Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Iringa wafikia asilimia 93 ukigharimu bilioni 68, rasmi kuanza kutumika Februari 22, 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Iringa, ulio katika Kata ya Nduli, Mkoani Iringa, umefikia asilimia 93 ya ukamilifu na umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 68. Kwa sasa, uwanja huo uko tayari kwa matumizi, huku safari za ndege kubwa zikitarajiwa kuanza rasmi tarehe 22 Februari 2025.

Hayo yamebainishwa leo, Februari 7, 2024, wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo ,Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, amesema kuwa uwanja huo utaanza kupokea ndege kubwa, ikiwa ni pamoja na ndege ya aina ya Bombardier.

"Ujenzi huu wa kisasa utafungua milango ya maendeleo kwa uchumi wa Iringa pamoja na uchumi wa nchi yetu, kwani utaongeza idadi ya watalii na shughuli nyingine za kiuchumi," alisema Mbarawa.

Kwa upande mwingine, Waziri Mbarawa ameeleza kuwa zamani wageni walikuwa wakitoka Zanzibar na kwenda moja kwa moja kwenye mbuga za wanyama, lakini sasa wataweza kutumia uwanja huu kuja Iringa na kuendelea na shughuli zao za utalii.

"Zamani, usafiri wa ndege kutoka Dar es Salaam hadi Iringa ulikuwa unafanyika kwa ndege ndogo, na gharama yake ilikuwa shilingi laki 700,000. Hata hivyo, kutokana na ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya uwanja huu, sasa abiria wataweza kusafiri kwa gharama ya shilingi laki 250,000 hadi laki 300,000."Alisema Waziri

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dr. Linda Selewa, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa amesema kuwa wananchi wa Iringa wanashukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za kukamilisha mradi huu, kwani utaongeza ukuaji wa uchumi katika mkoa wa Iringa na kutoa fursa za ajira kwa wananchi.

Meneja wa Kiwanja cha Ndege Iringa, Ashraph Mohamed, amesema kuwa kukamilika kwa mradi huu kutachochea ongezeko la shughuli za usafiri wa ndege na abiria, na pia kutachangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa ujumla.

Hata hivyo kukamilika kwa uwanja huu, Iringa Kwa sasa itakuwa na fursa ya kuongeza usafiri wa ndege na kuhamasisha ukuaji wa sekta mbalimbali za kiuchumi katika mkoa hapa.
1738947745540.jpg
1738947725926.jpg
 
View attachment 3228102View attachment 3228104
Machadomo yatanuna na kusema SSH hajafanya chochote
 
Hivi Arusha wameanza kujenga uwanja wa ndege au palikua hakuna mpango huo
 
Tatizo bei za ndege zimekuwa kubwa sana sielewi kwa nini? mfano wakiweka bei ya kawaida halafu ndege ikapiga tripu hata 5 au zaidi kwa siku kutokana na kuzidiwa na abiria kuna ubaya gani? Kuliko kuweka bei kubwa halafu zinasafiri tupu,Au ndiyo ushamba tuliokuwa nao sababu Viongozi wanatoka katika famiria za kimasikini kiasi kwamba wanachukulia kama usafiri wa ndege ni anasa?
Niko kwenye hii inchi yaani ndege ni kitu cha kawaida sana kiasi kwamba mfanyakazi wa ndani anakatiwa tiketi ya ndege.Michezo ya umishuta kama Tanzania,hapa vijana huwa wanapandishwa ndege kutoka jimbo moja kwenda jingine na ni maelfu ya vijana,jiulize ndege zinapiga tripu ngapi? Yaani mfano mashindano yafanyike mwanza halafu kila mkoa utoe vijana wanaoshiriki michezo ya aina yote kuanzia kutoka mtwara na mikoa yote wapelekwe mwanza na kuludishwa,lakini kwetu ni ndoto ila Viongozi ndiyo wanaweza kujipa maisha ya starehe na kufuru siyo kwa wanainchi wake
 
Kwa Iringa nauli zimekuwa nafuu mno return ticket ni 390k
 
Kwa iringa nauli zimekuwa nafuu mno return ticket ni 390k
Piga hesabu kwa familia, baba mama na mtoto, toa na mshahara wako, au wewe ndiyo wale wanaolipiwa na serikali?
 
Piga hesabu kwa familia,baba mama na mtoto,toa na mshahara wako,au wewe ndiyo wale wanaolipiwa na selikari?
Silipiwi na serikali ila kwa mshahara wangu namudu ndege mimi tu sio na familia ingawa kazini wananilipia.
 
Hongera Kwa Serikali kukamilika Mradi huu.

Nimeona Shirika la Ndege la Precision Air wamenitumia taarifa, kwamba wameanzisha route ya Iringa

Screenshot_20250207-220723.png
 
Back
Top Bottom