Ujenzi gorofa na utaratibu wa mipaka

Ujenzi gorofa na utaratibu wa mipaka

Nina shida na jirani anajenga gorofa la sakafu 6, pamoja na underground parking.

Shida kubwa ni kwamba, hajafuata mwongozo wa kuacha nafasi ya kutosha kati ya jengo lake na ukuta unaotutenganisha. Hii sheria inatokea wapi?

Ningependa kuwa na uhakiki wa reference kama kuna member anafahamu. Pia ningependa kujua kama jirani ninaweza kuuliza mwonekano wa jengo.

Ili nifahamu kama baraza zinatazamia upande wangu.
Wewe unaonekana ni mtu mkorofi sana.
By the way, umbali ni mita moja kati ya jengo na mpaka wa kiwanja. Wewe pia unaacha moja, jumla zinakuwa mita mbili.
Kama hajajenga kwenye eneo lako, hakuna mgogoro hapo.
 
Kisheria nadhani ni Mita 1.5 kila mmoja. Jumla mita 3 kwa ajili ya majanga. Mfano Moto. Kuzuia usi sambae jengo la jirani.

Kwake, ana weza kuacha 1.5m distance kutoka fensini na ww uka acha 1.5m distance kutoka kwenye fensi kama mna share fensi (ukuta) mmoja. Watu hawataki kuacha space za uchochoro kuzuia wezi.
 
Mleta uzi ameuliza swali la msingi sana na anastahili majibu sahihi. Kisheria kuna umbali unaotakiwa uachwe na kila mwenye kiwanja kutoka kwenye uzio hadi ukuta wa nyumba. Na sababu zake zinajulikana; kwani kuna huduma zinapitaga kwenye hayo maeneo na vile vile usalama kati ya jirani na jirani. Mwizi asije akotoka ghorofa moja na kurukia ghorofa nyingine. kwa sasa naona ujenzi unakiuka hiyo sheria na sababu kubwa ni mjengaji kutaka kujenga nyumba kubwa kuliko kiwanja chenyewe na wakaguzi kuzembea au kupokea chochote!
Kisheria anatakiwa aache mita 1.5 kutoka kwenye ukuta unaowatenganisha. Ili hata akiendelea kujenga kwenda juu athari za vitu kudondokea upande wako zisiwe kubwa sana.
 
Kisheria anatakiwa aache mita 1.5 kutoka kwenye ukuta unaowatenganisha. Ili hata akiendelea kujenga kwenda juu athari za vitu kudondokea upande wako zisiwe kubwa sana.

Hii inategemea ukubwa wa kiwanja hata hivyo Kariakoo sio Mfano mzuri kwa sababu kulikua na Kariakoo Redevelopment Scheme iliyoainisha namna na layout za majengo.
Kabla ya kujenga je aliweka bango la ujenzi!! Je ulienda kupinga manispaa ujenzi wake!? Kama hukufanya na ujenzi unaendelea nenda mara moja au andika barua aje Engineer na
Watu wa Mazingira na maafa wakague. Usikae na janga ujenzi hatari ni kifooo.
 
Back
Top Bottom