Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema hii leo kwamba sserikali kuu na zile za majimbo wamekubaliana kuhusu rasimu ya mapendekezo ya kuweka hatua kali za kujaribu kudhibiti wimbi la maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.
Hatua hizo ni pamoja na kufungwa kwa maduka mengi kuanzia siku ya Jumatano wiki ijayo hadi Januari 10.
Kadhalika viongozi wa serikali za majimbo na kansela Merkel wamekubaliana kimsingi kwamba shule zote zitafungwa katika kipindi chote hicho na waajiri watatakiwa kufunga shughuli zao au kukubali wafanyakazi wafanyie kati majumbani. Uuzaji wa fataki zinazotumiwa wakati wa kipindi cha mwaka mpya umepigwa marufuku.
Kiwango cha maambukizi nchini Ujerumani kila siku pamoja na vifo imefikia rekodi ya juu katika siku za karibuni na wanasiasa wengi wamekuwa wakitowa tahadhari.
Data za taasisi ya kushughulikia magonjwa ya kuambukiza nchini Ujerumani ya Robert Koch leo jumapili zimeonesha kwamba idadi ya maambukizi imeongezeka kwwa watu 20,200 na kufikia watu 1,320,716.
Chanzo: DW Swahili