Ujasusi / Upelelezi / Udukuzi: Maana yake halisi na uhatari wake

Kwa ujumla, mbabe ndiyo anayetawala na kula matunda ya mnyonge, japo mnyonge huyo haachi kujitutumua. Ni kawaida pia baadhi ya wajanja kutumia mianya iliyopo katikati ya wanyonge na watawala kujineemesha. Mitindo yote ya kupata neema na faida haitengenezwi kwa asilimia kubwa na njia halali.
 
Kinachoitwa haramu kwa upande mwingine ni halali na sifa kubwa katika upande pinzani. Majasusi, wadukuzi, wazandiki na magaidi hufurahia sana kila mipango yao inapofanikiwa. Kwa maana hiyo serikali na majeshi yao huendesha na kufundisha kwa kina watu wao haya madudu yanayoonekana haramu kwa wapinzani wao.
 
Wakati kuna mfumo dhabiti au legelege wa sheria, idara za serikali zinazohusika na usalama mara zote hutenda vitendo vya sheria nje ya ganda ambako umma umeaminishwa kuona, lakini nyuma ya pazia kuna vitendo vingi vya kihuni na dhambi za hali ya juu vinavyoidhinishwa na kakundi kadogo sana ka watu waliopewa mamlaka na sheria hizo hizo zinazopinga dhambi.
 
Rushwa, tamaa ya mali, undugu, madhambi ya mauaji na kuwafunga watu kwa kuwaonea kwa tamaa ya madaraka, n.k. husababisha mifumo halisi ya Ujasusi na mingine inayoshabihiana nayo kuhama katika utaratibu halisi wa kisheria unaoongoza taasisi hizo katika nchi na kumilikiwa na watawala wang'anizi wa madaraka, wanaokumbuka waliyoyatenda katika vipindi vyao halali, hivyo kudhani kuwa wakiwaachia wengine nafasi zao za maamuzi watawalipizia visasi.
 
Matokeo yake ni kujenga mifumo hiyo kwa mitizamo ya kikabila, kindugu na kirafiki ili kuendeleza utawala wao wa mabavu.
 
Ujasusi na upelelezi kwanza hujengwa na tamaa binafs ya jasus au mdukuz na mpelelez ya kutafuta habar na pia hufurahia kufanya hivyo
Vitendo hiv hata vipingwe na serikal au sheria watendaj bado hujiona wenye haki
 
Ujasusi na upelelezi kwanza hujengwa na tamaa binafs ya jasus au mdukuz na mpelelez ya kutafuta habar na pia hufurahia kufanya hivyo
Vitendo hiv hata vipingwe na serikal au sheria watendaj bado hujiona wenye haki

Tamaa binafsi ya Jasusi, Mpelelezi au mtu yeyote anayefanya kazi zinazoshabihiana huwa za aina tatu hasa kwa mtu aliyefundishwa na kuiva. Kwa kuwa umewahi kuliko mimi basi ngoja nikujulishe tu aina hizo za tamaa.
 
Bila shaka kiongozi spade 4spade cos sina uelewa wa taaluma hii bali natumia akili ya kuzaliwa na uzoefu binafs
Karibu tusemezane
 
Tamaa ya kwanza ni uzalendo halisi wa nchi au kikundi anachokitumikia. Kwa mafunzo yake na ujuzi wa mambo na uzalendo wake wa kutenda kazi na kuzalisha faida ya kazi yake katika nchi au kundi analofanyia kazi, mtu hujaa ujasiri na ushupavu wa kutenda zaidi ya uwezo wake hata kama anahatalisha maisha.
 
Tamaa ya pili ni ile inayochochewa na takrima ya fedha, madaraka, sifa, urithi au matukio fulani ya nyuma yanayomgusa mhusika moja kwa moja.
 
Tamaa ya kijinga na kiherehere tu kisicho na maana cha kujitangaza katika jamii na kujionyesha kuwa na wewe wamo hata kama huna uwezo huo.
 
YA mwisho imegawanyika Kwa makundi mawili ya ujasusi, upelelezi na udukuzi
Kwanza n kujionyesha kuwa na uwezo, na kutenda mambo expedition ambayo hupenda kuonekana Kwa wenzao na si jamii na kund la pili ndio wanaoishi Kwa kiherere na kujionyesha Kwa watu



Kundi la kwanza n born as spy and pili n made to be spy
 

Yap, nilisahau kuandika ya tatu lakini nilimaanisha hiyo ya mwisho niliyoandika. Nilikuwa nachambua kuhusu serikali kuwa na idara za ujasusi, udukuzi na zingine zinazoshabihiana.
 
amazing sana
 
mkuu Yericko Nyerere kwenye hayo maandishi niliyokoleza, hauoni kama ni vema kwa jasusi kulinda cover yake kwa kutochukua hatua yoyote ya moja kwa moja zaidi ya kufahamisha mamlaka husika za kisheria (law enforcement agencies) kama police and the like? au huo nao ni uozo wa sheria ya T.I.S.S ya mwaka 1996???!!!!!!!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…