Ujenzi mtambo wa kusafisha mafuta Jiji Tanga naipongeza serekali

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
21,490
Reaction score
38,302
Heshima sana wanajamvi,

Kati ya mambo yaliyonisikitisha ni mwaka huu ni mradi wa ujenzi kuhamishiwa Mombasa.

Nilimsikia Rais Ruto na baadae Rais Samia.
Kauli ya Dangote ya kupeleka mradi Kenya ilinipasua moyo wangu vipande vipande.Nilimchukia,nilimwona ni tajiri mwenye nyodo za kipuuzi.

Hakika ziara ya Kaguta nchini Tanzania ilinirejeshea furaha isiyo kifani.

Ngongo kwasasa Tanga.
 
Naunga mkono hoja https://www.jamiiforums.com/threads...umi-tutaweza-kuwalinda-mashujaa-hawa.2460523/
P
 
Usiwe mpumbavu sana, SGR ni mradi wa $10b , hadi leo haujakamilika na haifahamiki utakamilika lini, kisha usikie kuna mradi mwingine wa $10b unawekewa sign?!

Kwa taarifa yako, huyo Museveni aliwahi kupewa eneo kwenye bandari ya Tanga na utawala wa Mkapa, lengo lilikuwa ni kujenga bandari ya kupokelea na kusafirisha bidhaa za Uganda, hadi leo hawajawahi hata kuleta matofali mabovu 50
 
SGR nimeshaitumia nikitokea Dar hadi Dodoma.

Nadhani njia ya mabus Dar,Moro & Dodoma wanalijua hilo.

Naamini mradi wa SGR utakamilika tu ingawa kwa kusua sua.

Usisahau bomba la mafuta M7 katuletea Tanzania badala ya kulipeleka Kenya.
 
SGR nimeshaitumia nikitokea Dar hadi Dodoma.

Nadhani njia ya mabus Dar,Moro & Dodoma wanalijua hilo.

Naamini mradi wa SGR utakamilika tu ingawa kwa kusua sua.
Mmejipangaje kupata fedha za kukamilisha mradi katika mazingira ambayo beberu amekata mrija?
 
Naamini hilo suala litapatiwa ufumbuzi soon.

Mosi naamini mazingira bora ya siasa yatatatuliwa kupitia katiba mpya.

Pili naamini uchaguzi wa 2030 utakuwa huru na haki.

Tatu naamini Tanzania itapata katiba mpya.
 
Katiba mpya ipi?
Wakati Makamu wa Rais anahimiza watu wapambanie Katiba mpya, tunaona wapambe wa Rais wanahimiza Katiba iliyopo ni bora, hayo matumaini ya Katiba mpya unayatoa wapi?

Halafu watu wengi waliopo CCM wamepata nafasi za uongozi pasipokuwa na sifa za kuwa viongozi, watu kama Paul Makonda hawakufaa kuwa hata mabalozi wa nyumba 10. Huo uchaguzi huru na haki utapatikana kwa misingi ipi?
 
Katiba mpya ipi?
Wakati Makamu wa Rais anahimiza watu wapambanie Katiba mpya, tunaona wapambe wa Rais wanahimiza Katiba iliyopo ni bora, hayo matumaini ya Katiba mpya unayatoa wapi?
Yapo ktk ilani ya CCM.
 
Heshima sana wanajamvi,

Kati ya mambo yaliyonisikitisha ni mwaka huu ni mradi wa ujenzi kuhamishiwa Mombasa.

Nilimsikia Rais Ruto na baadae Rais Samia.
Kauli ya Dangote ya kupeleka mradi Kenya ilinipasua moyo wangu vipande vipande.Nilimchukia,nilimwona ni tajiri mwenye nyodo za kipuuzi.

Hakika ziara ya Kaguta nchini Tanzania ilinirejeshea furaha isiyo kifani.

Ngongo kwasasa Tanga.
Kwenye hii Dunia unaamini serikali kuwekeza yenyewe huu ni ujinga kama sio upambuvu wa kurudia makosa Yale Yale

Hii ni akili ya kizamani sana ya mwaka wa 48

Kwenye hii Dunia ya kisasa serikali inatakiwa itengeneza MAZINGIRA na sera nzuri Kwa wawekezaji Ili waweke mitaji Yao

Tumepoteza mabillion ya walipa Kodi maskini kwenye miradi mingi ya fikra za kizamani
 
Back
Top Bottom