Umeme ni nishati muhimu sanaa katika maendeleo ya taifa la Tanzania kwani uzalishaji wa bidhaa nyingi viwandani, migodini, mashambani, wajasiriamali na nyumbani hutegemea nishati ya umeme ambayo kwa kiasi kikubwa unaotokana na maji ambao ndio unaosemekana kua nishati yenye gharama nafuu zaidi katika kupatikana na unafuu katika gharama kwani wananchi wengi hushindwa kumudu gharama za nishati mbadala kama jua, makaa ya mawe, dizeli , petroli na gasi kwani gharama zake zipo juu sanaa hivyo kupelekea uzalishaji kuwa juu zaidi na kukosa tija katika shughuli zao ivyo tegemea linabaki kwenye umeme wa TANESCO unao tegemea zaidi chanzo cha maji ingawa mara nyingi umegubikwa na changamoto nyingi kwani wasambazaji wa umeme wamekua wakishindwa kutoa huduma ya umeme kwa uhakika mkubwa kwa sababu ya mabadiliko ya tabia ya nchi aitha kwa maji kua kidogo katika vyanzo vyao au mvua kua nyingi na kujaza matope na kuzuia ufanisi wa mitambo hivyo kupelekea upungufu au ukosekanaji wa huduma ya umeme nchini na kupelekea kero kubwa kijamii na kiuchumi kipindi panapo kosekana umeme wa uhakika.
Ingawa mamlaka husika TANESCO hutumia vyanzo vingine vya nishati kama umeme wa jua, upepo, gesi asilia na hata kuendeleza tafiti mpya za vyanzo vya nishati kama ufuaji wa umeme kwa joto ardhi lakini bado haijakidhi upungufu wa umeme, gharama na uhakika wa nishati hio muhimu kwa uchumi wa taifa kwani jitihada izo bado hazitoi mwanga wa matatizo hayo kama bado tutategemea maji kwa sababu zifuatazo;
Ujenzi wa bwawa la nyerere bado sio suluhisho la umeme Tanzania.
Pamoja na mradi huu mkubwa wa umeme kuigharimu serikali trilioni nyingi za pesa bado sioni kama ni mwarobaini wa watatizo la umeme nchini kwani mradi huu pamoja na faida zinazoelezwa zitaletwa na mradi huu mkubwa wa umeme unaotegemea maji ukikamilika bado nona changamoto nyingi zataendelea kuwepo kama zifuatavyo;
1. Mabadiliko ya tabia za nchi.
Kumekuwepo na mabadiliko makubwa ya tabia ya nchi kwa miaka ya hivi karibuni duniani kote na hata hapa kwetu tanzania kwani viwango vya juu vya joto vimerekodiwa nchini na viwango vya chini vya mvua na kupelekea kilio kwa sehemu kubwa nchini Tanzania kwa wakulima, wafugaji na mbaaya zaidi hata kwa wazalishaji na wasambazaji wa umeme nchini TANESCO wameathiriwa na mabadiliko haya kupelekea uzalishaji wao wa umeme kushuka na kushindwa kukidhi mahitaji ya wateja wao kwani vyanzo wanavyo tegemea vimekua na kiwango kidogo cha maji tokana na ukame kwani sehemu nyingi zimekosa mvua ya kutosha na hata hakuna anayejua uhakika wa mvua wa miaka ijayo sasa ni hatari kuendelea kuamini maji kama chanzo muhimu cha umeme.
Mradi huu mkubwa wa bwawa na nyerere pamoja na kuelezwa kama ni sehemu moja wapo cha uharibifu wa mazingira katika utekelezakaji wake bado unategemea mvua (maji) kujiendesha jambo ambalo bado ni hofu na mashaka makubwa maji ya kuweza kukithi mitambo hiyo yatatoka kwenye chanzo kipi kipya kwani hata sasa maji yatakayotegemewa yanagemea mvua jambo ambalo sio uhakika kwani kwa mifano dhahiri ya sehemu nyingine zinazotegemea maji zimeshindwa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kuacha swali maji ya kutosha na uhakika katika mradi huu yatatoka wapi kwani hata mvua pia zikizidi hua ni tatizo iwapo matope yatajaa kwenye bwawa.
2. Gharama za maradi huu ni kubwa hivyo hazionyeshi zitapunguza gharama kwa mwananchi za umeme
Mradi huu umegharimu pesa nyingi sana katika kuufanya na bado patahitajika gharama nyingine za kuendeleza mradi huu kama kuajiri matendaji wengi pamoja na matengenezo ya mitambo kila wakati jambo linalo fifisha unafuu kwa watumiaji wa umeme kwani gharama za uzalishaji lazima ziathiri mauzo kwani shirika linajiendesha kibiashara hivyo bei inaweza kua changamoto ingawa itaongeza upatikanaji wa nishati ingawa bado itategemea bahati ya hali ya hewa kua nzuri jambo ambalo ni hatari taifa kutegemea bahati katika miradi ya gharama kubwa kama hii.
3. Shirika kujiendesha kibiashara ingawa halizalishi faida
Shirika la umeme Tanzania limekua likijiendesha kibiashara kwa miaka mingi lakini halizalishi faida pamoja na kukosa ushindani wa shirika jingine na kua na wateja wengi wapya na wa zamani lakini limekua tegemezi na serikali kuendelea kutoa fedha kulinusuru shirika hili. Hapa inatia hofu namna fedha hizi zilizotumika kwenye mradi huu kama zitaweza kurudishwa moja kwa moja ingawa inaweza ikawa sio kipombele cha serikali kulipwa moja kwa moja gharama izo kwani uhakika wa umeme unaongeza wigo wa kodi kupitia shughuli za uzalishaji na hata mradi mkubwa wa treni za umeme unategemea pia umeme wa uhakika na hata uhakika wa umeme ni sehemu ya usalama wa nchi. Ila swali linabaki usalama wa mitambo utadumu kwa muda gani kama shirika halitakua na faida itakayotumika kutengeneza mitambo kununua mipya au kuajiri wataalamu sahihi wa mitambo jambo ambalo naamini serikali ipo makini lakini lazima ufuatiliji wa karibu.
Suluhisho la kudumu la tatizo la umeme Tanzania
Serikali imefanya jitihada nyingi za wazi kutatua tatizo la umeme Tanzania ingawa bado imeonekana ni mfupa mgumu mno ambao umepelekea watu binafsi kubuni mbinu mbalimbali kujipatia nishati mbadala kama umeme wa jua, gesi asilia, makaa ya mawe pamoja na mafuta kama dizeli na petroli ambazo zinagharimu fedha kubwa na kupelekea mzigo kwa wananchi kwani gharama kubwa za nishati hupelekea kupanda kwa bei za huduma na bidhaa na kupandisha gharama za maisha ingawa kipo kiwanda kimoja kimetumia njia ambayo naamini serikali na wadau wengine wanapaswa kuiga na kuboresha na kuondokana kabisa na tatizo la umeme Tanzania.
Matumizi ya mabaki ya miwa (bagasse) kuzalisha umeme.
Kiwanda cha kazalisha sukari mkoani Kilimanjaro cha TPC kimeweza kutumia njia salama kwa mazingira, rahisi na ya kipekee ya kuzalisha umeme kwa kutumia mabaki ya miwa baada ya kuzalisha sukari. Umeme huu umekua wa uhakika na toshelevu kwa kiwanda na ziada ambayo huuzwa nchi jirani jambo ambalo sina uhakika bado kwanini hawakuuza nchini na tuna uhaba wa umeme. Umeme wote kiwandani wanazalisha wenyewe kwa njia rahisi na ya bei nafuu na kuweza kusambaza kwa makazi ya wafanyakazi wote na kuuza umeme wa ziada.
Njia hii ya uzalishaji umeme nimeona ni salama na rahisi zaidi kuliko ambazo serikali na shirika zimekua zikitumia ambazo zimeshindwa kutatua tatizo la umeme nchini hivyo ni sahihi wakaiga na kujifunza mfumo huu au kuboresha zaidi na kuutumia kama njia kuu ya uzalishaji wa umeme nchini kwa kufanya yafuatayo:
1. Kuwezesha viwanda vyote vya sukari kuzalisha umeme binafsi na wa kibiashara.
Tanzania ina viwanda vingi vinavyozalisha sukari nchini hivyo viwanda hivi vikatumika kama sehemu muhimu ya kuzalisha umeme wa kiwanda husika (kupunguza utegemezi wa umeme toka TANESCO) na pia kuzalisha umeme kibiashara na kusambaza maeneo jirani na viwanda hivyo. Serikali iwezeshe utaalamu na mitaji kwa viwanda husika na viwanda ambavyo havitakua tayari kuanza biashara ya umeme watoe fursa kwa kampuni nyingine kuingia ubia na kushirikiana kwenye biashara hii au kuwauzia mabaki ya miwa.
2. Serikali kuanzisha viwanda vyake vya sukari kwaajili ya uzalishaji wa sukari na umeme.
Pamoja na uhaba wa umeme nchini pia kuna uhaba wa sukari. Serikali inaweza kuanzisha viwanda vyake kutibu matatizo kwa pamoja kwani sukari huingizwa nchini toka nje na hata bei ya sukari na umeme sio rafiki kwa wananchi. Huu ndo Muda wa serikali kuanzisha viwanda vingi vya sukari na kujikita kikamilifu katika uzalishaji wa sukari na umeme kwani kupitia njia hii tutapata umeme wa uhakika kwa bei nafuu pasipo kuharibu mazingira jambo muhimu ni kufanya tafiti ya kutosha.
3. Kuwezesha wazawa na kukaribisha wawekezaji katika uzalishaji wa sukari na umeme.
Yapo makumpuni mengi kutoka nje naamini yatajitokeza kuwekeza kama serikali itaweka wazi mpango huu hasa uhakika wa soko la umeme watakao zalisha kwani wanaweza weka utaratibu mzuri na bei ambayo TANESCO watanunua toka kwa wazalishaji hao wa umeme kwani uhakika wa soko la sukari upo na hata ushindani ukiongezwa sio mbaya katika soko la sukari hivyo umeme wa uhakika ukapatikana na kuachana na umeme wa kutegemea mvua kwani uzuri wa kilimo cha miwa hakihitaji maji mengi kama kuzalishaji umeme kwa kutumia maji pia ni rahisi faida ya miwa kuendesha uzalishaji wa umeme.
Hitimisho
Akili na ubunifu ndo pekee suluhisho la tatizo la umeme nchini na kuachana na kutegemea maji zaidi kwani Kiwanda cha sukari cha TPC Moshi kimeonyesha mwangaza wa kutosha kwa namna ya kisasa nafuu na rafiki kwa mazingira ya uzalishaji wa umeme kwa kutumia mabaki ya miwa jambo ambalo serikali inaweza kutumia na kupata umeme wenye gharama nafuu na uhakika zaidi na kuachana na kutegemea maji ambayo kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabia ya nchi yameathiri mfumo huu na bado hatujui kesho yetu katika ukame itakua vipi.

Upvote
5