Nakumbuka wakati wa Jk awamu ya kwanza kuna boss wangu mmoja aliwahi kunishauri nisikimbilie magali niwekeze kwenye ardhi kweli nikaenda nikanunua bagamoyo kama 1 heka kwa 400k wakati huo nikaweka banda baadae nikanunua tena mitaa ya boko kwa 1.5m wakati huo nalipwa 3k per month ila akwambie mtu lazima ujibane ndio ujenge pale boko nilianza kujenga vyumba 2 kwa mbinde lengo nikae ila mazingira hayakunivutia sana sababu ya uswahili flan flan nikapapangisha pesa ya kodi nikianza kuongeza chumba kimoja kimoja awamu ya pili ya JK nikapata kazi sehemu hivyo salary ikapanda mpk 700k nikamalizia Nyumba boko nikapata sehemu nyingine mbezi juu nikaanza kujenga kidogo kidogo kwa nyumba ya nyuma chumba na sebule pale nilipokuwa nafanyia kazi kuna wadau niliwashauri tununue sehemu ila walinicheka kwamba kwanza mbali na ofisi halafu hiyo pesa natumia kujenga niweke kwenye biashara na biashara ingenilipa kuningenunua nyumba wengi wao walikimbilia kununua magali na kufungua biashara za nguo, salooni na nk ambazo sasa hivi zimekufa na kampuni yenyewe inaendea kufa mie sasa hivi nimeshamalizia nyumba kubwa Kule bagamoyo nimeweka mifugo kama kuku,kitz, ng'ombe wa maziwa,na Kule kazi nilishaacha sasa hivi nipo busy tu na mifugo na kilimo moro na kusoma kujiendeleza kuajiriwa sitaki hata kusikia, watu wengi wanafeli kwenye ujenzi kutokana na kutishwa, kuwa na matarajio makubwa kuliko kipato,starehe za muda mfupi bila kuwa na malengo ya muda mfupi, kusubiria apate pesa nyingi bila kujua zitatoka wapi kwa uzoefu wangu sijawahi kwenda site zaidi ya 3m nilichokuwa nafanya nikipata pesa nawekeza vifaa dukani mpk natimiza lengo na kingine ukipata nyumba 1 ni rahisi kidogo ya kupata ya 2