Katika pitapita yangu mitandaoni,nimekutana na habari iliyoibuliwa na Bwana mmoja huko twitter kuhusu gharama ambazo serikali imetumia katika kugharamia ujenzi wa huo mradi ambapo muhusika ametoa nyaraka inayoonekana ni nyaraka iliyoandaliwa kwa ajili ya kujadiliwa Bungeni ikionyesha fedha zilizotengwa na serikali kwa ajili ya kugharamia huo miradi.
Kama nyaraka hiyo ni ya kweli(sio feki), basi serikali itakuwa ilitenga jumla ya shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa Ubungo interchange(nyaraka inaaonyesha zimetengwa bilioni 10).
Lakini mradi huu tunasoma kuwa utajengwa kwa mkopo wa Benki ya dunia ambapo utagharimu bilioni 200.7 bila VAT(kwa mujibu wa gazeti la Habari leo mtandaoni la tarehe 04/04/2019).Nitaweka link hapo chini.
Mkanganyiko huu ndio umenifanya kutafuta habari zaidi kuhusu gharama ambazo serikali imechangia na ndio nikakutana na hilo gazeti la HabariLeo ambapo limeandika kuwa serikali ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 1.2 kulipa fidia wananchi na kwamba mradi huo unagharamiwa kwa mkopo kutoka benki ya Dunia.
Cha kujiuliza hapa ni hiki:kama serikali ilitoa bilioni 1.2 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi waliotakiwa kupisha huo mradi,hiyo bilioni 10 inayoonekana katika hiyo document ya Bunge inayoonyesha zilitengwa bilioni 10 kwa ajili ya mradi huo zilitumika kufanya kazi gani?
Kama hiyo document ni feki,kwanini serikali au Bunge wasikanushe?
Zitto wewe kama mbunge na member wa JF,tusaidie kuhusu hiyo nyaraka na ukiweza tupe ufafanuzi wa hiyo bilioni 10 kama ilipitishwa na Bunge kama ilivyo au kama kulikuwa na makosa ya wakati waanaandaa hiyo document na baadae wakarekebisha.
Ni masikitiko yangu makubwa kuona interchange nzuri kama hii kuwa na traffic lights ambazo zitaleta usumbufu kwenye interchange. Kwa mtazamo wangu magari kutoka na kuelekea pande zote nne yalitakiwa yapite moja kwa moja bila kusimama ili kuyapisha magari mengine.
Ili kukamilisha hilo level nyingine ya nne ilitakiwa ijengwe. Levels tatu peke yake hazita leta ile mantink iliyotakiwa ya magari au madereva ku enjoy ile flavour ya interchange. Kuweka mataa kwenye interchange kunapoteza ile ladha ya magari kutereza kwenye lami kana kwamba mtu yuko kwenye ndenge vile!
Sababu ya pili ambayo ingeleta umuhimu wa kujenga level ya nne ni usalama. Kuwa na traffic lights kwenye interchange kama hii ni sawa sawa na kuhatarisha maisha ya madereva na abira wao. Sehemu kama hizi masaa ya usiku ni rahisi sana kwa madereva kujisahau kuwa wako kwenye junction na hivyo kusababisha ajari zisizo na msingi, kqani ni asili ya binadam, tutake tusitake tuna tabia ya kurudi nyumbani usiku tukiwa tumepewa kidogo.
Kwa wale ambao tumeishi kwa wenzetu ambako vitu kama hivi ni kawaida kwao watakubaliana na mimi kuwa maeneo kama haya precautions kubwa sana zimechukuliwa kuepukana na uwekaji wa traffic lights.
Sababu ya tatu na pia ni muhimu kwa mipango miji ni kuepuka kusababisha foleni tena baada ya mda sio mrefu, kwani kila mmoja wetu anajua kuwa maendeleo ya miji husababisha watu wengi hasa vijana wanao maliza masomo yao mikoani na vijijini kwenda kutafuta riziki zao za maisha mijini.
Structures kama hizi zinakuwa pia ni vivutio vikubwa kwao kama sisi wengi wetu tunavyo papatika na maisha ya kwenda kwa wezentu ng'ambo. Kwa hali hiyo sio ajabu kuona kuwa mambo kama haya yanasababisha tena msongamano wa watu wengi mijini na hivyo kusababisha traffic jums.
Kwenye hiyo pic nimeonyesha flow ya magari kwenye hiyo interchange kama ifuatavyo;
1. Magari yatokayo Tazara/Mandera kwenda City Center/Kariako na yale yanayo piga U-turn kurudi tena Tazara/Mandera (curves ya njano na kijani) yalitakiwa yawe kwenye level moja na magari yatokayo Mwenge kwenda Kimara na yale yanayo piga U-turn kurudi Mwenge (curves ya blau na nyekundu).
2. Magari ya kutoka City Center/Kariako kwenda Mwenge na yale ya kutoka Kimara kwenda Tazara/Mandera nayo yalitakiwa yawe kwenye level yake nyingine ya nne ambayo haipo na sidhani kama itakuwepo.
Kitu kingine ambacho kwa fantasy yangu naona kinakosekana ni underground pathways kwa waenda kwa miguu au baiskeli ambao wanataka kuvuka hizo barabara. Mara nyingi naushangaa sana mfumo wetu wa ujenzi wa barabara na hata ma-flyovers, mtembea kwa miguu na mwendesha baiskeli huwa hawawi considered kabisaa! Sielewi kwa nini. Sijui ni kwa sababu ya usokwe wetu? Yaani tunakosa sana kuwa na funtasy ya kufikiria hicho kitu. Ni masikitiko yangu makubwa sana kwa wapanga miji.
Kwa kuongezea tu kwa fantasy yangu, katikati ya hiyo interchange juu kabisa ingewekwa nembo kubwa ya ngao yetu ya Uhuru na Umoja ambayo inazungunga taratibu na usiku kutoa mwanga
Google-Ergebnis für https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/c/c2/Coat_of_arms_of_Tanzania.svg/1200px-Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png
na chini ya hiyo nembo saa kubwa ya pembe nne ya neon ambayo usiku inatoa mwanga mzuri ili watu wanao toka mikoani wakikaribia Ubungo wanaiona hiyo nembo na saa kutoka mbali kama ishara kuwa sasa wameingia jijini.
Pesa ngapi zimetumika hiyo haijalishi maadam tuna kitu cha kuvutia ambacho kitadumu miaka mingi. Kweli wewe umesha zihesabu hela zako ulizo zitumia mpaka sasa kwa malaya wako? Acheni unoko wa kifalah wa aina hiyo. Maisha ni fantasy na ubunifu wa kutengeneza vitu ambavyo vinaacha legacy.
Maendeleo hayapimwi kwa kujua unapesa ngapi mfukoni na umewanunulia malaya wako chips mayai ngapi? Maendeleo ni vitu pia vinavyo vutia.
Wajerumani kwenye miji yao wana vivutio vingi tofauti, Berlin kwa mfano wana Brandenburger Tor na Pris Eiffell Tower.
Google-Ergebnis für https://s3-eu-west-1.amazonaws.com/de-asitcp-ir-bz-data-prod/data/uploads/2016/08/dpa-picture-alliance-349486_1470418680-768x432.jpg,
Google-Ergebnis für https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/8/85/Tour_Eiffel_Wikimedia_Commons_%28cropped%29.jpg
Sent using
Jamii Forums mobile app