Yah mkuu
Reagan Carima nia siyo kupingana na ulichoandika hapa.
Ulichofanya ni kitu kizuri sana,tena sana kwamba hutoteseka na ujenzi kwa kipindi kirefu ila kuna ile kuja kuhisi nyumba kama haikutoshi,amekuja mama yako inabidi alale na mwanao mdogo ambaye angali anakojoa kitandani na hapo majukumu yamekubana kweli kweli unajisikia kutaka kuongeza ukubwa wa nyumba au uanze nyengine kubwa zaidi but mfuko unakataa hasa tukirudi main post point #1.
Nilianza ujenzi wa nyumba yangu kubwa nikiwa na ramani mkononi ambayo nilishaonywa kabisa kwamba haita-cost chini ya mill56 wakati huo miaka 10 nyuma ila nilijipa moyo kwamba kama nilipewa uwezo wa kununua kiwanja basi na uwezo wa kumaliza ujenzi nitapewa,hapo katikati nikapata misukosuko ambayo kwenye maisha ya utafutaji haikosekani ila sasa hivi nipo zaidi ya 90% kuimaliza japo makadirio siyo yale ya mwanzo hela inaenda kuzidi ila siyo kitu muhimu sinywei pombe nafanya la maana.so tusiwe waoga mie nilianza ujenzi na 8mill ikaishia yote kwenye msingi na deni la fundi ila leo naishi kwangu kimiujiza kijana mdogo naheshimika mtaani.
“Ukiji-limit kumiliki vitu vidogo,utamiliki vitu vidogo,ukiji-limit utamiliki vitu vikubwa utamiliki vitu vikubwa”
Believe me,Mungu huenda na akili yako inavyowaza hana muda wa kuilazimisha itake vitu ulivyoviogopa wakati alishakuonya usikate tamaa,ajabu ya maisha hakuna mwenye arifa lini atafanikiwa.
NB:kila mtu ana bahati yake,nilichokiandika hapa ukitaka kukichukua jitazame upo ktk step gani ya maisha,mie nilianza hivi nikiwa aged 23 sina wategemezi bado zaidi ya mama mzazi tu hivyo kama una familia tayari na kipato chako ni cha kawaida sana jipime mara mbili mbili.