Kombe la Dunia - Russia 2018, linatarajia kuanza nchini humo wiki ijayo. Kuna baadhi ya Timu maarufu kwa soka zinapewa nafasi kubwa ya kushinda Kombe hilo kwa mwaka huu. Timu hizo ni: Brazil, Hispania, Ujerumani na Ufaransa.
Hata hivyo, Mimi naweka kamari yangu kwa Ujerumani kutetea Kombe hilo licha ya kwamba, tangu Italia ya Giuseppe Meazza ifanye maajabu hayo mwaka 1934 & 1938, ikifuatiwa na Brazil ya akina Garincha na Pele, mwaka 1958 & 1962, yameshachezwa mashindano 13, sawa na miaka 56 bila Timu yoyote kutetea tena Kombe hilo, licha ya Argentina ya Diego Maradona kulikosa kosa mwaka 1990 kwa Ujerumani ambao iliwafunga mwaka 1986.
Unadhani nani ana nafasi ya kuchukua Kombe?