Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Bagamoyo (Makurunge) - Saadani - Pangani - Tanga (km 256) Sehemu ya kwanza Pangani-Tanga (km 50) kwa kiwango cha lami umefikia 75% Sehemu hii ya Tanga - Pangani inagharimiwa kwa fedha za ndani kwa asilimia 100.
Awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huo inaunganishwa na ujenzi wa awamu ya pili wa Daraja la Mto Pangani lenye urefu wa mita 525 ikijumuisha barabara za maingilio ya Daraja zenye urefu wa kilometa 14.3 na barabara unganishi za Ushongo (5.9km) na Pangani Mjini (5.6km),
Ujenzi wa awamu ya tatu ni wa barabara ya Tungamaa - Mkwaja - Mkalamo - Kwamsisi - Mkange (95.2 km) ikijumuisha barabara unganishi ya Kipumbwi (3.7km). Sehemu iliyobaki ya kutoka Mkange hadi Makurunge (Bagamoyo) km 73.25 bado mradi haujatangazwa. Awamu ya pili na ya tatu inafadhiliwa kwa fedha za Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Katika Taarifa yake kwa Umma, tarehe 4 Juni 2023, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tanga Eng: Eliazary T. Rweikiza amesema barabara hiyo ni sehemu ya barabara za Afrika Mashariki ambayo ipo kwenye ukanda wa Pwani ulionzia Miji ya Malindi - Mombasa hadi Lungalunga/Horohoro - Tanga - Pangani - Bagamoyo (Makurunge) wenye jumla ya kilometa 454. Sehemu ya Horohoro hadi Tanga Mjini ilishakamilika.
Amesema ujenzi wa barabara hiyo kipande cha Pangani -Tanga km 50 unaotekelezwa na Mkandarasi kutoka Kampuni ya M/s China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) ya Nchini China kwa gharama ya shilingi bilioni 68.039 ulipaswa kukamilika tarehe 24 Mei 2023, lakini haukukamilika kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa kazi hasa ya uondoaji udongo usiofaa na kuweka udongo unaofaa kwa ujenzi, kuhamisha miundombinu ya Umeme na Maji, uhamishaji wa makaburi pamoja na hali ya hewa isiyotabirika.
Pia katika mradi huu kumekuwa na mvua kubwa za mara kwa mara katika eneo la mradi, mabadiliko ya hali ya hewa hasa uwepo wa mvua nyingi umekuwa ukizuia shughuli za ujenzi kuendelea kama ilivyopangwa, Mkandarasi ameomba nyongeza ya muda ili aweze kukamilisha kazi ambapo kwa sasa Mkandarasi amepewa nyongeza ya muda wa matarajio (Interim Extension of Time )ya miezi mitatu (3) hadi tarehe 24 Agosti 2023.
Eng: Rwekiza ameongeza kuwa ujenzi wa tuta la barabara umekamilika kwa 75%, Magari yameruhusiwa kwenye baadhi ya maeneo kupita juu ya tuta la barabara mpya inayojengwa kwa kuwa maeneo hayo awali yalikuwa na madaraja madogo ambapo huwa yanazidiwa na maji na kufanya yasipitike, Magari yakisha pita sehemu za madaraja Mapya makubwa hurejea kwenye njia ya mchepuko, na kwamba tahadhari zote zimechukuliwa kuhakikisha hakuna uharibifu kwenye barabara mpya na endapo uharibifu utatokea basi Mkandarasi atarekebisha kwa gharama zake mwenyewe.
Aidha, barabara hiyo ni kiunganishi cha nchi za Kenya na Tanzania upande wa Pwani ya Afrika Mashariki na ikikamilika itachochea ukuaji wa uchumi ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa usafiri, urahisishaji wa kufanya biashara na kuwezesha wananchi kuchangamana kwa urahisi, kuwezesha kufikika kwa urahisi kwenye vituo vya utalii na kuwa kiungo kizuri cha bandari za Dar es salaam, Tanga na Mombasa na kuchochea uchumi wa Bluu.