Mwanamkiwi
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 2,023
- 2,402
Karamba Diaby alishinda jimbo la Halle (Saale) kwenye uchaguzi mkuu nchini Ujerumani tarehe 26 Septemba.
Dk Karamba alizaliwa Senegal akafika Ujerumani akiwa mwanafunzi mnamo mwaka 1986. Baada ya kuhitimu shahada ya uzamivu ya kemia alianza kujihusisha na siasa akajiunga na Chama cha Kijamaa-Kidemokrasia cha Ujerumani (SPD) na tangu mwaka 2013 amekuwa mbunge wa kitaifa kupitia orodha ya chama chake (wabunge wanaoingia kufuatana na asilimia za kura za chama). Wakati ule alikuwa mbunge wa kwanza Ujerumani aliyezaliwa Afrika.
Mwaka huu alifaulu mara ya kwanza kushinda moja kwa moja jimbo la uchaguzi la Halle kwa asilimia 28.8 (mgombea aliyemfuata alipata % 20).
Soma habari zake: