Ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu Dar es Salaam unahitaji bajeti ya milioni ngapi?

Ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu Dar es Salaam unahitaji bajeti ya milioni ngapi?

Salaam wakuu,

Kama mnavyojua ndugu zangu ni lazima tuhame kwa wazazi wetu tukaanze maisha. Na kutokana na hayo hatuna budi kufikiria kuwa na makazi yetu.

Uhalisia huo umenifanya niijiulize maswali mengi sana hasa ni gharama kiasi gani zinahitajika kutekeleza ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu na sebule yenye specifications zifuatazo;

Chumba kimoja master bedroom, vyumba viwili self contained. Public toilet moja, jiko, store, dinning, library na sebule.

Kutokana na specifications hizi napenda kujua gharama zake za ujenzi hasa hapa Dar es Salaam ili nijue najichanga vipi.

Nategemea mrejesho wenu wakuu.

Asanteni
nichek watsap nikufanyie hesabu na ukadiliaji 0753757303
 
Nenda kajenga mkuu usipoteze muda ukishindwa uza pangala nunua gari tuone kama kuna mtu atakupeleka mahakamani
 
We nenda kajenga badala ya kupoteza muda. Kila nyumba ina bei yake. Kila fundi ana bei yake. Kila eneo lina bei yake hata kama Dar ni moja. Kujenga ni uwezo wako wa kufikiri, kusimamia, na fedha bila kusahau kuchagua na kupanga vilivyo.
Umemshauli vizuri sana!
 
Back
Top Bottom