Ujenzi wa nyumba za kuficha paa/contemporary/ hidden roof

Kaka hebu nieleweshe wakati naanza ujenzi sikuwaza ujenzi wa namna hii lakini nyumba imefika saiz ya lenta inawezekana nisiezeke bâti?
Paua kawaida tu, nyumba nyingi wanazochange huwa contempo huwa hazina muonekano mzuri
 
Paua kawaida tu, nyumba nyingi wanazochange huwa contempo huwa hazina muonekano mzuri
Inategemea mkuu maana ukiacha mbwembwe zingine,huo muonekano utatafutwa kwa kuezeka mapaa yanayomwaga maeneo tofauti..

Nimeona nyumba ya hivyo haina marembo ya nje ila baada ya ku design mapaa ikawa na muonekano mzuri.

Ishu ya hizo nyumba ni kupata fundi mtaalamu.
 
Kaka hebu nieleweshe wakati naanza ujenzi sikuwaza ujenzi wa namna hii lakini nyumba imefika saiz ya lenta inawezekana nisiezeke bâti?
Inawezekana sana mkuu japo inaweza kuhitaji kuongezea vionjo kidogo.

Ninaomba radhi sikuingia jf muda nilikuwa nje kikazi na mazingira hayakuwa na internet access ya ihakika
 
Kuna post moja juzi
Mvua imenyeshaa bati imeshukia ndani
Chumbani kumegeuka bwawa

Nkasema hii style basi tena
Ngja tuendelee na style zinazojulikana
Tatizo sio muundo bali nani kajenga mkuu.
Si kila anayeitwa fundi anaweza kupaua au kujenga nyumba hii
 
Uko sahihi sana.
Kuna kitu tunaita Duct hii ni muhimu sana tena ziwe zaidi ya 4 hii hupokea maji kutoka gata
 
Unajua sababu ya kuvuja?
 
Fikiria umelala zako usingizi mzito, mvua kubwa inanyesha, ni saa saba usiku alafu inaanza kuvuja na hapohapo umeme unakatika.
Kwanini uvujiwe?

Tatizo wengi mnadharau taaluma za watu mnachozingatia ni bei nafuu huko ndiko mnalizwaga mkuu
 
Unajua sababu ya kuvuja?
Cyanee naomba kama utanisaidia kupata Ka ramani kazuri ka chumba kimoja na choo chake,chumba kikubwa wastani ila kachumba kawe na paa la kuficha kama hilo,ikikupendeza unipe gharama za ujenzi na gharama za nyumba mpaka nahamia.

Kama Mungu akipenda na wewe ukipenda pia nitafurahi ukiwa fundi wangu kwenye hako ka master single room.

Bei ujumuishe kila kitu kuanzia material mpk Ufundi ikikupendeza hapahapa kwa faida ya wengi,ya ufundi ndio unaweza nitumia Inbox kama utaona soo kuiweka hapa.Asante.
 
Ramani nitakuandalia mkuu.
Kuhusu kukujengea zaidi nitakupa ushauri
Utumie fundi wako mkuu.

Na usijali nitakushauri viziri fundi yeyote mwenye akili kwa maelekezo yangu atafanya kazi nzuri kabisa...najijua mimi ni zaidi ya mwalimu katika taaluma hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…