Urusi na Uchina wamerudi kwenye mahusiano yao ya kabla ya mwaka 1969 (Sino-Soviet Split).Utofauti ni kwamba kipind hiki ni:
Mosi, Uchina ndiyo kiongozi wa genge la Mashariki siyo Urusi.
Pili, huu ni muungano wao ni wa kimaslahi (An Alliance of Convenience).
Tatu, huu muungano unashikilia asilimia zaidi ya 31% ya Uchumi wa dunia.
Miaka nane iliyopita, January 7, 2017 mnamo saa tano asubuhi niliandika kwenye uzi namba #40 kwamba, hakuna jambo ambalo litampa Marekani changamoto kubwa kiusalama endapo Uchina na Urusi wataungana na kuanza kufanya kazi pamoja. Niliyaandika haya kwa kuweka kabisa rejea hasa kwenye aya ya tano, ambapo nilizungumzia msiamo wa Dr Henry Kissinger katika kutekeleza mkakati wake wa Divide Et Empera kuhakikisha kwamba Urusi na Uchina hawafanyi kazi pamoja.
Mwaka 2022 wakati vita vya Ukraine vimeanza, Dr Henry Kissinger aliyarudia haya maneno kwenye mkutano wa Davos, World Economic Forum ambapo alisema kwamba haitakiwi nchi za Magharibi ziitenge sana Urusi kiasi cha kuifanya iingie kwenye mikono ya Uchina. Maneno haya siyo ya Dr Kissinger peke yake, bali hata msomi mwingine ambaye alikuwa mwana mkakati mashughuli wa Marekani, Zbigniew Brzezinski aliyasema kwenye moja ya maandiko yake mwaka 1997, The Grand Chessboard: American Primacy and Its Geostrategic Imperatives.
Tatizo ni kwamba, wakati USSR inapambana vita baridi na Marekani, mbali na kuwa na jeshi bora kabisa lenye teknolojia kubwa kabisa, GDP yake ilikuwa ni asilimia 30% ya uchumi wa Marekani, huku ikiwa imetengwa kabisa na soko la dunia. Utofauti wa leo ni kwamba, Uchina inapambana na Marekani ikiwa siyo taifa lenye nguvu kubwa kijeshi, bali taifa lenye uchumi mkubwa (World's Economic Power House).
Uchina peke yake ana mambo muhimu yafuatayo tofauti na USSR:
1. Anashikilia asilimia 18% nzima ya Uchimi wa dunia.
2. Yeye ndiyo taifa la pili kwa uchumi mkubwa duniani (Katika GDP Metric)
3. Yeye ndiyo taifa la kwanza kwa uchumi duniani (Katika PPP Metric)
4. Yeye ndiyo taifa la kwanza kwa uzalishaji wa kiviwanda.
5. Yeye ndiyo taifa la kwanza kwenye biashara ya kimataifa.
6. Yeye ndiyo taifa la pili kuwa na idadi kubwa ya watu wengi.
7. Yeye ndiyo mshirika mkubwa wa kibiashara wa Marekani.
Ukizingatia haya mambo tu utafahamu kwamba Marekani ana changamoto kubwa mno kuliko kipindi chochote kile cha uhai wake kama taifa. Maadui wengi wa Marekani ndani ya miaka 200 iliyopita kama The British Empire, The Spanish Empire, Imperial Germany, Imperial Japan na Nazi Germany hawakuwa na nguvu kubwa kama ambayo Uchina anayo leo hii kwenye nyanja nyingi za kiushawishi.
Mbali na hapo, ni kwamba kwa mara ya kwanza Marekani inapambana moja kwa moja na taifa ambalo halitokei barani Ulaya, siyo taifa la kizungu (Latin/Saxon) na siyo taifa la kikristo kiasilia. Hivyo endapo hili taifa litamshinda, siyo tu itakuwa tatizo kwa Marekani, bali kwa mataifa yote ya Magharibi ambayo kiasilia ni Democratic-Ango-Saxon-Latinized-Judeo-Christian Nation States.
Uchina ni taifa la lenye watu ambao ni Communist-Mongoloid-Manchus-Hakkas-Buddhist-Confucianized Society, hivyo taifa hili likishinda dunia itaona mabadiliko makubwa mno ambayo haijaweza kuyaona ndani ya miaka 500 iliyopita tokea kuzaliwa kwa taifa la Ottoman.
Urusi akijifungamanisha na Uchina basi, Uchina itapa an Easy FootHold Over Europe, through the Eastern Gates. Ndiyo maana kina Kissinger na Nixon walilifahamu hili mapema na kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kambi ya Urusi na Uchina inavurugika.
====================================================
Mpaka sasa, Uchina hana haja ya kuingia vitani kupambana kijeshi na Urusi. Anachokifanya ni kuitumia Urusi, Iran na Korea-Kaskazini kuhakikisha Marekani anatingwa na majukumu yake kule Ulaya na Mashariki ya Kati kiasi cha kwamba hawezi kufanya The Pivot To Asia kirahisi ambapo anatamsumbua China na Taiwan.
Miaka ya Raisi Obama, Kurt Campbell waliyemuita the Asian Tsar, alikuja na mkakati wa The Pivot To Asia, kwamba baada ya kumaliza Global War On Terror na kuyashughulikia mataifa ya kiislamu ipasavyo, sasa ilitakiwa wahamishie nguvu zao Asia kupambana na taifa la Uchina ambalo ndiyo linaonekana kama Peer Competitor.
Aliyevuruga huu mpango ni Bwana Vladmir Putin, ambapo mwaka 2008 alipovamia Georgia alionekana anatania tu, kwasababu kwanza Urusi ilikuwa haina jeshi imara na la kisasa, lakini pia nchi ilikuwa na uchumi mbaya huku Vladmir Putin akitegemewa kutorudi madarakani tena mwaka 2012. Bahati mbaya akarudi mwaka 2012 na akafanya jambo la ajabu mwaka 2014 akafanya jambo la ajabu ambalo wengi wetu tulilishangaa la kuvamia jirani yake kimabavu.
Hakuishia hapa, akaingilia vita vya Syria mwaka 2015 akishirikiana na Iran na kundi la Hezbollah kuhakikisha serikali ya dikteta Bashar Al Assad inabaki madarakani kwa gharama yoyote ile. Uwepo wa Bashar Al Assad madarakani mpaka leo hii 2024, umechangia kwa sehemu kubwa kile kinachoendelea kule GAZA kwasababu nchi ya Syria imegeuka kuwa Launch-Pad ya Iran and Hezbollah dhidi ya Israel.
Wakati Marekani inajifikiria na jinsi ya kupambana na Vladmir Putin, ghafla mwaka 2016 Donald Trump akawa Raisi wa Marekani na kuanza kuvuruga ajenda nyingi zilizokuwa zimepangwa na watangulizi wake. Hasahasa kuhusu NATO na Ukraine. Sasa haya mambo yote yanayoendelea yanaigharimu Marekani, muda na rasilimali.
Kule Ukraine tu, mpaka sasa mataifa ya Magharibi yametumia zaidi ya dola za Kimarekani Bilioni 400 ambazo ni zaidi ya Trilioni 1000 za kitanzania. Huku mataifa ya Magharibi yakipeleka silaha zao na ujuzi wao uwanja wa vita, wakiua zinazosababisha vifo vya maelfu wa warusi na waukraine.
Mwisho wa siku, ukiangalia kwa makini Uchina ndiyo mshindi, maana itafika mahali the war of attrition between the West and Russia will wear off both parties, leaving China unscathed. Muda siyo mrefu itatokea vita kubwa Ulaya, endapo itaonekana Ukraine anashindwa, na mataifa ya NATO yataingia moja kwa moja na kusababisha matatizo makubwa mno.
====================================================
ENIWEI dunia ndivyo ilivyo, nadhani MUDA NI MWALIMU MZURI.