Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?

Hyo nyumba Ina design mbayaa!!

Kaka nadhani hii ndo sababu mpaka imepelekea kuonekana cheap, kwa gharama Ni sawa kabisa Ila muonekano wake cheap
Kiukweli designer ndo kawapponza, mengine yote nayakubali, mi nimejenga 100 imeisha Ila nyumba haijaisha. Spanish tiles vyooni tu 3 mil 10
 
Wskati unaendelea na uchunguzi ukumbuke pia ujenzi wa nyumba za kuishi hizi za kwetu ujenzi wake ni tofauti sana na seeikali
Mbona unang'ang'ania ni TOFAUTI ni TOFAUTI muda wote... Kwani hizo za SERIKALI ZINAJENGWA MBINGUNI KWAMBA HATUZIONI? Acha uongo wa kizamani ww.. Hilo JENGO hata kama floor na wall yake wangetumia terrazo bado isingefikia hiyo bei.. hata fittings ziko cheap sana.. angalia ukubwa wa madirisha na milango utaona.. Material ya serikali yananunuliwa na watu hawa ambao kila siku tunakuwa nao ofisni na sisi wenyewe wahasibu ndio tunaandikia voucher hizo.. Acheni utetezi wa ajabu. HILO JENGO haliwezi fika mil 100. Hata uwaweke hao wasimamizi ambao kimsingi wana mshahara ambao ndio moja ya jukumu lao.
 
Nimekusamehe bure kwani una jina linafanana na jina mke wangu
 
Inategemea ni taratibu zipi za ujenzi zimetumika kuanzia 10% ya aliyeandaa ramani kulingana eneo la ujenzi, 10% ya aliyeandaa BOQ nk,kuna hostel imejengwa na TASAF hapa kijijini kwa milioni 75 lakini kilichotumika kwenye jengo ni 50milioni,hizo milioni 25 kuna gawio kuanzia kamati ya TASAF ya kijiji,Ofisi ya Afisa Mtendaji wa kijiji,kata Ofisi ya TASAF wilaya hadi ya mkoa.Je huu ulaji wote wa nini na wameweka katika utaratibu.Mwisho zile nyumba ndogo za NHC(National Housing Cooperation) za vyumba 2 na sebule unaambiwa milioni 32 hadi 46 je ni vipi?
 
Kama munashangaa hiyo nyumba Mil 140 JPM angewauliza viongozi wake wa CCM waliotumia Bil 6 kujenga Mnara wa Mapinduzi Zanzibar!
 
Watu wanaongea ushabiki tuu,tena unaweza kukuta kwenye hiyo hela hata ya supervision ilikuwa inatoka kwa manati.Ujenzi wa kutumia ratio ya 20 block/50kg cement bags tena vibrated (electrical power).Unakuta mchanga na kokoto zinatoka mbali,gharama za material ya finishing. Hizo gharama huenda zipo sawa ila kwa uoga na kujipendekeza kuna watu watakuja na ripoti kuwa kuna hela imepigwa.
 
You nailed it.
Kuna watu hawajawahi au wanakuwa na mihemko tuu ya kisiasa.Woga utapelekea watu waangushiwe jumba bovu bure,yaani kufanya justification ya matumizi kwenye ujenzi hakuketi shida yoyote.Kuna jengo moja nilishiriki kwenye Project Committee,tena tulikuwa tunafanya renovation/rehabilitation (BoQ_alikuwa karibu 170m).Kwenye uhalisia sasa tumefikia zaidi ya 190m kukamilisha jengo.
Hebu imagine ili ufyatue tofali inakubidi upate mchanga wa aina tofauti tofauti uchanganye (maana kuna maeneo hakuna mchanga unaotakiwa zaidi ya vumbi vumbi).Hiyo gharama hapo jamaa kwenye supervision wamemega na hela yao ya mshahara aisee.
 
Tena matirio hayo bado yanapelekwa maavara kupinwa ubora kwa gharama kubwa tu
 
Nyumba za serikali lzm zijengwe kwa ubora sio km nyumba y mtu binafsi. Lzm serikali iwe makini kwa hili tusiingiize siasa kwenye taaluma. Nyumba sio kusimamisha tofali. Tizama finishing ikoje. Tukienda hivi kutaka nyumba iwe 43m zitajengwa nyumba za miaka 5 km kambi za wakimbizi.
 

Kama TAKUKURU Mambo yako hivyo,

Je, huko mwingine hali ikoje.

Nyumba tatu (3) zimejengwa,

moja ni hiyo ya ofisi

mbili ziko mitaani za kuishi WAJANJA na familia zao.
 
Mheshimiwa Raisi yupo sahihi kabisa, kwa milioni 40 with effective supervision unajenga kama hiyo
Haivuki ml 45
Ukinipa M 143 nakuletea nyumba kama hiyo mbili na vimilioni vichache vinabaki.
Hii nyumba kama ni mimi mpaka hapo haizidi milioni 70
Mimi ukinipa 20 nakujengea.
Iyo kwa ml 143 mmmhh wizi mi sio injinia lakini kwa mtizamo wangu wamepiga hata ujengwe msingi mrefu kiasi gani
Sawa ila hata kama lakini haivuki 15
Million 70 safi kila kitu, tuache unafiki
Milioni 143, zinatoka nyumba kama hizo tatu [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2445][emoji2445][emoji2445][emoji377][emoji377][emoji377]
Pale layman (mwanasiasa) anapokua injinia tena structural engineer.

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Unaongelea nyumba standard ya taasisi ya serikali au banda la kufugia kuku?

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Vinavyochangia majengo ya serikali kuwa na gharama kubwa baadhi ni hizi:-
  • Mshauri - huyu naye analipwa kutokana na ujuzi wake (kampuni)
  • Meneja wa mradi- hii itategemea kama atatoka ndani ya taasisi au nje
  • Mkandarasi- hii ni kampuni iliyoajiri mafundi na vibarua kujenga hilo jengo (Kampuni)
  • Upimaji wa udongo- hii pia ni gharama (Kampuni)
  • Upimaji wa malighafi mf. kokoto,mchanga, mawe n.k
  • Kutumia malighafi zenye ubora wa hali ya juu- hii pia ni gharama
  • Kutumia uwiano unaokubalika- mfano;- kwenye zege, tofali, mchanga na simenti, n.k
 
Haiwez kuzidi million 50. Tena hiyo Ni kwa viwango vya juu sana. Hicho mbona ni kibanda cha uani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…