Mtu kama yule alietengeneza helikopta ndiyo wanastahili kulindwa kwa ubunifu wao. Ni sawa na ukiangalia baiskeli ambazo zinatumiwa na baadhi ya nchi kwenye michezo ya Olimpiki ni kwamba hutakuja kuona au kufahamu formula na michoro iliyotumiwa kuunda baiskeli hizo.
Hiyo ndio inaitwa "intellectual property", na si tu hio kazi kama za usanii wa kuimba au kuchonga vinyago.
Ukibuni kinyago inatakiwa ulinde kipaji chako ulichotumia kubuni na kutengeneza kinyago hicho, na hata mtu akitaka kuiga anashindwa kama una protection ya kazi yako.