Ujenzi Bandari ya Bagamoyo: Aliyemshauri vibaya Rais Magufuli ni nani?

Kwanini unasema alikiwa right...tufungulie na sisi kile tusichokiona


Magufuli hakupinga Bandari ya Bagamoyo
Alikataa mkataba walioleta wachina

Mkataba wa wachina wanataja hela nyingi kuliko uhalisia wanaweka deni la mile
Wachina wanasema Bandari watajenga Kwa dollars bilion 20..

Sisi makusanyo yetu yote ya Kodi ni hayafiki hata dollars bilion 12 Kwa mwaka..

Halafu sehemu ya masharti ni kuwa wataimiliki bandari tukishindwa kulipa deni
Kitu ambacho ni so obvious..

Kingine bandari itakuwa kubwa mara 20 ya Bandari ya Dar but uwezekano wa mahitaji kuongezeka mara 20 ndani ya miaka hata 10 hakuna...

Magufuli baada ya kuona mkataba mbovu
Alianza tafuta wawekezaji wengine
Alishaongea hadi na waturuki..
Kumbuka hata ujenzi WA sgr wachina walitaka kutupiga ndo akawatafuta waturuki..

Mkataba alio saini Kikwete ni mbvu na haufai

Magufuli alikuwa right
 
Kwenye kumuamini mwendazake Mimi ndio ninapopata shida, Kama kitu hataki yeye ni lazima akinajisi kwa nguvu kubwa...
 
We ni mnafiki.
 


Mimi nakukumbuka Sana ulituambia atakuja Rais mlokole ..way back..
Attachment uliyonayo kwake naiheshimu Sana..
Nakumbuka those days Magufuli alikuwa waziri but ana attend makanisa ya kilokole kama Kwa Ferdinand openly..
So aliposhika nchi nilikumbuka maoni yako
Nikajua utakuwa umeguswa deep na Magufuli..

All in all ana mazuri yake na Mabaya yake..
But angalau hakuwa mwoga kuonesha msimamo wake waziwazi kwenye mambo kadhaa..likiwemo hili la mkataba mbovu wa Bandari ya Bagamoyo..

Kuna watu wanataka kumpa Presha Mama aanze kuruhusu kila kitu..
Nahofia inflation kubwa inakuja
 
Magufuli alitudanganya kuwa ATCL inapata faida, Si ajabu alitudanganya pia kuhusu masharti ya bandari ya bagamoyo.

Magufuli alikuwa akitaka jambo lake au kama alikuwa hataki jambo hakuona haya kudanganya.

Siwezi kuamini kauli ya Magufuli katika hili mpaka huo mkataba uwekwe wazi
 
Magufuli alikuwa right..
Sikumkubali Magufuli but Kwa Bandari ya Bagamoyo alikuwa 100 percent right

Wachina walimkatia yule mgogo kitu kidogo na ndio maana anataka kutuambia alishauriwa vibaya!! Je kuhamia Dodoma hakushauriwa vibaya we mgogo? Ndugai sio wa kumuamini he has no integrity; mnakumbuka Ufisadi wa mabiilioni ya shilingi alioufanya alipokwenda India? Huo ni ushahidi tosha kuwa haaminiki.
 
shida sio mkataba hapa ishu KATIBA mpya...mengine yasitusahaulishe jambojema kama hilo
 
"Wakipata hasara serikali iwalipe fidia lakini wakipata faida ni yao kwa muda wa miaka 40 " hiyo point tu imenifanya nione mradi ulivyo wa hasara kwa Tanzania na wa hovyo kabisa
 
Bunge si ndiyo mshauri wa serikali! Mlishauri vibaya?Vipi tena Ndugai
 
Kuambiwa pekee tunaweza kudanganywa..., Mkataba uwekwe wazi ili tujionee wenyewe kama tunapigwa au tunapiga...

Mbona wakati wa Kikwete Zitto hukuomba kuona mikataba ya Gesi inawekwa public? Na mikataba yenyewe ilipitishwa under certificate of urgency na wewe ukiwa bungeni?
 
"Wakipata hasara serikali iwalipe fidia lakini wakipata faida ni yao kwa muda wa miaka 40 " hiyo point tu imenifanya nione mradi ulivyo wa hasara kwa Tanzania na wa hovyo kabisa

99 YEARS!!! NO DEVELOPMENT OF OTHER PORTS!!
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ dunia inachekesha watu wa JF wanasema mkataba ulikuwa mbovu na ilihali hamjawahi kuuona huo mkataba bali mlisikia mkiambiwa sasa Ndugai yeye tangu 2018 mpaka leo kabaki na msimamo wake ule ule nahisi yeye alisha uona huo mkataba ....

Yaan hapa ni vita ya
Mliosikia kwa kuambiwa Vs Ngugai aliyeona mkataba ( me nafiiri ndugai yupo sahihi )
 
Kwani spika unataka kuniambia ndiyo kaliona hili leo? Kwanini bunge halikushauri enzi za uwepo wa jiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo mkataba ukiwekwa wazi ndo tutajua kua ni worth au not?
Saiv wengi wetu tunajadili cha kuambiwa na kusikia.
Pewen mkataba msome kwanza
Tunajadilije kitu tusichokijua?
 
Ni hao hao akina Ndugai waliomruhusu akajenge kila kitu chato.
 
Huna hoja ya kuthibitisha kauli yako, leta ushahidi juu ya mapungufu, maneno matupu hayaingii akilini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waache malomboso hao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…