Rais Putin wa Urusi
Umetoa elimu kubwa na nzuri
MALCOM LUMUMBA na hakika yapo mengi ya kujifunza kwenye uchambuzi wako huu.
Hivyo vitabu kwenye biblia mie nimeshawahi kuvisoma lakini huwa napata shida kuelewa maana halisi katika baadhi ya mistari yani natafakari na kutafakari bila kufika mwisho.
Kwangu mimi naona kuna ujumbe mzito sana humo lakini umeandikwa kwa mafumbo magumu kuyatatua na shida ndiyo inaanzia hapo.
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa
Majasusi wengi wana nafasi kubwa ya kuwa viongozi wazuri kwenye nchi endapo tu akiwa na kipawa na vinasaba vya Uongozi thabiti.
Sababu kubwa ni uongozi mzuri unatokana na mtu kuwa na kipawa/kipaji cha kuongoza pamoja na akili, hekima na busara.
Sasa huyo mwenye kipaji cha uongozi thabiti akipitia kwenye fani ya ujasusi basi hapa ule uwezo wake wa kuongoza na akili yake naona itakuwa maradufu, anakuwa ni kiongozi thabiti na aliye smart sana na wengi wao huwa ni wazalendo japo wapo wachache uzalendo wa kweli unakosekana na wanakuwa viongozi wabaya sana.
Pia Urusi ilikuwa na mifumo imara iliyojengwa na watawala waliotangulia kabla ya rais Putin na mingi ya mifumo hii imara ilijengwa kipindi kile cha USSR kubwa na yenye nguvu(The mighty USSR) alichofanya Putin ni kuiendeleza tu hiyo mifumo aliyoikuta.
Lakini changamoto kubwa sana Putin aliyoikuta ni Urusi dhaifu yenye majeraha mabichi ya kusambaratika kwa USSR mnamo miaka ya 1990 na yeye alipokea madaraka kutoka kwa rais mlevi Boris Nikolayevich Yeltsin ambaye aliacha Urusi ikiwa na changamoto lukuki.
Ufanisi wake katika kukabiliana na hiyo changamoto ndiyo kunafanya aonekane rais na kiongozi mzuri sababu kunairejesha tena Urusi ile imara yenye nguvu.
Putin alivyoingia tu madarakani kama acting president mnamo mwaka 1999 yeye aliapa yafuatayo:
Extracts from Putin speech, August 1999
- We need to put an end to revolutions. These are staged so that nobody can be rich. But at the moment the country needs reforms so that nobody can be poor. Although this task, unfortunately, is becoming harder by the day. There is no such thing as a thriving state with an impoverished population.
- A most important instrument and a most important priority for the government is a secure food supply. We will provide serious assistance to the agrarian sector and in the final analysis to millions of peasants who have just one concern - to feed the country with quality Russian produce.
- Russia's territorial integrity is not subject to negotiation. Or, especially, to horse trading or blackmail. We will take tough action against anyone who infringes upon our territorial integrity, using all the legal means available to us.
- Russia has been a great power for centuries, and remains so. It has always had and still has legitimate zones of interest abroad in both the former Soviet lands and elsewhere. We should not drop our guard in this respect, neither should we allow our opinion to be ignore
Hivyo ni vipaumbele vyake na kama alivyoapa anaishi katika kiapo chake hicho. Kwenye black lines hiyo misimamo yeye harudi nyuma na hakuna mjadala kwenye hilo na wote tumeona Crimea na Syria vile ni anatekeleza tu sasa.
Hii ni hatua kubwa kwake yeye akiwa kama kiongozi wa Urusi kwa sasa na ni mafanikio pia.
Wamagharibi kilichofanya wajisahau ni kule kusambaratika kwa USSR sababu walifikiri mchezo umeakwisha tayari waliamini hivyo.
Uchina na Urusi wanamkataba maalumu unaozitaka pande hizi mbili kusaidiana wakati wa dhiki na misukosuko mikubwa hiki nacho ni kama kiapo, na ndiyo maana millitrary tech kubwa China anategemea Urusi na Urusi aliwahi kusema China angekuwa katika hali ngumu sana kiulinzi na kiusalama bila Warusi kumpa high tech.
Hivyo kama Trump anataka kuwa na ushirika mzuri na Urusi na hapohapo mapambano dhidi ya China hilo sijui litawezekana vipi, wewe ni rafiki yangu mkubwa sana sasa adui yangu mimi anaeza kuwa rafiki yako?
Tuzidi kuangalia sera mpya za Trump zitaleta impact ipi kwenye hizi geopolitics duniani maana mie huwa namuona Trump kama mtu asiyekuwa na misimamo vile yani anabadilika badilika sana.
Nitazidi kuvisoma hivyo vitabu vya biblia nitafakari zaidi mkuu.