Maoni, serikali iruhusu halmashauri za wilaya, manispaa au jiji kama zinajiweza basi zijenge viwanja vya mpira ili kuendelea kukuza vipaji vya soka na kuendelea kutusahaulisha shida nyingine za maisha humu Tanzania. Au serikali kuu yenyewe ijenge viwanja vidogo vidogo sehemu mbalimbali nchini. Viwanja hivyo viwe vinakodishwa kwa bei nafuu kwa timu mfano za ligi daraja la kwanza
Tuachane na mpango wa kuvikarabati vile viwanja vya chama kile au virudishwe serikalini ndipo vikarabatiwe na viwe vinakodishwa kwa bei ndogo japo vingine vimeishachoka sana na kuwa magofu baada ya kutelekezwa na chama kile, wao ni kukusanya mapato tu ya frame za biashara katika viwanja vyao.
Nimekiona kiwanja cha Manispaa ya Kinondoni kumbe inawezekana tukawa na viwanja vya mashabiki wachache tu mfano elfu 15 au 20 katika mikoa mbalimbali ili kukuza soka. Pia viwanja vidogo ni rahisi kuvifanyia ukarabati.
Hata ukitazama ligi mfano za Italia, viwanja vingine ni vidogo tu kama cha Azam.