Uje na vifaa vya kujifungulia.,Jee hii ni sawa?

Uje na vifaa vya kujifungulia.,Jee hii ni sawa?

Tar 30/01/2018, nilienda na mama kijacho wangu ktk zahanati moja ya Serikali kwa lengo la kuanza Kriniki kama nimepatia, na tulienda wote hiyo siku ya kwanza kwakuwa kanuni na taratibu zinataka hivyo.

Ktk mambo tuliyofanyiwa na kushauriwa kwa maendeleo ya kijacho kuna baadhi yalituacha mdomo wazi kidoga, sasa sijui ni kwa7bu ya ugeni wetu ktk jambo hili au laa, lkn pamoja na ugeni, mboni mimi sioni uhalali wake?!!.

Bila kupoteza muda, jambo lenyewe lililotuacha mdomo nje ni hili hapa: tuliambiwa siku ya kujifungua ikifika ya mpendwa wangu anatakiwa aende na:-
1.Mpira wa kujifungulia.
2.Grops
3.Nyembe
4.Khanga doti 5
5.Beseni
6.Ndoo
7.Bandage na mkasi.

Jee, nikweli tunatakiwa tupeleke vitu vyote hivi hospital jamani?!!.
Acha utoto kijana....mimba uweke bure....huduma ya kujifungua unataka bure tena!mbona kwenye kuiweka hiyo mimba hukuomba ushauri/msaada?
 
Back
Top Bottom