Ujenzi kutumia Interlocking blocks

Ujenzi kutumia Interlocking blocks

Kumbuka hizi tofali zina dimension tofauti tofauti
Kuna Dimension hizi
1. 250mm x 125mm x 62.5mm
2. 250mm x 125mm x 65mm
3. 250mm x 125mm x 70mm
4. 250mm x 125mm x 72.5mm
5. 300mm x 150mm x 70mm
6. 300mm x 150mm x 75mm
7. 300mm x 150mm x 110mm
8. 300mm x 150mm x 140mm

Kwahiyo choice ni yako. Kuanzia namba tano mpaka namba 8 hizo size zimepishana kidogo sana na hizo tofali zetu tulizozizoea mtaani. Ila kama unataka muonekano mzuri sana hizi tofali ndogo zitakufaaa

Tukija kwenye mchanganuo hizi tofali huwa zinafidia gharama zingine kama plaster, skimming, rangi. Pia ni ujenzi wake hauna mambo mengi mfano badala yakukata ukuta uweke bomba za wire au maji hizi hutokata bali utapitisha kwenye yale matundu
Mkuu asante kwa maelezo,wewe ni fundi?kama ndio tuwekee namba yako hapa
 
Hapo umeongea kitu mkuu, tofali za kawaida zinaleta gharama mana lazima mortar,skimming,primer, na rangi tena..
 
Mkuu asante kwa maelezo,wewe ni fundi?kama ndio tuwekee namba yako hapa
Hapana mimi sio fundi, ni Mhandisi. Niko na kaproject nataka kutumia hizi tofali, nimeanza kuwekeza kwenye machine ingawa bado haijaisha.

Kwa miaka kama mitatu hivi nimekuwa nikijifunza namna ya kuzitumia hizi tofali, wabrazili wamekuwa msaada sana maana kwao wanazitumia sana hizi tofali
 
Changamoto ni machine, hapa Tanzania hamna watalamu wakutengeneza hizi machine. Ukitaka kuimport kutoka nje ni gharama sana.
1. Mfano manual Interlocking machine bila usafiri, kodi ni around Usd 1900 to 2000

2. Wakati ile ya Hydraulic interlocking machine ni around USD 3500 bila shipping na import tax.

Ingawa machine zao ni durable maana wao wanatumia laser kwenye welding na wanacast kwa Iron zile plate na mold box ukilinganisha na machine za Kichina mostly wanatumia Aluminium ambayo sio durable.

Machine za Brazil zinakuja na mold plate tofauti tofauti ambazo zinakuwezesha kutengeneza paving block kwakutumia udogo huo huo, na shape tofauti tofauti za tofali

Angalia hii catalogue za Verde Equipmental uone bei zao zilivyo. Hii ni fursa kwa wale ambao wana wazo la kufanya kama ujasiriamali.
View attachment Catalogo Verde 2020.pdf
 
gharama inapungua kidogo sana maana lazima kuwe na maungio yenye zege kali kwaajili ya kushikilia hayo matofali yasianguke, pia linta lazima iwe kali na ya ukweli vinginevyo ni kujiandalia majanga tu
 
Hizi ukijengea ukuta, panakuwa unyama sana kama ulaya
 
gharama inapungua kidogo sana maana lazima kuwe na maungio yenye zege kali kwaajili ya kushikilia hayo matofali yasianguke, pia linta lazima iwe kali na ya ukweli vinginevyo ni kujiandalia majanga tu
Kitu kingine covering area, kama sikosei ili tofali moja linaingia mara 3.45 ya tofali la block, ukizidisha x 500=1725 + (usafiri)=?
 
Back
Top Bottom