Taasisi ya Mifupa-MOI
Senior Member
- Apr 15, 2025
- 118
- 214
Ujenzi wa wodi mpya ya Wagonjwa Mahututi (ICU) kwa ajili ya watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) umefikia asilimia 98, hatua inayotarajiwa kuboresha huduma za kibingwa na kibobezi kwa watoto wenye uhitaji wa uangalizi maalum.
Akizungumza leo januari 15, 2026 MOI, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema kukamilika kwa mradi huo utasaidia kuongeza uwezo wa taasisi kuhudumia watoto bila kuwachanganya na watu wazima kwani wana mahitaji maalum.
“Kukamilika kwa wodi hii ya ICU ya watoto ni hatua muhimu katika kuboresha huduma za kibobezi kwa watoto nchini... Wodi hii itakuwa na uwezo wa kubeba vitanda 20, ikiwa na vifaa tiba vya kisasa pamoja na mazingira rafiki kwa watoto ,” amesema Dkt. Mpoki
Ameongeza kuwa kukamilika kwa wodi hiyo kutaongeza uwezo wa MOI kuhudumia idadi kubwa zaidi ya watoto kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, sambamba na kupunguza rufaa za nje ya nchi.
Kwa upande wake, Meneja Mazingira, Milki na Matengenezo MOI, Bw. Victor Kamagenge amesema ujenzi umefikia hatua za mwisho ambapo kazi zilizobaki ni pamoja na ufungaji wa baadhi ya vifaa tiba, majaribio ya mifumo ya umeme pamoja na hewa tiba.
Mradi huo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha miundombinu ya afya na kuongeza upatikanaji wa huduma za kibingwa na kibobezi kwa wananchi, hususani watoto wanaohitaji matibabu ya hali ya juu.