Waziri wa Ujenzi Profesa Mbarawa ameyasema hayo akizungumza na wadau wa sekta ya usafirishaji jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi la leo ni Kwambaza barbara hiyo itajengwa kwa utaratibu wa BOT yaani JENGA, ENDESHA, RUDISHA.
Ujenzi huo utaanza APRILI 2023.
Barabara hiyo ya Kilomita 215 itakuwa ya kulipia.
MY TAKE
Huu ni mwarobaini wa kuchelewesha uchumi. Ni hatua ya kupongezwa.
Hiyo barabara inapitisha magari yanayoenda kanda ya ziwa, nyanda za juu kusini na pia kanda ya kaskazini kwa kupitia Chalinze. Kibaha-Mlandizi ni 30km tu highway Ila unaweza tumia 2hrs tu kirahisi.