Ujenzi: Nimefanya uchunguzi kwanini watu wengi wanashindwa au kuchelewa kuwa na kwao

Ujenzi: Nimefanya uchunguzi kwanini watu wengi wanashindwa au kuchelewa kuwa na kwao

Heri moja kenda kuliko kumi nenda rudi, unajenga nyumba ya vyumba2, baada ya kuhamia unakaa miaka3 familia inakuwa kubwa. Mwisho unawaza kujenga nyumba nyingine kubwa.

Mkuu raha ya nyumba ujiachie. Sio unakuwa kwako utadhani upo geto, kajumba kadogooo.
Unajenga jumba kubwa, afu Finishing inakushinda.

Mpaka bati zinafikia pauka, hata lipu hujapiga.

Unajikuta UNAISHI saiti na sio nyumbani Tena.
 
Mpe mbongo bilioni 10 atajenga mijumba akitegemea kurejesha mapesa yake baada ya miaka 10 hadi 20.

Mpe msomali bilioni 10 atafungua maduka makubwa, ata import na kukuza biashara zake kwa eneo husika.

Mpe Muhindi bilioni 10 ataanzisha kiwanda kitakua kikubwa na atapiga pesa kwa muda mrefu.

Ujumbe tusifikirie kujenga sana tuache dhana ya uoga 😂😂😂😂😂
muhindi na msomal niwatu wakuzurura dunian. Ila mzawa kukaa nyumba zakupanga ni ubwege ardhi yote hii unapanga? Hata Mungu anakuona hauna akili. Nilienda kijiji kimoja 5km kutoka wilayani. Vijana wamepata ajira ya kwanza kijiji kina fursa ardhi unapata kipande mpaka laki tatu ila amini usiamini vijana wamepanga wilayani wanalipa kila siku 3000 nauli nakupanga 100,000 je hiyo akili au matope? Umasikin ni vile unawaza ardhi ndio biashara ya kweli asikudanganye mtu. Bihashara ya uchuuzi haiwez kukupa maendeleo ya kweli. Jiulize Bush anakuja miliki ardhi Tz what the secret?
 
Ujenzi wa nyumba kubwa inabid ujipange kweli kweli..lenta tu ujiandae na 1.5M.View attachment 1503172
Mkuu nikupongeze kwa hatua hii uliyofikia,upo hatua 900 mbele ya anaenza leo nikupe moyo kwamba utaimaliza.me yangu ilisimama hivi almost miaka 7,I mean 7 years bila kufanya chochote na mfukoni hela sina kila nayoipata inatosha kwa matumizi ya wakati husika tu ila sikuwahi kukata tamaa,imani yangu ilikuwa ipo siku kama nipo hai nitaimaliza

Namshukuru Mungu,ndoto yangu amenipa uwezo wa kuitekeleza.hii pic ipo Google photos niliipiga mwaka 2017 siku ya jumapili,nikiwa hapa nilikutana na mjumbe wa mtaa akaniambia pagale lako linafuga wezi kama umeshindwa si umuuzie fulani (ni jirani yangu ana hela kidogo za kubadilisha mboga) na alikuwa ameshamnunua jirani yangu wa upande wa kushoto,nilijisikia huzuni sana nakumbuka nilikosa kauli sahihi ya kumjibu nikakaa kimya na hivi lilikuwa limefurika majani nikijiangalia mfukoni hela sina dah,binadamu wanajua sana kukatishana tamaa ila sasa maisha yanaendelea.

Mpaka nafikia hatua ya kuweka bati hizo tofali zilishabadilika rangi zikawa rangi nyeusi tii!kikubwa tusikate tamaa pumzi ikiwepo pambana.
Screenshot_2020-07-10-23-00-21-511_com.miui.gallery.jpg
IMG_20170326_154122.jpg
IMG_20191228_205000.jpg
 
muhindi na msomal niwatu wakuzurura dunian. Ila mzawa kukaa nyumba zakupanga ni ubwege ardhi yote hii unapanga? Hata Mungu anakuona hauna akili. Nilienda kijiji kimoja 5km kutoka wilayani. Vijana wamepata ajira ya kwanza kijiji kina fursa ardhi unapata kipande mpaka laki tatu ila amini usiamini vijana wamepanga wilayani wanalipa kila siku 3000 nauli nakupanga 100,000 je hiyo akili au matope? Umasikin ni vile unawaza ardhi ndio biashara ya kweli asikudanganye mtu. Bihashara ya uchuuzi haiwez kukupa maendeleo ya kweli. Jiulize Bush anakuja miliki ardhi Tz what the secret?
Usimlaumu mkuu,wabongo wengi wanafikiri kufanya biashara ni rahisi sana hawajui kama hadi mtu kumiliki mf:kiwanda panakuwa na mikono ya karibia familia nzima iki-support mpaka mabinamu wa muhusika.Wahindi wengi wenye mali hawawezi wakasimama man to man kusema mali ni zao binafsi kutokana na familia nzima huwekeza nguvu na maarifa yao pamoja.
 
Akili kubwa[emoji109]
Kuna ile dhana umepata kiwanja kizuriii unasema kwa kuwa hichi kiwanja ni kuzuri najenga eneo hili sitaki nije bomoa tena nataka nijenge kitu cha moja kwa moja vyumba vya kutosha mfano vinne, hapo ndipo wengi wanapo anguka, unajenga vyumba vinne matokeo yake humalizi kwa wakati na bila malengo na kuendelea kukuongezea gharama, wakati ungejenga vyumba vitatu ingefaa tu na kumaliza na kuhamia kwa haraka
 
Mpe mbongo bilioni 10 atajenga mijumba akitegemea kurejesha mapesa yake baada ya miaka 10 hadi 20.

Mpe msomali bilioni 10 atafungua maduka makubwa, ata import na kukuza biashara zake kwa eneo husika.

Mpe Muhindi bilioni 10 ataanzisha kiwanda kitakua kikubwa na atapiga pesa kwa muda mrefu.

Ujumbe tusifikirie kujenga sana tuache dhana ya uoga [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ndugu sisi hapa TZ ni nyumbani hao wasomali, wahindi, hapa sio kwao na wao huko kwao walianza na kujenga kwanza mahali pa kulala
 
Back
Top Bottom