Tungepata raisi kama huyo ,tungeendela inashangaza urusi ndio wenye technolojia nzuri ya umeme wa nuclear na kuchimba gesi lakini tunawakodolea macho tu hatuchangamki tunawaogapa USA. 😱😱😱😱😱
Raisi Jakaya Kikwete alikuwa na mpango wa haya mambo ya nishati ya nyuklia.
Lakini Maveteran wengi wa Usalama walishauri kwamba itakuwa ni hatari kwa taifa kwasababu Tanzania kuna rushwa sana hivyo hiyo teknolojia ya Nyuklia au madini ya Uranium yanaweza yakaanguka kwenye mikono ya makundi hatari ya kigaidi.
Hata wataalamu (Scientists) wanaosomea haya mambo ya nyuklia duniani kote huwa wanaangaliwa sana kwa jicho la tatu,
sasa kwa jinsi mifumo ya nchi yetu inavyolega na watu wanauzana kwasababu za Kisiasa na kimaslahi kama ambavyo tumeshuhudia tokea awamu ya pili unategemea hawa wanasayansi hawatakuwa sumaku ya utekaji kweli ???
Ushauri mwingine walisema inawagharimu sana mataifa makubwa kwenye kutunza vile vinu,
Pamoja na utupaji taka za Nyuklia ambao inasemekana ni gharama mno kwa nchi kama yetu.
Isitoshe ukisoma hata mtaji unaohitajika kurutubisha ile Yellow Cake ni pesa kubwa sana sanaa.
Tupilia mbali bado hujapeleka mamia ya wanasayansi nchi za nje kusoma.
Wanasema Tanzania bado hatujajiandaa.
NB: Lakini kubwa zaidi wazungu wanasema sisi tunaweza kuuza madini kwa nchi korofi kama Korea Kaskazini na Iran,
Kwasababu Tanzania tumeshawahi kupata kashfa miaka mingi nyuma kwamba tunaongoza kwa kuficha magaidi hatari hapa nchini kwetu. Pia miaka ya karibuni tumeshutumiwa kuwasaidia Iran na Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa. Hivyo kuwa na hii teknolojia kunaweza kuleta Unnecessary Attention ya mataifa makubwa nchini mwetu ambapo mambo yetu mengi ya kiulinzi na kiusalama yatakuwa hatarini. Inamaanisha Majasusi ya CIA, MI6, BND, MOSSAD na mengine yanaweza kupanua wigo wa kazi zao hapa nchini hadi wakapenya kila sekta kuhakikisha kweli tunakuwa na matumizi salama ya nyuklia (Watawala wetu hawatapendwa sana kumulikwa na hawa wazungu)
Japo, binafsi nasema kama nchi inabidi tubadilishe Mtazamo wa kifikra.
Hizi fikra za wale wazee wa miaka ya 60's, 70's na 80's inabidi zifanyiwe tathmini kwa upya ili nchi iendelee.
Dunia kila baada ya masaa 24 inapiga hatua kubwa sana ambazo hazimsubiri mtu, na taifa imara ambalo halitataka kuendana na kasi ya dunia basi ni lazima litakuwa katika huruma ya mataifa yenye nguvu. Kama tunahitaji viwanda basi ni lazima tujipange kuzalisha nishati ya kutosha kwa matumizi ya wananchi, wawekezaji na nyingine tuuze hata nje ya nchi.
Nawapenda sana wakina Dr. Kitine, Mzee Warioba, Mzee Mahiga na wengine wote ambao ni First Generation,
Lakini ili hili taifa liende mbele kuna mpaka ni lazima hawa wazee wawekewe, kwasababu naona wengi wao wana Nostalgia ya kutaka Tanzania ya mwaka 2018 ya karne ya 21 iwe kama ile ya miaka ya 1970's ya karne ya 20 ambayo wao waliishi na kuona ni Golden Age. Hatutawatenga kabisa lakini tunahitaji kutengeneza Mzani wa Chuma ambao utahakikisha mawazo ya wazee yanakuwa Realistic kuweza kulinganana hali ya sasa na pia mawazo ya kizazi cha vijana hayatishia misingi ya taifa. Hawa wazee wetu wameshachoka sana na ifike mahali hata kama tunawahitaji ni lazima wakae katika nafasi ya kushauri tu na siyo kimaamuzi. Japo Tanzania tuna changamoto kubwa sana ya kukosa Skilled Manpower hasa kwa vijana, japo naamini tukiweza kufanya Professional Synchronization tutaikabili hii changamoto.
ENOUGH WITH POLITICS OF FEAR......
THIS COUNTRY HAS TO MOVE FORWARD AT A GOD SPEED.
WE ARE 100 YEARS BEHIND THE WEST AND 60 BEHIND THE EAST,..WE NEED TO CATCH UP.
OR WE ARE GOING TO BE THE VICTIMS OF EASTERN ECONOMIC DEVELOPMENT JUST AS WE WERE TO THE WESTERN.