika brazil aende Sau Paulo na kisha tena Aende hadi Montevideo nchini Uruguay.
Katika harakati hizi zote kila alikopita huyu Anton Kunzle alionekana ni mfanyabiashara mkubwa haswa kwa kuwa alikuwa anatoa "Tips", kukodi na kukaa kwenye hotel za gharama na pia kula kwenye migahawa ya bei mbaya. Hii imlimtengenezea " Cover up" au tunaweza sema virtual Cover up kama mfanyabiashara mkubwa haswa kwa kila aliyekutana naye kwenye harakati zake zote hizi alionekana kwake pesa kwake haikua tatizo .
Kiuhalisia huyu bwana sio kwamba alikuwa mfanyabiashara mkubwa kihivyo na wala hakuwa na background yotote kuhusu biashara. Katika harakati zake zote hizi kwenye hii miji mikubwa, huyu bwana alikuwa anajitengenezea Version yake nyingine na kufuta uhalisia wake na background yake kwa ajili ya kazi maalum na nzito iliyokuwa inamsubiri mbele yake ambayo,One mistake atayoifanya ingemgharimu uhai wake na kupelekea kashfa kubwa sana ya kimataifa .
Sasa basi
Huyu Anton Kunzle version yake ya kiuhalisia alikuwa ni jasusi wa mossad (Israel intelligence service) na alitambulika kama Yitzhak Sarid. Nikudokezee jambo , ni kwamba hizi harakati za huyu bwana wakati zinafanyika katika kujitengenezea utambulisho mwingine, ilikuwa ni mwezi September mwaka 1964.
Sasa tukirudi nyuma hadi tarehe moja mwezi huo wa September, huyu Yitzhak Sarid au Anton Kunzle aliitwa kuhudhuria kwenye kikao maalum cha timu ya majasusi wa mossad walokuwepo hapo Paris Ufaransa . Timu hii Majasusi yaani TASKFORCE wa mossad ilikuwa na jina la uficho iliyojulikana kama CAESAREA. Na sehemu waliyopaswa kukutana ilikuwa kwenye nyumba moja ya Siri au "safe house" iliyopo karibu na barabara ya Avenue de Versailles kwenye viunga vya mji wa Paris.
Mkuu wa timu hii ya kijasusi ya mossad yaani operation commander alijulikana kwa jina la Yoske Yariv, jamaa fulani hivi mkakamavu kipande cha mtu ambaye alikuwa ni afisa mstaafu wa jeshi la IDF. Yariv alikuwa ni aina ya wale watu ambao kwa kimombo tunasema "He brooks no nonsense" au kiswahili sanifu ni aina ya mtu "asiyependa utani au ujinga na ha intertain upumbavu.
Huyu yariv baada ya kumuita Sarid au Anton Kunzle,alianza kumpa briefings na maelezo kadhaa kuhusiana na kazi maalum iliyokuwa inatarajiwa kufanyika.
Bwana Yariv alianza kueleza kwamba, serikali ya Ujerumani magharibi(West Germany) kupitia bunge lake lilitaka kupitisha mswada tata wa sheria ambao ulikuwa kiuhalisia unaondoa vikwazo vya kutoshtakiwa kwa baadhi ya raia au viongozi waliokuwa na uhusiano na chama cha Nazi ambao bado wapo mafichoni. Hivyo basi kupitia sheria hii watu hawa ambao walikuwa wamejificha wangeweza kujitokeza na kuendeleza maisha yao ya kawaida bila kuukimbia au kuwa na kinga ya kutoshtakiwa na mkono wa sheria. Hivyo basi huyu bwana Yarid alitaka sheria hii isipitishwe na kuitaka kuikumbusha dunia bado kuna "Monsters" au wahalifu wa Nazi walio wengi na walihusika kwenye mauaji ya Halaiki ya wayahudi na bado wapo mafichoni.
Hivyo kikao hiki kikiongozwa na huyu Yariv,alitaka mtu mmoja ambaye amehusika na mauaji ya wayahudi ambaye bado yupo mafichoni auliwe . Mtu huyu alijulikana kama "The Butcher of Riga". Ambaye Taarifa za kijasusi zilionyesha huyu bwana bado yupo hai na anaishi huko America kusini. Mtu huyu ambaye alihusika na mauaji ya wayahudi elfu 30,000 hakuwa mwingine bali ni mnazi Herbert Curkus mwenye asili ya Latvia.
Na pia mkurugenzi wa Mossad alikuwa ameshatoa ruhusa au green light ya hii operation ya kummaliza huyu Herbert Curkus. Hivyo Yariv alimtaka huyu Sarid au Anton Kunzle ajibadilishe na kuonekana kama mfanyabiashara mkubwa mwenye asili ya Austria kisha aende hadi Brazil kwa ajili ya kumnasa huyu bwana ikwezekana mzima au amekufa. Kivyovyote vile.
Sasa basi siku kumi baadaye yaani tarehe 10 September ,baada ya kikao hiki huyu bwana Sarid au Anton Kunzle kama alivyojitambulisha aliabiri ndege safarini kuelekea Rio de Janeiro Brazil. Ingawaje huyu bwana alifurahia hii safari lakini mda mwingine alijikuta na wasiwasi kutokana na aina hii ya mission . Ukweli ni kwamba alikuwa peke yake ,tena kwenye nchi ya ugenini mbali kabisa na bara la ulaya. Hii iliuwa ina maanisha mission yenyewe ilikuwa na hatari na risk zilikuwa kila mahali. Hivyo kosa dogo ambalo angefanya lingemgharimu uhai wake.
Akiwa safarini ndani ya ndege huyu bwana Anton Kunzle alikuwa akipekua mafaili na documents kadhaa zilizokuwa zinaonyesha Taarifa za huyu mtu anayeitwa Herbert Curkus.wasifu wa Herbert Curkus kwa kifupi ungemtafsiri kama muuaji katili au cold blooded murderer kutokana na alichowafanyia wayahudi nchini latvia wakati akihudumu kama mwanajeshi wa kujitolea wa wa Nazi.
Ukatili wa huyu Herbert Curkus ulikuwa hauelezeki.
Kwa mfano inadaiwa aliamuru wayahudi zaidi ya 100 kuzamishwa kwenye ziwa la maji baridi. Pia alihusika na mauaji ya wayahudi 300 kwa kuwachoma wote ndani ya sinagogi . Pia alikuwa akiua watoto wa kiyahudi kikatili kwa kuwagongesha vichwa vyao ukutani. Baadaye huyu Curkus aliamua kutorokea nchi ya Brazil ili kukwepa mkono wa sheria kwenye mashtaka ya Nuremberg trials baada ya utawala wa Nazi kuanguka
Wasifu huu wa kutisha ulimwogopesha sana bwana Sarid au Anton Kunzle kuhusu aina ya mtu aliyekuwa anaenda kukabiliana naye huko America kusini.
Ni kwamba Taarifa za kijasusi kuhusiana na Herbert Curkus zilionyesha baada ya kukimbilia Brazil alienda moja kwa moja hadi Rio de Janeiro,lakini alitoroka mji huu baada ya jamii za kiyahudi zilizokuwa zinaishi hapo Brazil haswa kwenye mji wa Rio de Janeiro,kumhisi kuhusika na mauaji ya wayahudi kipindi akiwa Latvia. Baadaye akaamua kuhamishia familia yake mjini Sau Paulo na kuanzisha biashara ya Taxi kwa kutumia ndege . Yaani kusafirsha watalii hapa na pale kwenye vituo vya kitalii ndani ya mji wa Sau Paulo ingawaje biashara yake hii ilikuwa na pandashuka kutokana na maisha ya wasiwasi aliyokuwa akiishi. Sasa huyu bwana akawa anaishi kwa wasiwasi na akihisi kwamba instinct zake zilikuwa zinamwambia anawindwa. Hii ni kwa sababu alikuwa ana maadui tayari ndani ya Brazil na alihisi tu one Day atatafutwa na kuuawa.
Sasa basi Anton Kunzle alijua anaenda kukabiliana na mtu hatari sana maana huyu Herbert Curkus hakuwa mchache . Sasa baada ya kufika mji wa Rio de Janeiro , Anton Kunzle kabla ya kuingia kwenye mission rasmi aliamua ku spend siku kadhaa ndani ya mji huu Hususani kwenye fukwe za Copacabana na Ipanema akifurahia uzuri wa Totozi za kibrazil(mulattoes )na misambwanda yao kwenye bikini.😎😎😎 Muda mfupi akiwa kwenye mji huo Alitengeneza mazoea na baadhi ya wazito au tuseme baadhi ya matajiri kadhaa waliowekeza kwenye biashara ya utalii na yeye akijitambulisha kama mfanyabiashara mkubwa kutoka Austria na alikuwa ana nia ya kuwekeza kwenye hii biashara ya utalii.
Pia alijikuta ametengeneza connection hadi na waziri wa utalii kwenye mji huo na mwisho akapewa baadhi ya barua za utambulisho au recommendations letter kwa ajili ya kuziwasilisha kwa baadhi ya maafisa wazito kwenye mji wa Sau paulo kama mfanyabiashara mkubwa na aliye na nia ya kuwekeza kwenye sekta ya utalii. Katika harakati hizi Kunzle alikuwa amepata moja ya anwani ya Herbert Curkus ambaye naye alikuwa ni mwekezaji wa utalii Hususani kwenye Air. Taxi huko Sau Paulo.
Anton Kunzle alifika kweli kwenye mji wa sau paulo , .
Kama mtalii aliamua kutembelea baadhi ya fukwe mjini Sau Paulo,na kwa kuwa alikuwa anajua anwani ya sehemu Herbert Curkus anapopatikana haikumpa shida sana.
Alifika kwenye fukwe moja na kukutana na mrembo aliyekuwa akiuza ticket kwa watalii eneo la ufukwe na kumuuliza mawili matatu kuhusiana na mji wa Sau Paulo.
Mrembo huyu alimweleza Kunzle kwamba hajui sana kuhusiana na mambo ya utalii sana ila alimwelekeza kwa "boss" wake ili akapate maelezo kuhusiana na utalii eneo hilo.
Asichokuwa akikifahamu Anton Kunzle ni kwamba mrembo aliyekuwa akimuuliza kuhusiana na mambo ya utalii alikuwa ni mke wa kijana mdogo wa Herbert Curkus 😳😳😳.
Kama mtalii , Anton Kunzle alifika kwa jamaa mmoja alieelekezwa kwake ambaye alikuwa ni Rubani na akajitambulisha kama mwekezaji kutoka Austria. Na hapo huyu Anton Kunzle alimuuliza huyu bwana maswali muhimu ya ki professional na aliyajibu pasipo hiyana wala tashwishi. Rubani huyu hakuwa mwingine bali ni Herbert Curkus mwenyewe.
Sasa baada ya kupiga gumzo kiasi , Anton Kunzle alitaka akodi ndege ya huyu Herbert Curkus kwa ajili ya utalii wa hapo mji wa Sau paulo ,yaani kufanya Sight Seeing. Na baada ya dakika kadhaa walikuwa angani wakifurahi na kucheka huku stori zikiwa zimenoga. Kiuhalisia ni kwamba Anton Kunzle alikuwa anajua namna ya kutengeneza marafiki kwa muda mfupi sana ukizingatia na pesa kwake haikuwa tatizo. Na baadaye walirudi na huyu Herbert Curkus alimkaribisha huyu "Mgeni" wake kwenye moja ya boti yake ya kifahari kwa ajili ya kupata kinywaji huku stori zikiwa zimenoga.
Katika harakati zote hizi , Anton Kunzle alikuwa akimfanyia Assessment huyu bwana Herbert kijasusi sana. Na aligundua mara moja tu huyu bwana kwanza anapitia kipindi kigumu cha kiuchumi kutokana na biashara kutokuwa stable. Hivyo Kunzle alianza kutengeneza mazingira ya kumuingiza huyu Curkus kwenye mtego au angle ambayo angeamini msaada wake wa kifedha ungetokana na huyu businessman from Austria ili aweze kuwa stable kiuchumi. Kwa kifupi Curkus alikuwa anasogezewa ndoano taratibu iliaimeze.
Katika harakati za kupiga stori , Kunzle alimweleza huyu Herbert Curkus nia yake ya kuwekeza kwenye biashara ya utalii na pia kuna kampuni ya marafiki zake kutoka ulaya walio na nia ya kuwekeza kwenye biashara hii , hivyo kama na yeye atakuwa tayari ku join hakuna pingamizi kwa kuwa yeye (Curkus) tayari ni mwenyeji na anajua mazingira ya utalii ndani ya Brazil na Latin America kwa ujumla. Hii kama ilimwingia Curkus akilini akaachwa alifikirie , asijue yeye ndio chambo...waliachana siku hii. Hili likapita
Sasa basi, siku hiyo majira ya usiku huyu Anton Kunzle alituma ujumbe wa siri kwa njia ya telegram hadi kwa operational commander bwana Yoske Yariv kumpa briefings kuhusiana na kukutana na "target" yaani Herbert Curkus. Katika ujumbe huo wa siri lilitumiwa jina la "Deceased" yaani mfu kama utambulisho wake Herbert Curkus.
Lakini pia naye huyu Deceased au Herbert Curkus usiku huo na yeye aliweka kwenye dairy yake jina la Anton Kunzle kwenye list ya MAADUI ZAKE. Kwa kifupi machale yalianza kumcheza😳😳😳😳.
Sasa basi wiki moja baadaye , huyu Anton Kunzle alifika kwenye nyumba moja iliyozungushiwa ukuta mkubwa na nyaya za seng'enge zenye short iliyopo kwenye kitingoji cha Riviera ndani ya mji wa Sau paulo. Hapo ndipo makazi ya Herbert Curkus. Kwa kifupi hiyu jamaa alikuwa amejizatiti kiulinzi kutokana na kuishi kimachalemachale. Baada ya kufika Anton Kunzle alijitambulisha kwa mlinzi na kukaribishwa ndani na Herbert Curkus . Baada ya kutambulishwa kwa mke wa Curkus, huyu Curkus pia alimwonyesha Anton Kunzle private armory store. Yaani silaha anazomiliki baada ya kupatiwa kibali na mamlaka ya Brazil. Pia alimwonyesha medali mbalimbali alizopata kipindi akiwa vitani. Kwa kifupi hapa Herbert Curkus alikuwa anatuma ujumbe kwa Anton Kunzle kwamba hata yeye sio "mchache" na anajiweza😁😁🤣. Naye Anton Kunzle alitia hili maanani na awe VIGILANT kutokana na aina ya mtu anayeenda kubdili naye.
Sasa kama marafiki huku stori zikinoga Herbert Curkus alimtaka huyu Anton Kunzle siku akipata muda waende wakatembelee mashamba yake yaliyo nje kidogo ya mji kama sehemu ya matembezi. Kweli jamaa alikubali . Na wakati anarudi hotelini baada ya kuachana na Herbert Curkus aliamua kupitia kwenye duka moja la hardware na kununua kisu kidogo cha kukunja cha mfukoni (switchblade) kama tahadhari just in case siku wakienda huko mashambani kutembea.
Sasa baada ya siku kadhaa jamaa hawa wawili wakaenda matembezi huko mashambani milimani kama sehemu ya kutalii. Ikumbukwe kila mmoja anamlia timing mwenzake hapa. Katika safari hii Anton Kunzle alikuwa amejihami na kisu kidogo cha mfukoni lakini pesa ya kutanua alikuwa nayo kutokana na kuwa ni "mfanyabiashara mkubwa" , lakini huyu rafiki yake Herbert Curkus alikuwa amejihami na bunduki ila financially broke.
Na kweli baada ya mwendo wa safari wa maili kadhaa walifika kwenye uwanda na kusimamisha gari . Akilini mwa Anton Kunzle kukapita mawazo kwamba "usikute huyu Herbert Curkus amenileta huku kuja kuniua na kuficha ushahidi?". Haikuwa hivyo huyu Curkus alitaka kumwonyesha huyu Kunzle jinsi alivyo mtaalamu wa kulenga shabaha. Na kweli Curkus alikuwa yupo bizuri katika kulenga shabaha. Naye pia huyu Anton Kunzle aliambiwa ajaribu. Kwa ustadi alilenga shabaha sehemu moja ya kwenye target 🎯 iliyotengeneza kipenyo cha sentimita tatu kwa risasi kumi peke yake. Huu ulikuwa ni ustadi wa juu sana. Curkus alifurahia kipaji cha huyu best yake. Baada ya hapo waliondoka na kuendelea na safari. Katika harakati hizi zote ilikuwa ni kutengeneza bond kama marafiki lakini mmoja alipaswa afe.
Wiki kadhaa baadaye Kunzle alimtaka huyu Curkus waende matembezi ya mbali hadi Uruguay kwa ndege katika kufanya tathmini ya Maeneo gani ya kuwekeza kwenye biashara ya utalii ikiwemo majengo ya ofisi. Na gharama zote za kusafiri zilikuwa juu yake. Kumbuka huyu Curkus machale yalikuwa yanamcheza sana kumhusu huyu rafiki yake, raia wa Latvia ambaye ni mwekezaji. Hivyo aliamua siku ya kwenda huko aende na camera ndogo ya kupiga picha.
Kunzle alitangulia kwenda Montevideo Uruguay, kisha baada ya siku chache huyu Curkus alimfuata hukohuko. Laiti huyu Curkus angejua anasogezwa kwenye mtego wa kifo asingetamani kusafiri. Sema tu chambo ya pesa ilikuwa imeshamnasa.
Siku ya kufika airport, bwana Curkus alipokelewa na Anton Kunzle,lakini kama surprise Curkus alitoa camera yake na kumpiga picha Kunzle kama surprise.. haikuwa big deal sana kwa Kunzle, ila kwa upande wa Curkus alichokifanya ni KUMPIGA PICHA MUUAJI WAKE,KAMA KUMBUKUMBU 😳😳😳😳.