Ujenzi wa nyumba za kuficha paa/contemporary/ hidden roof

Tafadhali tufahamishe kimo kilichopo kati ceiling board na paa/bati.
Wiring ya hizi nyumba kwenye roof hufanyikia wapi ukilinganisha na nyumba za kawaida?
 
Weka uzuri na ubaya wa hizo nyumba ili watu wapate kifahamu.
 
Mafundi wengi hawawezi kuziezeka japo kwa tamaa zao watakupa moyo na maneno mengiijj, mwisho Wa siku kuvuja kupo pale pale mnaanza kuzungushana. Mafundi wanaozimudu wapo ila ni wachache sana
Kiufupi hakuna fundi anayezimudu kwenye upauaji uezekaji .
 
Kiufupi hakuna fundi anayezimudu kwenye upauaji uezekaji .
Hakuna fundi anayezimudu kupaua au wewe ndio huwajui mafundi mkuu??

Tatizo kinachowacost watu ni kutokujua
Hizi nyumba sio kwamba gharama inapungua kama wengi wanavyodhania, ile gharama inayopungua kwenye bati na mbao utaifidia pale kwenye gata, na ikitokea fundi wako amejenga gata la kubana matumizi hapo sasa ndio utavujiwa mpaka akili ikukae sawa.
 
Weka uzuri na ubaya wa hizo nyumba ili watu wapate kifahamu.
Uzuri au Ubaya wa kitu chochote upo kwa mtu anayehitaji hicho kitu. Ndiyo maana pamoja na watu kusikia kwamba nyumba za namna hiyo huvuja sana (Mabaya) lakini hawaachi kujenga.
Ila kwa upande wangu naweza sema, uzuri wa nyumba hizi kwa uchache

1. Zina muonekano mzuri kama mchora ramani yako alikuwa vyema kwenye kuinakshi hiyo ramani na ukapata mtu sahihi wa kufanya finishing.
2. Inaokoa gharama ya mbao kwa kiasi fulani
3. Inaokoa gharama ya bati kwa kuwa bati unayoweka yaweza kuwa ya kawaida kimuonekano lakini ni bati bora.

Ubaya
1. Ni nyumba inahitaji maintainance kubwa zaidi ukilinganisha na aina ingine.

Kumbuka, pamoja na huo unaitwa ubaya wa kuvuja kwa nyumba hizi, hata ukipiga bati kawaida na usipopata fundi mzuri lazima zivuje.

Asante
 
Mbona swali lako hili pia ni la kijinga! Kwani elimu ndo inajenga nyumba au ujuzi wa mtu! Hujifunzi kwa mainjia wale wa majengo wanavoharibu kazi na mavyeti yao!
Jamaa anadhani vyeti ndio kila kitu.. nina watu si chini ya watano nawafahamu hawajamaliza hata darasa la 7 ila ni mafundi wazuri mno mno mno kuliko graduates wengi tu
 
Tafadhali tufahamishe kimo kilichopo kati ceiling board na paa/bati.
Wiring ya hizi nyumba kwenye roof hufanyikia wapi ukilinganisha na nyumba za kawaida?
Mkuu komaa kwanza na kujulishwa namna ya kuzuia kuvuja mengine baadae,mana hilo ndio tatizo kuu la hizo nyumba. Nazipenda sana ilazishaanza kunikaatishaa tamaa. Fundi wengi wanaashindwa kuezeka vema, hivyo zinavuja sana
 
Kuna post moja juzi
Mvua imenyeshaa bati imeshukia ndani
Chumbani kumegeuka bwawa

Nkasema hii style basi tena
Ngja tuendelee na style zinazojulikana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…