Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,047
- 63,206
Husubiri nyumba ikamilike ndiyo upige plan. Una plan kwanza ndiyo unajenga. Nadhani jibu sahihi ungeelezea kwa undani kuwa hicho anachohofu hakiwezi kutokea.Ebu acha kwanza zikamilike then ndio tuanze kukosoa kwa sasa bado mapema.
Hii ndio sukuhisho ya msongamano wa magari. Nadhani malengo ya BRT sio kupunguza msongamano wa magari bali ni kuondoa magari binafsi ya abiria.Hebu sasa serikali ifikirie kujenga Subways na Metro jijini Dar. Hiyo inaweza kuwa effective zaidi kuliko haya mabarabara ya mwendokasi kila sehemu
Sasa huoni ukiondoa msongamano wa magari binafsi huoni kuwa umepunguza foleni?Hii ndio sukuhisho ya msongamano wa magari. Nadhani malengo ya BRT sio kupunguza msongamano wa magari bali ni kuondoa magari binafsi ya abiria.
Kwa jinsi jiji lilivyo busy, ni ngumu sana kuondoa magari binafsi yabakie magari ya mwendokasi.
Soma vizuri hoja yangu mkuu.Sasa huoni ukiondoa msongamano wa magari binafsi huoni kuwa umepunguza foleni?
Miradi ya Mwendokasi hata treni za mijini lengo ni kupunguza foleni. Sababu kukiwa na usafiri wa uhakika,watu hawa minyani na hawakai mda mrefu kituoni, hamna mtu atakaye tumia gari kwenda ofisini,yaani ktk watu kumi basi watu watakao tumia magari yao hawazidi watano.
Husubiri nyumba ikamilike ndiyo upige plan. Una plan kwanza ndiyo unajenga. Nadhani jibu sahihi ungeelezea kwa undani kuwa hicho anachohofu hakiwezi kutokea.
MkuuKwa kweli aliyekuja na mpango wa kupanua ujenzi wa Mwendokasi sijui kama alizingatia mipango ya awali ya namna jiji lenyewe lilivyo.
Inaonekana kilichofanyika ni kujaribu kuleta plan mpya juu ya plan ya zamani kabla hata ya kufanya mabadiliko makubwa ktk plan ya zamani.
Leo barabara za zamani zinaminywa ukubwa ili kujenga mwendokasi. Matokeo yake ni kuwa unaminya flow ya magari binafsi ili kutoka nafasi kwa magari ya kampuni moja ya mwendokasi, maana magari binafsi hayaruhusiwi kutumia njia ya mwendokasi. Hii kamwe haitotatua tatizo la misongamano ya magari bali inaweza kuzidisha.
Kibaya zaidi ktk kuminya barabara za magari ya kawaida, hata space kwa ajili ya watembea kwa miguu inakosekana. Hii ni disasater.
Ukiachilia mbali hilo, unakuta mavituo ya mwendokasi ni makuuubwa kwelikweli, sasa sijui unatengeneza kituo kikubwa cha mwendokasi ili iweje. Haya ni matumizi mabaya ya pesa
Ukienda mjini huko Posta, mwendokasi eti mwendokasi nayo imepenyezwa kwenye kipande cha barabara ya Tanganyika library na Posta, halafu kuna likituo likuuubwa pale wakati tayari posta ya zamani kuna likituo lingine kwa magari yanayotokea Ferry. Hii ni ajabu sana.
Hebu sasa serikali ifikirie kujenga Subways na Metro jijini Dar. Hiyo inaweza kuwa effective zaidi kuliko haya mabarabara ya mwendokasi kila sehemu
Hakuna kitu wanafanya.
Wanapaka rangi machuma ya kuingia vituo vya mwendokasi lakini mabasi mabovu 🤣🤣🤣.
Yani bora hata vituo visingejengwa lakini mabasi yakawepo.
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa.
Kupunguza unapunguza ndio najua mji unakuwa, magari yataongezeka na ndio maana serikaini kuna watu wa planning ndio kazi yao kudeal na future ya jiji, ila foleni unaipunguza hata kwa asilimia thelathini.Soma vizuri hoja yangu mkuu.
Kwa nature ya jiji la Dar na shughuli zake ni ngumu sana kumaliza msongamano wa magari. Hata hizo nchi ambazo zimeendekea na zinatumia metro bado barabara za pembeni zina magari mengi ingawa hakuna misongamano kwakuwa miundombunu yao iko vizuri gari zinatembea vizuri.
Mwendokasi kamwe haiwezi kuondoa msongamano wa magari. Kilichosaidia ni kuondoa vidaladala ndio maana unaona kuna unafuu. Magari binafsi bado yataendelea kuwepo hata zikiwekwa metro.
Ukirejea comment yangu ya awali utaona alichomaanisha mtoa mada na nilicho support ndio hiki umekieleza hapa. Mwendokasi inapunguza au kuondoa aina zingine za usafiri wa umma ila haziondoi msongamano wa magari. Hivyo njia zote zinapaswa kupewa kupaumbele sawa.Kupunguza unapunguza ndio najua mji unakuwa, magari yataongezeka na ndio maana serikaini kuna watu wa planning ndio kazi yao kudeal na future ya jiji, ila foleni unaipunguza hata kwa asilimia thelathini.
Mfano nchi kama China,US au India hivyi bila hizi mwendokasi,treni zao mjini we unazani foleni yake ingekuwaje, pamoja na kuwa na mtandao mkubwa wa barabara still bado foleni wanazo,ila foleni zingekuwa kubwa mnoo kama wasingekuwa na mwendokasi na hizi metro za mijini.
Nimekuulizwa swali simple pata picha China,India,US kama wasingekuwa na Mwendokasi au Metro hivi kwa sasa hali yao ingekuwaje?Ukirejea comment yangu ya awali utaona alichomaanisha mtoa mada na nilicho support ndio hiki umekieleza hapa. Mwendokasi inapunguza au kuondoa aina zingine za usafiri wa umma ila haziondoi msongamano wa magari. Hivyo njia zote zinapaswa kupewa kupaumbele sawa.
Umesema wafanyakazi wataacha magari, ni sawa ila wafanyakazi hapo Dar wenye magari ni wangapi, na kama msongamano unasababishwa na wafanyakazi, kwa nini muda wote barabara ziko busy. Ina maana wafanyakazi muda wote wako barabarani?
Tukubaliane tu kwamba mwendokasi inaondoa aina zingine za usafiri wa umma ila haziondoi msongamano wa magari.
Usilinganishe mabarabara mapana ya kule na vibarabara vidogodogo vya huku.Nimekuulizwa swali simple pata picha China,India,US kama wasingekuwa na Mwendokasi au Metro hivi kwa sasa hali yao ingekuwaje?
Kwani mimi nimesema muda wote kuna foleni?, foleni zipo asubuhi na jioni sababu watu wanawahi makazini na jioni wanarudi majumbani. Kwa kupaki magari kwa mda wa jioni na asubuhi utakuwa umepunguza magari mengi tu barabarani.
Kwani neno mfanyakazi ww unalielewaje?au unazani walio ajiriwa......?
Maana ni ngumu kukihudumia chombo cha usafiri kama huna kazi ya kukuingizia kipato tena cha uhakika.