Mpepetaji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 346
- 213
Ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Jiji la Dodoma (ring road) umefikia zaidi ya asilimia 85 ya utekelezaji wake.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesomewa taarifa hiyo alipotembelea ujenzi huo ili kuona maendeleo yake.
Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 112.3, ni miongoni mwa barabara za kimkakati mkoani Dodoma, na wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi huo Waziri Ulega aliwaambia waandishi wa habari kuwa barabara hiyo itaing’arisha Dodoma hasa nyakati za usiku kwani itafungwa taa.
“Nimekagua na nimeridhishwa na hatua zilizofikiwa katika awamu zote mbili na malengo ya Serikali ya Rais DKt. Samia Suluhu Hassan ni kuwa mradi huu ukamilike kwa wakati na nimeelekeza wataalam kutoka TANROADS hadi kufikia mwezi Juni ujenzi uwe umefikia asilimia 90”, amesisitiza Ulega
Amesema ujenzi wa barabara hiyo ni sehemu ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara katika Jiji la Dodoma na Tanzania kwa ujumla, na kwamb a Serikali inatarajia kujenga barabara ya njia nne na sita kuanzia Chamwino Ikulu hadi katikati ya Jiji hilo ambapo kwa sasa ipo katika hatua za mwisho za manunuzi za kumpata mkandarasi wa kutekeleza mradi huo.
Katika eneo la Ihumwa, Serikali ina mpango wa kujenga barabara ya kisasa ya njia za kupishana (interchange).
Pia soma: Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze