Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tafadhali tufahamishe kimo kilichopo kati ceiling board na paa/bati.Habari waungwana na wadau wa ujenzi.
Nawajaribisha tushirikiane kujadiliana aina hii ya ujenzi kwa wataalam na wadau wa ujenzi wa aina hii....karibuni
1.Je una changamoto katika ujenzi wa nyumba tajwa hapo juu?
2. Umejengewa nyumba ukakutana na changamoto ya kuvuja?
3. Wewe ni mjenzi na hujui namna ya kujenga kwa usahihi nyumba za kuficha paa?
4. Una ndoto ya kujenga nyumba za aina hii lkn hujui gharama zake?
Niko hapa kutoa ushauri bure kabisa.
View attachment 1803969View attachment 1803971
......................................................................................
Chukua haya yafuatayo;
1. Msingi uinuke
2. Boma liwe na tofali laini 11
3. Baada ya lenta hakikisha unatengeneza sehemu ya kupokelea maji
4. Pawepo na ducts za kupitishia maji na sio bomba
5. Upake bitumen pamoja na mebrane cloth maeneo ya wazi ya kupokelea maji.
6. Epuka slop ndefu za paa bali livunje vunje vipande vipande ili maji yashukie sehemu tofauti
Ukizingatia haya nyumba hii hsivuji na utaifurahia na haina gharama kubwa
Achana nazo fata mkeo anavyopenda hakuna mtu anayejua undani wa hizi nyumba.Dah ndoto yangu hii ingawa mke wangu hazipendi
Fikiria umelala zako usingizi mzito, mvua kubwa inanyesha, ni saa saba usiku alafu inaanza kuvuja na hapohapo umeme unakatika.Wewe na mimi tuko chungu kimoja
Hizi Nyumba nazipenda Sanaaaaa Ila nikisikia huko kuvuja naingiwa nyongo sana
Utakapovujiwa utatengua kauli yako bila kupenda. Unavujiwa saa 8 usiku.Hata mimi naitaka sana Potelea mbali ikivuja mbele kwa mbele
Zinaaminika sana na ni madhubuti.Hapana hizi zilikuwepo zamani ndio zinarudi sasa .
Nyumba za mapaa marefu ndio zinapitwa na wakati kwa sababu hazina jipya kwenye finishing
Weka uzuri na ubaya wa hizo nyumba ili watu wapate kifahamu.Kwa utafiti wangu mdogo nimeufanya, wengi wanaosema hazifai wapo na maneno ya kuambiwa. Hawajawahi hata kujenga hizo nyumba. Ni kama wale wanaokwambia usinunue Nissan haifai kabisa, ukiuliza kama amewahi hata kumiliki utagundua ni maneno ya kijiweni.
Nakubaliana na wanaosema tatizo ni mafundi. Nyumba hizi zinahitaji fundi anayezijua. Tatizo lipo kwa wenye nyumba, unamuamini fundi aliyekufanyia kazi za tofali akuezekee na bati tu kwa sababu gharama amefanya ndogo.
Contemporary ni zaidi ya kuezeka na mafundi wazuri wapo.
Fafanua vizurikama vitu gani? kwan wiring lazim ipite juu ? si hata chin
Kiufupi hakuna fundi anayezimudu kwenye upauaji uezekaji .Mafundi wengi hawawezi kuziezeka japo kwa tamaa zao watakupa moyo na maneno mengiijj, mwisho Wa siku kuvuja kupo pale pale mnaanza kuzungushana. Mafundi wanaozimudu wapo ila ni wachache sana
Hakuna kabisa lazima uwe na elimu ya kutosha.Kuna mtu mwenye kipaji cha kufanya operation ya moyo au operation ya ubongo bila ya kupata kwanza elimu?
Hakuna fundi anayezimudu kupaua au wewe ndio huwajui mafundi mkuu??Kiufupi hakuna fundi anayezimudu kwenye upauaji uezekaji .
Uzuri au Ubaya wa kitu chochote upo kwa mtu anayehitaji hicho kitu. Ndiyo maana pamoja na watu kusikia kwamba nyumba za namna hiyo huvuja sana (Mabaya) lakini hawaachi kujenga.Weka uzuri na ubaya wa hizo nyumba ili watu wapate kifahamu.
kwenye magorofa wiring zinapita wap si chini.kama ynaona wiring juu huwez pitisha bonba chini kwneye floor piga snake wireFafanua vizuri
Jamaa anadhani vyeti ndio kila kitu.. nina watu si chini ya watano nawafahamu hawajamaliza hata darasa la 7 ila ni mafundi wazuri mno mno mno kuliko graduates wengi tuMbona swali lako hili pia ni la kijinga! Kwani elimu ndo inajenga nyumba au ujuzi wa mtu! Hujifunzi kwa mainjia wale wa majengo wanavoharibu kazi na mavyeti yao!
Mkuu komaa kwanza na kujulishwa namna ya kuzuia kuvuja mengine baadae,mana hilo ndio tatizo kuu la hizo nyumba. Nazipenda sana ilazishaanza kunikaatishaa tamaa. Fundi wengi wanaashindwa kuezeka vema, hivyo zinavuja sanaTafadhali tufahamishe kimo kilichopo kati ceiling board na paa/bati.
Wiring ya hizi nyumba kwenye roof hufanyikia wapi ukilinganisha na nyumba za kawaida?