Ujenzi wa Soko la Majengo Dodoma na maswali ninayojiuliza

Undule Lumuli

Member
Joined
Mar 24, 2025
Posts
6
Reaction score
5
Mnamo tarehe 3 Machi, katika pitapita zangu Mitaa ya Majengo nikiwa natoka kazini nilisikia Tangazo (PA) Kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji kuwa kuanzia tarehe 6 Machi wataanza ubomoaji wa Soko la Majengo na kuanza Ujenzi ambao utachukua miezi 12, hivyo baadhi ya Barabara zitafungwa ili kuruhusu wafanyabiashara kuendelea na biashara zao

Zoezi limeanza rasmi ambapo barabara iliyokuwa inaruhusu magari kutoka Roundabout ya Safina kwenda Mipango, Chang'ombe, Nkuhungu, Mnadani nk kufungwa na hivyo kutakuiwa kuzunguka karibu na Ukuta wa Hospitali ya General kisha waendelee na safari

Baadhi ya Stendi za Daladala pia zimebadilishiwa matumizi na kumejengwa vibanda

Mipango ya Serikali ni mizuri kwani siku zote watu wanapisha maendeleo na sio maendeleo yanapisha watu

Maswali ya kujiuliza ni
Je Serikali haikujipanga kutafuta eneo la wazi ili kuwahamishia wafanyabishara hawa kwa muda wakati wakisubiri Soko kujengwa? Kwani kwa sasa imekuwa ni kama uchafu na vurugu katikati ya miji vibanda (temporary) vimejengwa hadi kwenye njia za watembea kwa miguu barabara ya mchepuko ni finyu kiasi kwamba magari kupishana ni mtihani jambo linalosababisha foleni

Je, wafanyabiashara hawa watakuwa hapa kwa muda gani, au masuala ya uchaguzi yakipita wataondolewa maana kwa sasa wapiga kura hawabugudhiwi, what if kama ujenzi utaenda zaidi ya miezi 12 hivi vibanda vitaendelea kuwa hapo?

Je, miundombinu ya huduma za kijamii zipo za kutosha kuhudumia idadi hiyo kubwa kwa kuvunja soko zima kwa mara moja?

Kwani jambo hili lilikuwa la dharura au lililikuwa kwenye Mpango Mkakati?

Lakini Wahusika hawaoni hatari kwa watu kuendelea kujenga vibanda wakati huo huo kuna watu wanafanya biashara chini, na baadhi ya akina mama wana watoto wadogo?

Jamani Dodoma, Dodoma Fahari yetu eeee

IMG_20250327_174808_290.jpg

IMG_20250327_174648_495.jpg

IMG_20250327_180125_118.jpg
 
View attachment 3285279
View attachment 3285280
View attachment 3285281
Si wahamie Soko la Ndugai,liko tupu?!
 
Back
Top Bottom