Ujenzi: Nimefanya uchunguzi kwanini watu wengi wanashindwa au kuchelewa kuwa na kwao

Ujenzi: Nimefanya uchunguzi kwanini watu wengi wanashindwa au kuchelewa kuwa na kwao

Unafuu upo wapi? ni kwa mkopo au
Dah...gharama za maisha mkuu...wengi tunawaona wanajenga mahekalu Mkoa wa Pwani….wanahamia lakini miezi 2 tu wanarudi tubanana huku mjini kati….mahekalu wanainjoi vijana wa bustani ....labda kama unatumia nguvu ya wavuja jasho (STL) 🤭
 
Msipende kuangalia ujenzi na gharama ya umbali na eneo la kazi na kupiga hesabu hivi this is too wrong, itafika mahala hutataka kujenga kabisa useme upange mjini karibu na offisi, kwani ukijenga mbali ukapangisha nyumba hile kodi ikawa ndiyo inakulipia apartment mjini karibu na eneo la kazi huoni utakua umetatua tatizo na bado unakua na asset yako ya nyumba hata kazi ukiachishwa au ukiacha utaenda kuhamia huko kwako?

Kujenga mbali faida moja kuu ni kupata kiwanja kwa bei ndogo na pia utamakiza ujenzi bila vikwazo, nyumba ni asset na ni permanent asset, kazi haiwezi kuwa ya kudumu kuna kufukuzwa kazi, kustaafu nk
Dah...mkuu sijasema kwamba usijenge nje ya mjini…..nilichokizungumzia ni kuangalia gharama za Maisha...na Maisha ya baadaye...kama ukinunua apartment katikati ya jiji...ni asset yenye thamani kubwa kuliko nyumba kubwa iliyo nje mji...kama ukikomaa kufanya kazi tuseme 20yrs...utakopa ...utalipa deni na kujenga nyumba nje ya mji pia kuwa na uhakika wa kipato ukichoka….
 
Wakati tukiendelea na majadiliano napenda kuwapa mrejesho kama mleta mada hii.
Kama mnavyoona kwenye picha hiyo ndio nyumba ambayo nilianza kujenga na sasa nimefikia stage hiyo.

Mpaka hapo unapoona sina popote nilipoathirika hasa kibiashara na uchumi kiujumla na hiyo yote ni sababu nilimaua kujenga nyumba ya uwezo wangu na sio nyumba ya ndoto zangu.View attachment 1626766
Hongera sana, Nimevutiwa.
 
Dah...gharama za maisha mkuu...wengi tunawaona wanajenga mahekalu Mkoa wa Pwani….wanahamia lakini miezi 2 tu wanarudi tubanana huku mjini kati….mahekalu wanainjoi vijana wa bustani ....labda kama unatumia nguvu ya wavuja jasho (STL) [emoji2960]
Wahindi huwa sio hulka yao kujenga na wewe ni mhindi mkuu
 
Dah...mkuu sijasema kwamba usijenge nje ya mjini…..nilichokizungumzia ni kuangalia gharama za Maisha...na Maisha ya baadaye...kama ukinunua apartment katikati ya jiji...ni asset yenye thamani kubwa kuliko nyumba kubwa iliyo nje mji...kama ukikomaa kufanya kazi tuseme 20yrs...utakopa ...utalipa deni na kujenga nyumba nje ya mji pia kuwa na uhakika wa kipato ukichoka….
Ukinunua kiwanja mjini sasa si utaishia kununua kiwanja tu hela ya ujenzi utatoa wapi, bei ya viwanja mjini ni 30,20,15 m sasa bado hujaanza ujenzi, ujenzi ni mipango
 
Sahihi boss wangu, idea nishapata hapa zimepelea hela za kujengea tu...ndio nimekuja nipate dili mbili tatu toka kwako[emoji4]
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Sasa situjenge tu pamoja eti happiness , kweli nakujengea halafu unaenda kuyaishi maisha mazuri peke yako, ngoja niangalie salio jiandae kusinamia ujenzi
 
Kwa wakazi wengi wa mjini kuna jambo moja ambalo limekuwa kizungumkuti sana kwa watu wengi hasa sisi wa uchumi mdogo.

Hakuna mtu anayependa kuishi kwenye Nyumba za kupanga hivyo kila mtu anapenda kujenga awe na kwake, mahala ambapo atakuwa huru kufanya anavyotaka yeye.

Nimefanya uchunguzi ni kwanini watu wengi wanashindwa au kuchelewa kuwa na kwao.

1. Watu wengi wanaogopa kujenga, yaani mtu anakuwa anasubiri awe na pesa nyingi ndio aanze ujenzi.
Mara nyingi kadiri mtu umri unavyoongezeka na majukumu nayo huongezeka hivyo kipato hakitaruhusu uwe na pesa nyingi

2. Watu wanatamani vitu ambavyo hawana uwezo navyo. Jirani yangu kuna mama alipata pesa yake kiasi akaamua kwenda kuanza ujenzi kwenye kiwanja chake, pasipo kufanya tathmini ya uchumi wake alianzisha msingi wa jumba kubwa kiasi kwamba pesa aliyokuwa nayo yote iliishia kwenye msingi.

Mpaka sasa anajikongoja lakini kutokana na ukubwa wa nyumba basi imesogea mpaka kwenye madirisha ndani ya miaka kama mitano sasa. Lakini ukipiga hesabu vizuri ni kwamba pesa aliyokwisha tumia angeweza kujenga nyumba ndogo angalau ya vyumba viwili na sebule na leo angekuwa anaishi kwake.

So tukadirie haya mambo
Mimi watu wengi wananishangaaga nawezaaje kufanya kazi nyingi ndani ya muda mfupi kwa kutumia rasilimali Kidogo. Siri wasioijua ni kuwa ,binafsi nawaamani watu na taaluma zao. Mi nilimchukua ndugu yangu mjenzi, nikamchorea ramani ya nyumba ndogo nitakayo. Akanitajia gharama za materials na ufundi wake. Nikamkabidhi materials yote kama milioni 8 na yeye nikampa milioni 2, jumla milioni 10. Baada ya siku 45 akanipa funguo za mjengo huu , nimehamia, vingiine ntamalizia nikiwa ndani. Nafight hivi sasa, nipate kausafiri simple.
IMG_20201029_123359_1.jpg
IMG_20201029_123326_1.jpg
IMG_20201029_124101_1.jpg
Ramani Simple.jpeg
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Sasa situjenge tu pamoja eti happiness , kweli nakujengea halafu unaenda kuyaishi maisha mazuri peke yako, ngoja niangalie salio jiandae kusinamia ujenzi
[emoji23][emoji23] Nakuombea herii mimi, nikagombane na mafundi site
 
Finishing unaweza ukafanya mdogo mdogo ,Kupaua ndio issue maana lazima uwe na pesa yote kwa pamoja ,hela ya mbao,hela ya ufundi,hela ya misumali na hela ya bati.

Hakika, nimefikia hatua hii ikabidi nitulie kwanza kujitafakari na kutunza kila senti ninayopata ili nikamilishe hatua hii.
 
Hakika, nimefikia hatua hii ikabidi nitulie kwanza kujitafakari na kutunza kila senti ninayopata ili nikamilishe hatua hii.
Hapo kuna mziki ,lazima ujipange kujichanga,lazima uwe na mpunga wote wa kuezeka.
 
Mimi watu wengi wananishangaaga nawezaaje kufanya kazi nyingi ndani ya muda mfupi kwa kutumia rasilimali Kidogo. Siri wasioijua ni kuwa ,binafsi nawaamani watu na taaluma zao. Mi nilimchukua ndugu yangu mjenzi, nikamchorea ramani ya nyumba ndogo nitakayo. Akanitajia gharama za materials na ufundi wake. Nikamkabidhi materials yote kama milioni 8 na yeye nikampa milioni 2, jumla milioni 10. Baada ya siku 45 akanipa funguo za mjengo huu , nimehamia, vingiine ntamalizia nikiwa ndani. Nafight hivi sasa, nipate kausafiri simple.
View attachment 1629185View attachment 1629186View attachment 1629188View attachment 1629193
We jamaa si nimeona hii nyumba unaonesha jukwaa mbalimbali kuwa unawajengea watu kwa 12m?

Mara hii imekuwa yako na umejenga kwa 10m?[emoji849][emoji849][emoji15]

Na aliyekujengea ni ndugu yako?[emoji23][emoji23][emoji1745]

Kweli za kuambiwa + na zak..
 
Back
Top Bottom