Ujenzi wa Barabara ya Kimara - Bonyokwa - Kinyerezi (KM 7) Waanza Rasmi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
WhatsApp Image 2024-12-31 at 10.19.16_36dd0a61.jpg

WhatsApp Image 2024-12-31 at 10.19.17_aa481bd8.jpg
Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Abdallah Ulega, amefanya ziara ya kikazi kutembelea barabara ya Kimara - Bonyokwa - Kinyerezi yenye urefu wa kilometa 7, mkoani Dar es Salaam, na kusisitiza umuhimu wa kuharakisha ujenzi wa barabara hiyo ya kimkakati.

Katika ziara hiyo, Waziri Ulega ameagiza mkandarasi anayejenga barabara hiyo, kampuni ya kizawa ya Nyanza Road Works, kuhakikisha kuwa kazi zinafanyika usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa haraka na kwa ubora unaotakiwa.

"Kazi imeanza rasmi na wananchi wataanza kushuhudia maendeleo ya ujenzi wa barabara hii muhimu. Mkandarasi ahakikishe anakuwa na wafanyakazi wa kutosha na kwa ajira zisizo za ujuzi zitolewe kwa wananchi wa maeneo ya jirani na mradi ikiwemo Bonyokwa kama sehemu ya kurudisha kwa jamii," amesema Waziri Ulega.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli, ameunga mkono agizo hilo, akisisitiza kuwa ajira za muda mrefu wakati wa ujenzi ni fursa kwa wananchi wa Bonyokwa, Kinyerezi, Kimara na maeneo jirani.

Barabara hiyo muhimu inatarajiwa kuwa kiunganishi kikubwa kati ya majimbo ya Ubungo na Segerea, hatua inayotarajiwa kuboresha huduma za usafiri na kuinua uchumi wa eneo hilo.
WhatsApp Image 2024-12-31 at 10.19.18_f9811eba.jpg

WhatsApp Image 2024-12-31 at 10.19.18_1f05991e.jpg
Waziri Ulega ameahidi kuwa serikali itasimamia mradi huo kwa weledi huku akiwahakikishia wakandarasi kuwa malipo yao ni kipaumbele cha serikali.

"Nyanza Road Works mmeonesha rekodi nzuri, tunawaamini, na tunategemea kazi bora zaidi katika mradi huu," aliongeza.

Wananchi wanaoishi maeneo ambayo barabara hiyo inapita Kimara, Bonyokwa, Kinyerezi na maeneo jirani sasa wana matumaini makubwa ya kupunguza changamoto za miundombinu, usafiri na wanatarajia kunufaika kiuchumi kupitia mradi huu wa ujenzi.

Ujenzi wa barabara hiyo utajumuisha daraja lenye mita 25 na madaraja madogo saba ya kalvati na mkandarasi akitakiwa kufunga taa za barabarani.
 
Hii barabara tumepita Juzi hakuna Kifaa chochote kilichokuwepo pale, kuanzia Kimara Mwisho hadi Bonyokwa hakuna kitu chochote,
Sasa huo ujenzi ambao umeanza mara moja umeanzi lini?

Miezi kama kumi hivi waliweka alama na watu washapisha ujenzi mda mrefu kasoro TANESCO na NGUZO ZAO bado hawajahamisha nguzo zao kuzisimika pembeni nje ya Mradi.

NB;- Hii barabara ikijengwa, Kiukweli ni njia nzuri sana ya Shortcut kutoka KINYEREZI, SEGEREA, BANANA kwenda KIMARA
 
Tabata hii ndio solution, sio mwendo kasi.

A step in the right direction
 
Wananchi wanaoishi maeneo ambayo barabara hiyo inapita Kimara, Bonyokwa, Kinyerezi na maeneo jirani sasa wana matumaini makubwa ya kupunguza changamoto za miundombinu, usafiri na wanatarajia kunufaika kiuchumi kupitia mradi huu wa ujenzi.
Watajenga vipi ilhali kuna zuio la Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi (Dar es Salaam) kupitia kesi ya Ardhi Na. 24793 ya 2024 kuwa wasubiri mpaka itakaposikilizwa kesi ya msingi kwa wahanga walioelekezwa kubomoa nyumba zao bila kupewa fidia?? Au ndio Mambo ya kudharau amri za mahakama?
 
Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Abdallah Ulega, amefanya ziara ya kikazi kutembelea barabara ya Kimara - Bonyokwa - Kinyerezi yenye urefu wa kilometa 7, mkoani Dar es Salaam, na kusisitiza umuhimu wa kuharakisha ujenzi wa barabara hiyo ya kimkakati.

Katika ziara hiyo, Waziri Ulega ameagiza mkandarasi anayejenga barabara hiyo, kampuni ya kizawa ya Nyanza Road Works, kuhakikisha kuwa kazi zinafanyika usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa haraka na kwa ubora unaotakiwa.

"Kazi imeanza rasmi na wananchi wataanza kushuhudia maendeleo ya ujenzi wa barabara hii muhimu. Mkandarasi ahakikishe anakuwa na wafanyakazi wa kutosha na kwa ajira zisizo za ujuzi zitolewe kwa wananchi wa maeneo ya jirani na mradi ikiwemo Bonyokwa kama sehemu ya kurudisha kwa jamii," amesema Waziri Ulega.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli, ameunga mkono agizo hilo, akisisitiza kuwa ajira za muda mrefu wakati wa ujenzi ni fursa kwa wananchi wa Bonyokwa, Kinyerezi, Kimara na maeneo jirani.

Barabara hiyo muhimu inatarajiwa kuwa kiunganishi kikubwa kati ya majimbo ya Ubungo na Segerea, hatua inayotarajiwa kuboresha huduma za usafiri na kuinua uchumi wa eneo hilo.
Waziri Ulega ameahidi kuwa serikali itasimamia mradi huo kwa weledi huku akiwahakikishia wakandarasi kuwa malipo yao ni kipaumbele cha serikali.

"Nyanza Road Works mmeonesha rekodi nzuri, tunawaamini, na tunategemea kazi bora zaidi katika mradi huu," aliongeza.

Wananchi wanaoishi maeneo ambayo barabara hiyo inapita Kimara, Bonyokwa, Kinyerezi na maeneo jirani sasa wana matumaini makubwa ya kupunguza changamoto za miundombinu, usafiri na wanatarajia kunufaika kiuchumi kupitia mradi huu wa ujenzi.

Ujenzi wa barabara hiyo utajumuisha daraja lenye mita 25 na madaraja madogo saba ya kalvati na mkandarasi akitakiwa kufunga taa za barabarani.
Wanataka wapige Ile pesa ya DMDP
 
Back
Top Bottom