RAYAN THE DON
JF-Expert Member
- Aug 21, 2019
- 679
- 1,220
Hapo sawa mkuu. Ngoja nipambane.Noooo [emoji38][emoji38][emoji38] nitakupa ushauri ni jokes tu hizo boss, ila mzee vyumba 6 ni mjumba sio nyumba, ila kuna plan za kufanya kaa na mafundi boss weka nao mikakati, mafundi wanatakiwa wajue una hela kidogo hata kama una milion 100 ili uoate ushauri halisi, unakaa nao na kuwauliza nataka kumalizia hapa nafanyaje na hela inakata!!? Watakupa ushauri na utatoboa boss
aya ndio mambo ya watu weusi mtu unakaa kwenye nyumba ya serikali miaka nenda rudi unashindwa kununua kakiwanja na kujenga kajumba kako matokeo yake mnaanza kutolewa balu kama mbwa aibu kubwa sana hapa kuna kitu cha kujifunzaMfano yuke mama wa zenji imenisikitisha na inatia huruma, mume wake alikua na kazi serikalini wakawa wanakaa kwenye nyuma ya serikali mume wake kafa akalazimishwa kutoka kwenye nyumba kinguvu, sasa wakati wanamuhoji anasema hajui pakwenda waende wapi inasikitisha sana
Kuna mtu anazaliwa sehemu ya kulala kwake sio shida. Kuna mtu anazaliwa hao waliomzaa na babu zao bado sehemu ya kulala ni shida.Mpe mbongo bilioni 10 atajenga mijumba akitegemea kurejesha mapesa yake baada ya miaka 10 hadi 20.
Mpe msomali bilioni 10 atafungua maduka makubwa, ata import na kukuza biashara zake kwa eneo husika.
Mpe Muhindi bilioni 10 ataanzisha kiwanda kitakua kikubwa na atapiga pesa kwa muda mrefu.
Ujumbe tusifikirie kujenga sana tuache dhana ya uoga 😂😂😂😂😂
Yote uliyoyataja nakuhakikishia kama umedhamiria na umeweka nia yanawezekana pasipo shaka, watanzania wengi tuna uoga fulani hivi wa kujaribu au kutembea na fursa, kuna ile dhana ya kuogopa au kuhisi utashindwa hilo ndio tatizo kubwa.Ila mkuu mimi siwezi kumcheka mbongo anayejenga nyumba nitamcheka ambaye amehonga pesa na kunywea pombe.
Haya mambo yanaendana na tamaduni mkuu huwa hatuigani kwenye maisha.
Wahindi kitu kingine wana elimu na connection kubwa ya mambo ya biashara.
Kwa mfano utakuta muhindi yupo Bongo lakini kuna ndugu zake wapo Zambia,South Africa,Dubai,Canada,China wanafanya biashara kubwa kubwa.
Kwa hyo mtu kama huyu akifungua biashara hawezi kuyumba,coz anapoanzisha tayari anakuwa na plans zake kichwani kwamba bidhaa fulani nitachukua zambia,zingine nitachukua South Africa kwa bei fulani,zingine nitachukua Dubai kwa bei fulani na nikishafikisha bongo nitauza kwa bei fulani tena kwa haraka.
Lakini mwenzangu na mimi hujawahi kufanya biashara na wala Dubai/SA/China hujawahi kufika unapasikia tu siku ukienda kwa mara ya kwanza unaanza kushangaa shangaa mwishowe unaishia kutapeliwa tu pesa.
Na kingine pia wana ushirikiano sana ikitokea mmoja wapo amefirisika watamchangia hadi ainuke tena.
Lakini huku bongo ukifirisika ndio basi tena unabaki kuchekwa na kuzomewa tu.
Kwa hiyo ukiona mtu anajenga mijumba ule ni uoga anajihami asije kuja kuchekwa baadae akifulia.
Yote uliyoyataja nakuhakikishia kama umedhamiria na umeweka nia yanawezekana pasipo shaka, watanzania wengi tuna uoga fulani hivi wa kujaribu au kutembea na fursa, kuna ile dhana ya kuogopa au kuhisi utashindwa hilo ndio tatizo kubwa.
Unakuta mtu ana milioni 10 benki anaogopa kufanya biashara anangojea miambilimbili anazopewa na benki, kumbe huku mtaani kuna chinga anapiga pesa nyingi tu na hana hata huo mtaji alio nao mwenye milioni 10.
Linawezekana mkuuHapo sawa mkuu. Ngoja nipambane.
Binafsi naamini kufeli ni njia nzuri zaidi ya kujifunza namna ya kufaulu, kwasababu kuanzisha kitu mpaka kifanikiwe lazima ukumbane na changamoto ili kesho yake ujifunze namna ya kuzikwepa, kama unaanzisha biashara inaanguka unakimbilia kuanzisha project nyingine nayo inafeli, utaendelea kufeli kwasababu hujajua bado unafeli wapi.I agree by 50% sio wote waliothubutu kuingiza pesa kwenye biashara walifanikiwa karibu theluthi mbili huwa wanafirisika.
Halafu ukiangalia hiyo nyumba walivyo iboresha utafikiri hawatakuja kuhama, yani nyumba ya serikali unaifanyia ukarabati asilimia 100 kama ndiyo umeinunua? sasa wanataka nyumba yao mama kabomoa hadi tiles, mama analalamika hajui atawapeleka wapi watoto hana pakwenda, tustuke eti hii ni aibuaya ndio mambo ya watu weusi mtu unakaa kwenye nyumba ya serikali miaka nenda rudi unashindwa kununua kakiwanja na kujenga kajumba kako matokeo yake mnaanza kutolewa balu kama mbwa aibu kubwa sana hapa kuna kitu cha kujifunza
Umeongea kisomi sana, umeongea vyema sana mkuuBinafsi naamini kufeli ni njia nzuri zaidi ya kujifunza namna ya kufaulu, kwasababu kuanzisha kitu mpaka kifanikiwe lazima ukumbane na changamoto ili kesho yake ujifunze namna ya kuzikwepa, kama unaanzisha biashara inaanguka unakimbilia kuanzisha project nyingine nayo inafeli, utaendelea kufeli kwasababu hujajua bado unafeli wapi.
Huu ni mtizamo wangu binafsi.
Mkuu naomba kuuliza; Hivi kujenga nyumba nusu nusu, haiwezi kuleta shida ya nyufa pale kwenye maungio...kwamba umejenga, halafu ukaacha matofali yaliyotokelezea pale..Haya unayosema kiongozi ni sahihi ,mimi nimejenga nyumba ya ndoto yangu ila kidogo kidogo ,..
Nilichofanya ni kuwa na ramani ya nyumba nayoitaka, kisha nikaanza kuinyanyuwa vyumba viwili ambavyo master na nashukuru haikuchukua muda sana, japo nayo imenigharimu kulingana na aina ya ujenzi niliotaka.
Maana nilitaka nijenge nyumba ambayo zitakuja kujutia baadae au kuja kujenga tena, kwa hiyo nilijitahidi kujenga kila kitu katika kiwango bora ila kama ningetaka nimalize ramani yote nahisi mpaka yesu angerudi angenikuta nipo kwenye msingi ama linta na sijapauwa sijui napauwa lini.
Kwa wapambanaji kufeli ni kawaida tu mkuu. Haijalishi umefeli mara ngapi ila ipo siku utanyanyuka tu. Mfano mzuri ni mimi mwenyewe. Nilishawahi kuwekeza katika mradi wa Mpe-sa na tigo pesa ila watafutaji wanaotumia nguvu kubwa kutafuta wakanifilisi nikawa zero. But baadae nikanyanyuka nikaanzisha duka la vipodozi nikaangukia pua tena but today as we speak namshukuru Mungu mambo siyo mabaya yanaenda vizuri sana.Binafsi naamini kufeli ni njia nzuri zaidi ya kujifunza namna ya kufaulu, kwasababu kuanzisha kitu mpaka kifanikiwe lazima ukumbane na changamoto ili kesho yake ujifunze namna ya kuzikwepa, kama unaanzisha biashara inaanguka unakimbilia kuanzisha project nyingine nayo inafeli, utaendelea kufeli kwasababu hujajua bado unafeli wapi.
Huu ni mtizamo wangu binafsi.
Mimi bado nitakua kwa mbongo naona amewaza vyema, we endelea kuwasifia hao wengine, ni hivi kwenye biashara ni lazima uwe risk taker unakuta hiyo pesa uliochukua kama mkopo kwa mfano kipindi kama hicho cha corona ambapo imeathiri uchumi kwa kiasi kikubwa hivi hiyo pesa ya marejesho unaipataje? kama umeweka huko na hii coroma ndiyo imepotea hivyo na bado unahitajika marejesho au faida, mbongo idea yake ya nyumba kwanza nampa like yes unamega kiasi kidogo unajenga nyumba kinachobaki unafungua biashara, ni heri kuwa muoga usipoteze kuliko kuwa mwerevu lakini mjinga tu na kupata hasara tuMpe mbongo bilioni 10 atajenga mijumba akitegemea kurejesha mapesa yake baada ya miaka 10 hadi 20.
Mpe msomali bilioni 10 atafungua maduka makubwa, ata import na kukuza biashara zake kwa eneo husika.
Mpe Muhindi bilioni 10 ataanzisha kiwanda kitakua kikubwa na atapiga pesa kwa muda mrefu.
Ujumbe tusifikirie kujenga sana tuache dhana ya uoga [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
mkuu hakuna kitu kikubwa hapa duniani kama kuwa na umaskini wa fikra, waliwezaje kukarabati nyumba ya serikali badala ya kutumia iyo pesa kwenda kujenga makazi yake binafsi na familia yake, labda walijua watapata huruma ya serikali kwakuwa wameikarabati iyo nyumba embu angalia aibu hii na fedhea waliyopata.Halafu ukiangalia hiyo nyumba walivyo iboresha utafikiri hawatakuja kuhama, yani nyumba ya serikali unaifanyia ukarabati asilimia 100 kama ndiyo umeinunua? sasa wanataka nyumba yao mama kabomoa hadi tiles, mama analalamika hajui atawapeleka wapi watoto hana pakwenda, tustuke eti hii ni aibu
Hizo ni theories za motivational speakers tu.Umeongea kisomi sana, umeongea vyema sana mkuu
=Architect na sio architecture.Nilikuwa nawaza sana suala la ujenzi. Nikishaenda kwa architecture akanichorea ramani moja tamu sana ila nilipopiga hesabu nikagundua ile nyumba ili niikamilisha basi itanipasa kupambana na kuitesekea sio chini ya miaka 10.
Ni kweli kiongozi unajua watu huwa tunatishana chakwanza kwenye ujenzi na pili watu kutaka mambo makubwa kwa haraka ,mtu ana plani kujenga gorofa anadhani gorofa ni kitu kidogo , gorofa yataka ujiminye na uwe na kipato cha kueleweka au uwe kwako unajenga mdogo mdogo ,lkn ukilipigia mahesabu ukiwa nyumba ya kupanga alafu kipato cha kuunga unga huku unalipa kodi kubwa ww utahamia kwako ukiwa kaburini ,We muache ipo siku atakukumbuka, na majuto kibao ndiyo dawa ya watu wabishi majuto kwao ndiyo mafundisho,
Huwezi kumaliza kila kitu unahamia na vingine vinaendelea wakati upo kwako, mdogo mdogo, aiseehh mbona unamaliza, tena ni kwako kwanza unakua na shauku na raha kupamaliza yani ukipata hela tu huyo unakimbilia site[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787], nyumba za kupanga kuna kero sana, sisajua huyo dada anazifurahiaje,
Yani ujenzi uneletaga raha sana ukiwa unajenga kwako asikuambie mtu, kama mtu unajinyima unajenga kwako ni jambo la heri, jioni nilikua natoka na mafundi site nakaa nao mahali nawapa vinywaji nawambia nataka kumaliza kitu fulani ila hela imekata, wananipa moyo napata ushauri aiseeeh najikuata nimemaliza, so ushirikiano na mafundi pia umenisaidia sana sana
Mkuu inategemea na aina ya ujenzi unaojenga ,ukijenga kidogokidogo kwa umakini na ukapata fundi mzuri kwanza huwezi jua imejengwa kiswahili au kwa kuungwa ungwa , na pia hakikisha unapata fundi wako mmoja unaanza nae mwanzo mpaka mwisho ,Mkuu naomba kuuliza; Hivi kujenga nyumba nusu nusu, haiwezi kuleta shida ya nyufa pale kwenye maungio...kwamba umejenga, halafu ukaacha matofali yaliyotokelezea pale..
Naomba kujua.
Mungu atakusaidia mkuu ,kama unavyosema kujenga mipango ,ukiwa na mipango ukajiwekea mikakati kidogokidogo basi mwisho wa siku utajikuta unafikia lengo ,unajuwa wengi wanataka mambo makubwa kwa haraka na haiwezekani ,kujenga ni mipango jamani na sio upate mabilioni ndio ujenge, nina kieneo changu pembeni kidogo mwa mji nimeanza kufyatua matofali yangu kipato nachopata najitaidi kukigawa kidogo kila mwezi natumai baada ya mda kidogo malengo yangu yatatimia isitoshe ujenzi unaitaji mda
Shukrani.Mungu atakusaidia mkuu ,kama unavyosema kujenga mipango ,ukiwa na mipango ukajiwekea mikakati kidogokidogo basi mwisho wa siku utajikuta unafikia lengo ,unajuwa wengi wanataka mambo makubwa kwa haraka na haiwezekani ,
wewe nenda mdogomdogo jikusanye kwa tofali ,utafika tu ipo siku maana mungu ni wetu sote sio wao peke yao