Ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu Dar es Salaam unahitaji bajeti ya milioni ngapi?

Raja Casablanca

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
706
Reaction score
368
Salaam wakuu,

Kama mnavyojua ndugu zangu ni lazima tuhame kwa wazazi wetu tukaanze maisha. Na kutokana na hayo hatuna budi kufikiria kuwa na makazi yetu.

Uhalisia huo umenifanya niijiulize maswali mengi sana hasa ni gharama kiasi gani zinahitajika kutekeleza ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu na sebule yenye specifications zifuatazo;

Chumba kimoja master bedroom, vyumba viwili self contained. Public toilet moja, jiko, store, dinning, library na sebule.

Kutokana na specifications hizi napenda kujua gharama zake za ujenzi hasa hapa Dar es Salaam ili nijue najichanga vipi.

Nategemea mrejesho wenu wakuu.

Asanteni
 
Million 55 kama tayari unakiwanja mpka kuhamia ila ingependeza ukaeka ramani kabisa ili wataalamu wakusaidie
 
Unataka kuhamia dar wapi? Mjini nje ya mji? Ujenzi wa Buguruni na Temeke haujapishana sana lakini ujenzi wa Gongolamboto na jeti umepishana kidogo na ujenzi wa Ilala na kigamboni bei zake zipo tofauti sana.

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Ukija kuomba ushauri wa ujenzi hapa Jf hapa utatishwa na watu ambao hata bei ya Tofali za tope hawajui.

Watakuambia millioni Sabini utoke hapa umekata tamaa.

Mimi nakushauri kwanza amua standard ya nyumba unayoitaka kisha aanza sasa kufanya planning ya costs utakazotumia.
 
Gharama kubwa ya nyuma itakuwa kwneye finishing ila ukiijenga basic milion 30 inakamilika. Aina ya Finishing ndio itakupeka hadi 60m
 
Kwa kweli swali lako lipo vibaya na tegemea majibu tofauti.
1. Majibu yatatofautia kutokanabna fikra za mjibu swali juu ya ubora wa materials yatakayotumika.
 
Kama hii
FB_IMG_1633000388953.jpg
FB_IMG_1633000384286.jpg
 
Unataka kuhamia dar wapi? Mjini nje ya mji? Ujenzi wa Buguruni na Temeke haujapishana sana lakini ujenzi wa Gongolamboto na jeti umepishana kidogo na ujenzi wa Ilala na kigamboni bei zake zipo tofauti sana.

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
Buyuni au Chanika mkuu
 
Salaam wakuu,

Kama mnavyojua ndugu zangu ni lazima tuhame kwa wazazi wetu tukaanze maisha. Na kutokana na hayo hatuna budi kufikiria kuwa na makazi yetu.

Uhalisia huo umenifanya niijiulize maswali mengi sana hasa ni gharama kiasi gani zinahitajika kutekeleza ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu na sebule yenye specifications zifuatazo;

Chumba kimoja master bedroom, vyumba viwili self contained. Public toilet moja, jiko, store, dinning, library na sebule.

Kutokana na specifications hizi napenda kujua gharama zake za ujenzi hasa hapa Dar es Salaam ili nijue najichanga vipi.

Nategemea mrejesho wenu wakuu.

Asanteni
Hongera sana kwa wazo mtambuka.
Ni njia kubu ya kufikia ndoto yako.

Bro,
Kutaja idadi ya vyumba na migawanyo yote ni sawa, ila ukubwa nao ni chachu mhimu ya utambuzi gharama.

Tunaweza kukutajia mamilioni yanayo husu nyumba usio hitaji ukavunjima moyo au ,hyo unayo tajiwa ukawa nayo kumbe hailingan na nyumba utakayo.

Ushauri wetu UVIMO , kama unataka kujenga kweli, tenga 100,000-150,000 ya ramani itakayo tupa tathimini ili tufanye kitu kwa uhakika.

UVIMO ni kitu gani?
Ni kituo cha huduma kwa wateja wa ujenzi kuanzia ramani hadi kukukabidhi ufunguo.

Kama unatupa kazi, gharama za kuchora ramani, kutathimi hadi kujenga na finishing zote ni nafuu sana.

Wasiliana nasi,
0629361896
0753927572 + Wasap
 
Salaam wakuu,

Kama mnavyojua ndugu zangu ni lazima tuhame kwa wazazi wetu tukaanze maisha. Na kutokana na hayo hatuna budi kufikiria kuwa na makazi yetu.

Uhalisia huo umenifanya niijiulize maswali mengi sana hasa ni gharama kiasi gani zinahitajika kutekeleza ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu na sebule yenye specifications zifuatazo;

Chumba kimoja master bedroom, vyumba viwili self contained. Public toilet moja, jiko, store, dinning, library na sebule.

Kutokana na specifications hizi napenda kujua gharama zake za ujenzi hasa hapa Dar es Salaam ili nijue najichanga vipi.

Nategemea mrejesho wenu wakuu.

Asanteni
We nenda kajenga badala ya kupoteza muda. Kila nyumba ina bei yake. Kila fundi ana bei yake. Kila eneo lina bei yake hata kama Dar ni moja. Kujenga ni uwezo wako wa kufikiri, kusimamia, na fedha bila kusahau kuchagua na kupanga vilivyo.
 
Back
Top Bottom