SEHEMU YA PILI
Marafiki hawa baada ya kukutana ndani ya mji wa Montevideo tena waliendelea kufurahia maisha ya utalii huku wakifanya tathmini ya Maeneo muhimu ambayo wangeweza kuweka kambi au ofisi ya kampuni ya utalii ambayo Kunzle alikusudia kufungua. Harakati zote hizi gharama zilikuwa juu ya Kunzle ikiwemo kula kwenye restaurant na gharama zote za hoteli kwa siku kadhaa walizokuwa ndani ya mji huo.
Badada ya muda waliamua kuagana na kuahidi kukutana tena siku chache zijazo kuendelea na PROJECT hii hivyo Curkus akarudi zake sau paulo na Kunzle akaruka hadi Ulaya.
Sasa basi.
Anton Kunzle alipofika Paris na kutoa tathmini na mchanganuo mzima mbele ya kikosi kazi cha mbele ya Maafisa wa mossad kuhusiana ja Curkus, lilipitishwa Azimio kwamba huyu Curkus alipaswa kuuliwa Uruguay na sio ndani ya ardhi ya Brazil. Kwanini sio Brazil?
Kwanza tathmini iliyofanyika ilionekana kwamba Curkus ana connection na vyombo vya usalama vya Brazil kama polisi hivyo zoezi lingekuwa gumu kidogo kummaliza. Pili ilionekana kwamba ndani ya Brazil kuna jamii kubwa ya Wayahudi ,hivyo kumuua Curkus kungesababisha jamii hizi za Wayahudi kushambuliwa na wale Pro-Nazis wa kijerumani ambao nao wanaishi humohumo kama njia ya kulipiza kisasi. Na pia brazil bado ilikuwa na sheria ya adhabu ya kifo, hivyo ikatokea mpango mzima umeenda ndivyo sivyo na kukamatwa, wangepotea moja kwa moja.
Ikaamuliwa kwamba kummaliza Curkus kwenye nchi ya Uruguay ingekuwa na unafuu kiasi.
Baada ya tathmini kukamilika , mchakato ulianzishwa mara moja . Kikosi cha wauaji kikiongozwa na Yoske Yariv ambaye ni operational commander wa CAESAREA TEAM. ukiachana Yoske pia timu hii ya wauaji ilikuwa na Ze'ev Amit(Slutzky) ambaye alikuwa ni mpwa wa mkurugenzi wa Mossad wa wakati huo bwana Meir Amit. Wengine walikuwa Anton Kunzle, Eliezer Sudit pamoja na Arye Cohen. Timu hii ikawa imekamilika.
Timu hii ya wauaji wa mossad waliwasili Montevideo Uruguay mwezi February mwaka 1965. Na rasmi kila mmoja akaanza kuingia kwenye majukumu yake aliyopangiwa. Huyu Eliezer Sudit ambaye alitambulika kama Oswald tausig alipofika tu alikodisha gari aina ya Volkswagen pamoja na nyumba ndogo kwenye mtaa wa Cartagena , kitongoji cha Carrasco kwenye mji wa Montevideo. Kisha alipewa kazi ya kununua sanduku kubwa kiasi aina ya trunk kwa ajili ya kutumiwa kuweka mwili wa Herbert Curkus. Hili likawa limekamilika. Na mitego ikawa imesetiwa ipasavyo.
Sasa ilipofika tarehe 23 February 1965, Anton Kunzle alimualika tena Herbert Curkus wakutane tena ndani ya Montevideo Uruguay lengo likiwa kuendeleza project yao.
Baada ya mapokezi uwanja wa ndege, Anton Kunzle alimchukua Herbert Curkus kwenye gari ndogo aina ya Volkswagen na kumpeleka hadi kwenye mji mdogo wa Casa cubertini kwenye mtaa wa Cartagena ambapo timu ya wauaji ilikuwepo ikimsubiri "Deceased" Herbert Curkus awasili.😋😋😋
Herbert Curkus aliamini kwamba wanaenda kuangalia baadhi ya nyumba zitakazofaa kwa minajili ya kuweka ofisi za utalii kama alivyoambiwa na Kunzle. Na kweli walifika kwenye nyumba moja iliyokuwa ikiendelea kufanyiwa ukarabati na "mafundi" wakiwa bize kufanya kazi hapa na pale.
Kunzle alishuka kwenye gari na kutembea kuelekea mlango mkuu wa nyumba hiyo iliyokuwa ikikarabatiwa. Herbert Curkus naye akashuka akimfuata jamaa kwa ajili ya kuangalia site nini kilikuwa kikiendelea asijue kwamba anakaribia kuiendea Mauti yake🥺🥺.
Baada ya kufungua mlango huo Anton Kunzle na Herbert Curkus kuingia ndani ya jengo hilo,Ghafla hali aliyokutana nayo Herbert Curkus hangeweza kuamini kama angefanikiwa kutoka hai. Alipoingia ndani tu hivi timu hii ya Wauaji wa Mossad walikuwa wamesimama kwenye ukuta wakimsubiri Herbert Curkus,the butcher of Riga kwa usongo mwingine ambao hauelezeki. Anton Kunzle aliurudishia mlango kwa kuubamiza kwa nguvu. Sasa hapo ikawa kwamba Herbert Curkus hana la kufanya zaidi ya kuipigania roho yake.
Mkono ulipigwa haswa na kutokana nguvu alizokuwa nazo huyu Curkus,alifanikiwa kuwamudu hawa Mossad kwa kiasi. alipotaka kutoroka kwa kuuwahi mlango ili atoke nje lakini walifanikiwa kumdhibiti na kumuangusha chini. Hivyo Amit alichukua nyundo na kumshushia Curkus pigo moja tu la kichwa.
Nyumba nzima ilitapakaa damu haswa . Curkus alipotaka kumchomoa bunduki yake aliwahiwa na Arye Cohen na kupigwa risasi mbili za kichwa kwa kutumia bastola yenye kiwambo cha sauti (silencer) ili isizushe tafrani kwa wapita njia walioko nje.
Kutokana na damu kutapakaa kila mahali kwenye sakafu na ukutani , Afisa mmoja haraka alitoka nje na kuleta hosepipe ya maji kwa ajili ya kusafisha nyumba hiyo. Ikumbukwe kwamba huyu Herbert Curkus alipswa kukamatwa akiwa mzima na kufikishwa kwenye mkono wa sheria lakini kutokana na kumchukulia poa ikapelekea wamalizane nae.
Hivyo haraka ikaletwa sanduku kubwa au trunker lililokuwa tayari limenunuliwa kwa ajili ya kuuweka mwili wa Herbert Curkus humo. Lengo ni kwa ajili ya kuwaaminisha police wa Uruguay watakapofanya uchunguzi wao waamini pengine huyu Curkus alitakiwa atoroshwe akiwa hai kwa kutumia sanduku hilo. Baada ya kukamilisha hili zoezi juu ya sanduku hilo waliacha ujumbe wa maandishi uliosomeka hivi ;
"Considering the gravity of the crimes of which Herberts Cukurs
was accused, notably his personal responsibility in the murder of thirty thousand men, women, and children, and considering the terrible cruelty
shown by Herberts Cukurs In carrying out his crimes. we condemned the said Cukurs to death. The accused was executed on February 23, 1965, by 'those
who will never forget.' "
Timu hii ya mossad baada ya kukamilisha hii operation waliondoka. Watu waliokuwa nje ya jengo hili hawakujua ni nini kilikuwa kikiendelea. It was too late.
Timu hii ya majasusi walijigawa na kila mmoja aliondoka kivyake ili kufuta traceability na kufuatiliwa na mda mchache kila mmoja alikuwa ameshika njia yake kurudi Ulaya na wengine Israel.
Huku nyuma Uruguay baada ya siku nane polisi ndio walifika eneo la tukio hapo Cartagena street ulipotokea mkasa, tena ni baada ya gazeti moja la nchi hiyo kupewa fununu na mmoja wa hii timu ya Mossad kuhusiana na mauaji hayo.
Kesho yake , magazeti yaliripoti tukio hili baada ya mwili wa mfanyabiashara Herbert Curkus kugunduliwa kwenye nyumba iliyokuwa ikikarabatiwa . Magazeti yalijaribu ku suspect majina mawili kama ya wahusika wa huu mkasa na jina lake Anton Kunzle lilichomoza kwenye kurasa za mbele kama main suspect. Na pia picha yake iliwekwa kwenye kurasa za mbele zikiambatanishwa na jina lake. Haikusaidia sana Herbert Curkus the butcher of Riga was NO MORE.
Siku chache baadaye mke wa Curkus alipata barua kutoka kwa rafiki wa mumewe yaani kutoka kwa Anton Kunzle iliyosomeka hivi.
My dear Herberts,
With God's help and that of some of our compatriots. I have safely
reached Chile.
I am now resting after a liringjourney. and I am sure lhat you, too, will very soon be back home, Meanwhile, I've discovered that
we were followed by two people, a man and a woman We must be very careful and take every precaution As I've always said, you are running
a great risk in working and traveling under your own name, It could be
disastrous for us, and also lead to my real identity being discovered. I hope that the complications in Uruguay have taught you a lesson
for the future, and that You'll be more prudent now, If you notice
anything suspicious in or around your house, remember the advice I
gave you: go and hide among Von Leeds's men until
the question of all amnesty is settled.
When you get this letter, reply to the address you know of.
in Santiago Chile,
Yours, Anton k.
Kwa kifupi barua hii ilitaka kumjulisha tu huyu mke wa Curkus kwamba "MIMI ANTON KUNZLE NDIO NIMEMUUA MUME WAKO".
Kwa mara nyingine mossad walifanikiwa kulipa kisasi .
End .