Ujenzi Mkubwa unaoendelea Kigamboni(Dege Eco Village), ni mradi wa nani?

Ujenzi Mkubwa unaoendelea Kigamboni(Dege Eco Village), ni mradi wa nani?

Kwa sasa umeme umefikia eneo la Camel Oil. Nimewataka Tanesco kuingiza kwenye Mipango yao mradi wa kufikisha umeme Mwasonga.
Kwa kupitia mradi umeme vijijini (REA) maeneo ya Kimbiji na Kisarawe II yatapata umeme. Kazi hii kwa sasa inaendelea.
Asante sana Mh. Mbunge kwa taarifa hii ila ningependa kutoa maombi mawili na kuulizwa swali moja.

Kwanza ni kuhusu kuiangalia upya barabara ya Kibada - Mwasonga. Ukarabati uliofanyika baada ya kuisha kwa msimu wa mvua haukuwa kiwango ambapo kilichofanyika ni kupitisha greda tu.

Hii imepelekea maeneo korofi kuchimbika mapema sana sababu hakuna kifusi kilichoongezwa na hasa ukitilia maanani kuwa barabara hiyo siku hizi inatumika na magari mazito ya sementi.

La pili ni kuomba kwamba utilie mkazo mradi huu wa umeme ili waty wa mwasonga tuweze kupiga hatua za maendeleo kwa haraka.

Na mwisho ni swali langu kutaka kujua ni lini mradi wa chuo cha kilimo cha wakorea Mwasonga utaanza ili wadau tujipange kuchangamkia fursa.

Asante
 
Barabara ya Kibada-Mwasonga imechongwa miezi miwili iliyopita kwa ajli ya ufunguzi wa Mwenge na wala sio planned imeishia kona ya kwenda Nyati Cement Kijaka
 
Dr F. Ndugulile tolea majibu post ya ndg king kong kuhusu huyo akbaru.

Then haina maana kuja mbele ya public kujifanya unajibu hoja za wananchi halafu unaishia kujibu hoja nyepesi ambazo unaona zina kuongezea umaarufu halafu unaacha hoja nzito na zenye msingi zaidi.

Hatupo hapa kusifia mazuri sababu kufanya mazuri ni wajibu wa kiongozi na binadamu yoyote yule kwahiyo haihitaji kusifiwa.Sisi tunataka kuongelea maovu na ukiukwaji wa taratibu kama hili swala lako.

CC Dr F. Ndugulile

Ningependa sana kusikia majibu ya Mh Ndugulile kwa swali la king kong kuhusu bwana Aqbal kumiliki mashamba kwa zaidi ya miaka mitatu bila kuyaendeleza na bado anatazamwa tu.. Kwa nini sheria haichukui mkondo wake?

Dawa ya Huyo Akbaru ni kuyachukua kinguvu hayo maeneo au kupeleka shauri kwenye mahakama za zinazoshughulikia ardhi ili anyang'anywe maana hayajaendeleza kwa zaidi ya miaka mi3,serikali inasisitiza kilimo kwanza huku wao wenyewe hawa walk the talk!
 
September 23, 2014
Mradi wa nyumba unaosimamiwa na kampuni ya Hifadhi inayoitwa Dege Eco-Village umeshiriki maonyesho ya nyumba yaliyoanza kufanyika jijini Dar es Salaam jana.

Wakati Meneja Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village akiongea alisema “Kwa sasa ujenzi unaendelea na karibu aina ya nyumba (apartment) 3000 zitakuwa tayari ifikapo Januari 2015. Aliongezea kusema kwamba kupitia mradi huu waTanzania watanufaika kwa kupata ajira na pia kuwa na huduma kama hospitali, shule na maduka katika eneo la Kigamboni.

Mradi huo unajengwa kwenye eneo takriban heka 300 na kampuni hiyo imewekeza zaidi ya dola milioni 350. Kwa ujumla nyumba aina ya villa ziko 300 na apartment ziko 7400. Mradi huu utakamilika mwaka 2018. Apartment zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018.

Ndani ya mji huu wa Dege Eco-Village wakazi hawatahitaji kwenda popote kwasababu kila kitu kitakuwepo kama shule za watoto, kituo cha polisi, hospitali, supermarket, na kadhalika.

IMG_9549.jpg
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo,Bw. Azhar Malik akiefafanua juu ya mradi huo wa Dege Eco Village kwa wateja wapitao katika banda lao (hawapo pichani).

Source: Michuzi Blog MICHUZI BLOG: MRADI WA NYUMBA WA DEGE ECO-VILLAGE WAANZA
 
Kwa mujibu wamaelezona mapitio ni mradi wa uwekezaji katika ujenzi reason ni kuwa Jiji la Dar ni la 3 kwa ukuaji wa haraka Afrika na la 9 Duniani so those with money incorporate with NSSF they have decided to invest in that matter kama kuna behind that may I don't know.
 
Na Mkuranga nayo ina Wachina kibao wanatengeneza yebo yebo, tunakula nao kuku wa kienyeji mitaa ya Dundani/Mwanambaya. Mitaa ya Kisemvule kwenda mbele ni Hwang Hoo.

Hivi kina Tembo bado wapo Dundani?
 
Hivi kina Tembo bado wapo Dundani?

Dadaaa weee,

Hawa jamaa ni noma sana, nini tembo, hamna kima, wala mbwa wala mijusi mitaa ile, kila kitambaacho juu ya Dundani kinaliwa. Kunguru wa Zanzibar ndio wako salama.
 
Dadaaa weee,

Hawa jamaa ni noma sana, nini tembo, hamna kima, wala mbwa wala mijusi mitaa ile, kila kitambaacho juu ya Dundani kinaliwa. Kunguru wa Zanzibar ndio wako salama.

Si tembo nauliza akina Tembo, ni ukoo huo walikuwa hapo Dundani na Kariakoo, Udoe street. Maana Udoe naona nyumba yao waliiuza limekuwa ghorofa.

Ndiyo nauliza Dundani bado wapo? Au na huko wameshavuta ndefu?
 
Si tembo nauliza akina Tembo, ni ukoo huo walikuwa hapo Dundani na Kariakoo, Udoe street. Maana Udoe naona nyumba yao waliiuza limekuwa ghorofa. Ndiyo nauliza Dundani bado wapo? Au na huko wameshavuta ndefu?

Unasema akina Tembo Wazaramo wenzangu, lile eneo la kulia kama unakwenda Mkuranga walishavuta mkwanja, na wao wamejenga fremu nyingi mkono wa kushoto kabla ya msikiti. Tatizo zile fremu zao hazijapata wateja.
 
Tuna shukuru kwa kujibu hoja zetu kwa usahihi Mh. Mbunge Dr F. Ndugulile;

Nipende kuuliza kama kuna mpango wa haraka wa kuikarabati barabara ya Kibada- Mwasonga katika hadhi ya lami? Kama ndio ni lini?

Kwani umuhimu wake ni mkubwa sana kwa sasa.
 
Ngone tusubiri tuone mwisho wake. Kuna miradi kama hii kadhaa iliyoanza kama huu.
(1) Mradi wa Pruitt-Igoe huko Marekani
(2) Mradi wa Nova Cidade de Kilamba huko Angola
(3) China Manhattan Project huko China

Huo wa kwanza ulijifia kifo cha mende; huo wa pili na huo wa tatu inasemekana ziko kwenye life support. Mambo haya huhitaji balance kubwa sana baina ya supply na demand.
 
Dr F. Ndugulile, wewe ni mmoja wa wabunge wa CCM waliojitahidi kuusimamia ukweli hata kuchukiwa na CCM wenzako.

Mwaka huu CCM wakionesha dalili ya kutokutaka wewe...hamia CHADEMA ...Utashinda saa 3 asubuhi
 
@Dr F.Ndungulile wewe ni mmoja wa wabunge wa CCM waliojitahidi kuusimamia ukweli hata kuchukiwa na CCM wenzako.

Mwaka huu CCM wakionesha dalili ya kutokutaka wewe...hamia CHADEMA ...Utashinda saa 3 asubuhi

CC @Dr F.Ndungulile
Daaah!!
 
Hivi wakuu, na huu mradi wa Avic city unaendeleaje?

Any comment!?

Nafikiria kuinvest kwenye huo mradi. Ni mradi upi nafuu kati ya huu wa Avic na Dege
cc.
Dr F. Ndugulile, Kichuguu, Pasco
 
Last edited by a moderator:
Hivi wakuu, na huu mradi wa Avic city unaendeleaje?

Any comment!?

Nafikiria kuinvest kwenye huo mradi. Ni mradi upi nafuu kati ya huu wa Avic na Dege

Google mkuu, miradi yote hiyo miwili ina website zenye details za kutosha ila kwa kifupi Nyumba zao si chini ya 100M
 
Google mkuu, miradi yote hiyo miwili ina website zenye details za kutosha ila kwa kifupi Nyumba zao si chini ya 100M

Mkuu, asante kwa majibu. Nimegoogle lakini hakuna bei kwenye website zao, only NHC. Nimejaribu kupiga simu hawapokei na e-mail hazijibiwi. Nimeamua kuandika ili kupata opinion!!
 
Back
Top Bottom