MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
IKUNGI-SINGIDA
Na Gregory Jumbe Mahanju,
Wakati Mama yetu anaendelea kujipambunua kutafuta pesa kwa wahisani ili kutekeleza ilani ya CCM, huko Wilaya ya Ikungi mkoani Singida katika kata za Ntuntu na Irisya tangu pesa zitolewe miradi ya ujenzi wa vituo vya afya katika kata hizo haijakamilika na haijulikani ni lini itakamilika wakati vituo vingi ambavyo vilipokea mgao wa pesa hizo sawa kwa pamoja nchini vimeshakamilika na vimeanza kutoa huduma.
Tatizo kubwa juu ya hofu iliyopo kua hizi pesa kiasi cha shilingi milion 500 ambazo zilitolewa na Mhe Rais almaarufu kama pesa za UVIKO-19 zimetafunwa au kupigwa kwa lugha ya mtaani ni kwamba hakuna ripoti wala taarifa yeyote ya wazi inayotolewa juu ya ujenzi wa vituo hivi, hofu inatajwa kua ni kuanzia Ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Ikungi pamoja na ngazi ya kata na vijiji au kamati ambazo zinasimamia miradi hiyo. Wananchi wanahoji kama vituo vingine ambavyo vilipokea mgao sawa ni hivi vya kwao na muda ni ule ule, ni kwanini wengine wakamilishe lakini Vituo vya Ntuntu na Irisya bado? Matumizi ya milioni 500 za Mama Samia ripoti taarifa zake ziko wapi?
Wakiulizwa viongozi wa Wilaya hawana majibu, wakiulizwa viongozi wa Tarafa,kata na Vijiji mbona taarifa za ujenzi wa vituo hivi hazitolewi na ni kwanini imekua siri kiasi hicho nao wanarusha mpira kwa uongozi wa wilaya. Hivyo wananchi wanajiuliza, kama vituo hivi haijakamilika, usiri kwenye utoaji wa taarifa za ujenzi wake kwanini uwe siri.
Uongozi wa Wilaya ya Ikungi unatajwa na baadhi ya wananchi umekua na tabia ya kupika na kuficha taarifa pale kunapokuwa na ugeni wa kitaifa kukagua miradi ili waonekane kua ni wasafi na kuficha tabia zao za mashaka. Ni ombi kwa Mama Samia kutuma kikosi chake kwenda kukagua ujenzi wa miradi hiyo, au Wizara ya TAMISEMI nayo ni wajibu wake kufuatilia hali hii ili ikionekana kuna ubadhirifu watu wawajibishwe. Wananchi hawawezi kuendelea kuteseka kwa kukosa huduma za afya kwa sababu ya tabia za watu wachache ambao hawaeleweki.