Ujerumani, Tanzania wazindua Kituo cha Taarifa cha Serengeti

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
1.jpg

SERENGETI. Tanzania na Ujerumani leo wamezindua rasmi Kituo kipya cha Taarifa cha Serengeti baada ya kukarabatiwa, hatua inayolenga kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo katika uhifadhi wa bayoanuwai, utalii endelevu na maendeleo ya jamii zinazozunguka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Kituo hicho kinawapa wageni fursa ya kujifunza kuhusu ikolojia ya Serengeti, historia yake na uhamaji wa wanyamapori unaofanyika kila mwaka, huku kikieleza umuhimu wa uhifadhi na mchango wa jamii zinazozunguka mfumo wa ikolojia wa Serengeti.

Kituo hicho kina Ukumbi wa Uhifadhi (Conservation Hall), Ukumbi wa Historia na Uhamaji (History and Migration Hall), Watu Pavilion pamoja na Njia ya Uhamaji (Migration Walkway).

2.jpg

Ujerumani imetoa takribani Euro milioni 1.3, sawa na Sh bilioni 3.9, kupitia Benki ya Maendeleo ya KfW kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho.

Tangu mwaka 2013, Ujerumani imetoa takribani Euro milioni 67, sawa na Sh bilioni 203, kupitia KfW kwa ajili ya shughuli za uhifadhi na maendeleo ya jamii katika mfumo wa ikolojia wa Serengeti.

Balozi Mteule wa Ujerumani nchini Tanzania, Annett Günther, amesema kituo hicho ni mfano wa ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Ujerumani katika kulinda urithi wa asili wa Tanzania.

“Serengeti ni urithi wa asili wa Tanzania, na Ujerumani inajivunia kusimama pamoja na Tanzania katika kuilinda. Kituo hiki ni mfano unaoonekana wa ushirikiano wetu wa muda mrefu katika uhifadhi, maendeleo ya jamii na utalii endelevu,” amesema Günther.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamad Hassan Chande (Mb), amesisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano katika kulinda Serengeti na kuhakikisha sekta ya utalii inakua kwa kuzingatia misingi ya uendelevu.

Mbali na uwekezaji katika uhifadhi, ushirikiano wa Tanzania na Ujerumani kupitia miradi ya Serengeti unalenga pia kuboresha maisha ya jamii zinazozunguka hifadhi hiyo.
3.jpg

Maeneo yanayonufaika ni pamoja na miundombinu, afya, elimu, shughuli mbadala za kiuchumi na hatua za kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori.

Ushirikiano huo una historia ndefu. Mwaka 1957, mtaalamu wa wanyama kutoka Ujerumani, Bernhard Grzimek, pamoja na mtoto wake Michael, walifika Serengeti.

Filamu na kitabu chao cha mwaka 1959, Serengeti Shall Not Die, vilisaidia kuitangaza Serengeti kimataifa na kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kulinda mfumo huo wa ikolojia.

Kituo hicho kimejengwa kupitia ushirikiano wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Serikali ya Ujerumani kupitia KfW Development Bank, Frankfurt Zoological Society na wadau wengine wa uhifadhi.

Uzinduzi huo unatarajiwa kuongeza uelewa wa wageni kuhusu thamani ya Serengeti, huku ukisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, washirika wa maendeleo na jamii katika kuhakikisha rasilimali za asili zinalindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
 
View attachment 3686032

View attachment 3686033

View attachment 3686034

well done Federal Republic of Germany & The Government of United Republic of Tanzania that development project :NoGodNo:
 
Back
Top Bottom