Ujenzi wa Barabara unaoendelea maeneo mengi ya Dar kwa wakati mmoja, Je, ilifanyika tathmini ya awali kubaini athari?

Ujenzi wa Barabara unaoendelea maeneo mengi ya Dar kwa wakati mmoja, Je, ilifanyika tathmini ya awali kubaini athari?

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Kwa kipindi cha hivi karibuni kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam kumekuwepo na kilio cha foleni hasa kutokana na ujenzi unaondelea katika meneo mengi hususani njia za mwendokasi pamoja na utanuzi wa barabara za kawaida.

Natumaini ni matamanio ya kila mmoja wetu humu kuona miundombinu ya Jiji inaboreshwa ili kuwezesha urafiki wa kupitika kwa uharaka jambo ambalo linaweza kuwa chachu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Hata hivyo nimekuwa nikijiuliza kutokana na uzoefu wa foleni kwenye jiji la Dar es salaam, imekuwaje mamlaka zimeamua kutekeleza miradi mingi ya ujenzi wa barabara kwa wakati mmoja! Bado sina majawabu ya swali hilo ikizingatiwa unyeti au umuhimu wa jiji.
Screenshot 2025-05-27 170826.jpg

photo_2025-05-27_16-57-47.jpg
Najiuliza, hivi ilifanyika tathimini ya awali kabla ya uamuzi wa kuamua kuanza kutekeleza miundombinu hiyo yote kwenye jiji kuu ambalo lina harakati za kiuchumi kila kona, hiyo tathimini ilifanyika kubaini athari au tija zilizopo kabla ya kufanya uamuzi, suala la kifedha nalo vipi, walijiandaa?

Ni msukumo gani uliotukimbiza tufanye hivyo, kwa sasa barabara ya Tegeta-Mwenge imechimbuliwa, Mwenge- Morocco, Morocco-Posta, Posta Kisutu- Mnazi Mmoja, pote ni ujenzi, Ubungo-Mwenge, Kimara-Ubungo, Buguru - Kkoo hali ni hiyo hiyo, Gongoramboto nako bado hakujakamilika.

Bora ujenzi huo ungekuwa unafanyika na kukamilika kwa wakati uenda hi lingeleta matumaini, lakini kwa dalili zilizopo maeneo mengi ujenzi unaenda ‘slow’, mfano kipande cha Buguruni -Kkoo kupita Karume, Mwenge-Tegeta, barabara inachimbuliwa yote lakini baada ya hapo mambo yanaanza kwenda taratibu na kusababisha foleni kwa kipindi kirefu.
Screenshot 2025-05-27 170642.jpg

photo_2025-05-23_09-44-03.jpg

864438e881953ef99f6850a5f8d8edd2.jpeg
Kwa sasa hali ya foleni kwenye njia mbalimbali za Mkoa wa Dar es salaam imeongezeka zaidi, mfano kwa sasa kutoka Kariakoo kuitafuta Tegeta mida ya saa 12 jioni au saa moja asubuhi unatumia takribani masaa matatu, Ubungo - Kumara hali ni hiyo hiyo.

Naamini endapo tathimini ingefanyika ipasavyo zingebainika athari za miundombinu hiyo kutekelezwa kwa wakati mmoja au tungekuwa tunaona uwajibikaji zaidi uanaolenga kuweka msisitizo zaidi kwa miradi ya ujenzi kutekelezwa na kukamilika kwa wakati tofauti na ilivyo sasa.

Kwa kuwa tayari miradi imeanza nitoe wito kwa mamlaka husika hususani Wizara ya Ujenzi kuongeza kasi ya ufuatiliaji na usimamizi wa miradi hiyo, shughuli zifanyike usiku na mchana kama ambavyo tumekuwa tukiambiwa kwenye kutia saini na endapo kama kuna changamoto katika malipo wakandarasi jambo hilo lifanyiwe kazi kwa uharaka ili ujenzi usiendelee kuchukua muda mrefu

Wenye dhamana ya usimamizi wazingatie kwa kutambua kuwa Jiji la Dar es salaam ni sehemu muhimu katika kukuza uchumi wa Taifa hivyo uwepo wa foleni kwa kipindi kirefu kuna athari za moja kwa moja kwa Nchi pamoja na Mtu mmoja mmoja.
 
Huyu mama mpaka anatoka madarakani hii miradi hatoimaliza

Ova
 
Back
Top Bottom