Ujenzi kutumia Interlocking blocks

Ujenzi kutumia Interlocking blocks

XhosaVica

Senior Member
Joined
Sep 29, 2020
Posts
157
Reaction score
155
Nimeangalia nchi nyingi katika ujenzi wanatumia Interlocking blocks. Je, kwa nini sioni ujenzi huu Tanzania?

Kuna mtu anaweza kutujulisha ni unaweza kusaidia kupunguza gharama za ujenzi kwa kiasi gani hasa wakati huu ambapo gharama za ujenzi zimepanda?

1613017553772.png
 
Nimeangalia nchi nyingi katika ujenzi wanatumia Interlocking blocks. Je kwa nini sioni ujenzi huu Tanzania?
Kuna mtu anaweza kutujulisha ni unaweza kusaidia kupunguza gharama za ujenzi kwa kiasi gani hasa wakati huu ambapo gharama za ujenzi zimepanda?
Bongo upo huo ujenzi sema gharama zake ni kubwa bora ujenge ya kawaida.
 
Ninachopendea baadhi ya design za interlocking blocks ni kwamba zina mwonekano mzuri, hata bila finishing inapendeza.

Pia ukiwa na tofali za kutosha, hata wiki mbili haziishi nyumba unahamia.

Zaidi ya hayo, zinapunguza sana drama za fundi ujenzi na zinasaidia makisio sahihi ya ujenzi wa Boma
 
Huu ujenzi ni maarufu sana kwa nchi ya India, ila hata Kenya wanauendeleza sana ukilinganisha na huku kwetu bado mapokeo si makubwa sana.

interlocking.jpg
 
Maeneo ambayo nyumba hizi zimejaa ni yale ambayo mchanga mweupe ni adimu.
 
Zile gharama za kupiga plasta zinawezwa kuingizwa kwenye tofari hizi
Sio plaster tu, la hasha bali hata mortar inayotumika kubond tofali na tofali, white cement/gypsum powder na rangi.

Kwa ufupi tukiweka mchanganuo hapa wa kujenga tofali za block/ brick na hizi interlocking basi gharama za ujenzi kwa tofali hizi za interlocking zitapungua sana almost 40%
 
Nimesubiri majibu kitambo sana kuhusu gharama za tofali na ujenzi. Ninataka kujenga eneo ambalo lina udongo mzuri wa kufyatulia. Kama kuna wafyatuaji, Je bei ni kiasi gani kwa tofali, kama tatizo ni mashine naweza kugharamia kukodi au kununua.
 
Nimesubiri majibu kitambo sana kuhusu gharama za tofali na ujenzi. Ninataka kujenga eneo ambalo lina udongo mzuri wa kufyatulia. Kama kuna wafyatuaji je bei ni kiasi gani kwa tofali, kama tatizo ni mashine naweza kugharamia kukodi au kununua
Mkuu sio kila udongo unafaa kutengenezea haya matofali, unatakiwa kufanya soil testing kujua kama unafaa au haufai. Udongo unaofaa unatakiwa uwe na composition ya 50% to 70% of sand. Usiseme tu mzuri sababu umeona una rangi ya tofali za kuchoma. Fanya soil testing kwanza kujiridhisha ili baadae usijepata kadhia ya tofali kumeguka

Kuhusu swala la mashine kama unataka kununua ili uweze kufyetulia tofali za kujengea nyumba tu na si kwa matumizi ya biashara ni heri ukanunue tofali, bali kama wataka kwa lengo la biashara ni sahihi ukanunua machine na faida yake ni kwamba itakusaidia kupata tofali zako na pili utaweza kuitumia kwa biashara pia.
 
Mkuu sio kila udongo unafaa kutengenezea haya matofali, unatakiwa kufanya soil testing kujua kama unafaa au haufai. Udongo unaofaa unatakiwa uwe na composition ya 50% to 70% of sand. Usiseme tu mzuri sababu umeona una rangi ya tofali za kuchoma...
Asante mkuu, maeneo nilipo tofali za kuchoma zinatumika sana, je hizi interlocking zina mahitaji tofauti ya udongo? Soil testing nitaizingatia. Vipi gharama kwa tofali 1
 
Asante mkuu, maeneo nilipo tofali za kuchoma zinatumika sana, je hizi interlocking zina mahitaji tofauti ya udongo? Soil testing nitaizingatia. Vipi gharama kwa tofali 1
Ndio, sio kila udongo unafaa, kama nilikueleza hapo juu udongo unaotakiwa ni wenye mchanganyiko wa sand ya 50 to 70 %. Ndio maana nikasema kabla ya kutumia huo udongo kufyetua tofali angalia kama composition ya sand katika huo udongo unarange katika hizo asilimia 50 mpaka 70.

Kuhusu gharama za tofali hizi naona kama hazina bei ambayo ni constant, kuna wengine jimeona wanaziuza 500 kwa tofali moja lenye ukubwa wa 300mm x 150mm x 100m, gharama za udongo na cement ikiwa juu yao wewe unafyetuliwa tofali zako hapohapo site
 
Mkuu sio kila udongo unafaa kutengenezea haya matofali, unatakiwa kufanya soil testing kujua kama unafaa au haufai. Udongo unaofaa unatakiwa uwe na composition ya 50% to 70% of sand. Usiseme tu mzuri sababu umeona una rangi ya tofali za kuchoma..
Wataalamu wake wanasema udongo mfinyanzi ndo unaofaaa.
 
Back
Top Bottom