kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kama barabara hizi hazitatumika kusafirisha mazao, mifugo na bidhaa kwenda na kutoka zinakopita zitatumiwa na wananchi kusafirisha vyuma vya madaraja na alama za barabarani vya barabara hizo vilivyokatwa na kung'olewa na wananchi kwenda kuuza na kujipatia fedha ya kujikimu.
Tunapomimina hela za kujenga barabara tumimine fedha wakati huohuo fedha za kuboresha kilimo, ufugaji na bidhaa ningine.
Kugawa ardhi ya mashamba makubwa yaliyokuwa ya mifugo, katani, ngano, mpira, nk kwa wakulima wadogo wanaolima kwa jembe la mkono na mbegu za kizamani ni kuendeleza umaskini wao na taifa.
Mashamba makubwa (plantations and ranches) yataajiri vijana wengi zaidi kuliko kugawa ardhi kwa mtu mmojammoja. Mashamba madogo yawepo lakini mashamba makubwa ya wawekezaji wakubwa yawepo pia.